mwita ke mwita
JF-Expert Member
- Aug 13, 2010
- 7,922
- 3,618
So Abiria watalala njiani maskini
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
sasa mbona boda boda ndio kaigonga gari , gari ipo kwenye njia yakeHabari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa kundi la waendesha bodaboda, leo Februari 27, 2024 wamelichoma moto na kuliteketeza basi linalodaiwa kuwa ni mali ya Kampuni ya Saibaba, lililokuwa linatoka jijini Dar es Salaam kuelekea Arusha, baada ya kudaiwa kumgonga bodaboda mmoja na kusababisha kifo chake.
Habari zilizotufikia hivi punde, zimeeleza kuwa tukio hilo limetokea katika eneo la Kona ya Semkiwa, Korogwe mkoani Tanga na kusababisha kukatika kwa mawasiliano kati ya pande mbili za barabara hiyo, jambo lililosababisha foleni iliyodumu kwa takribani saa mbili.
Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya ajali iliyosababisha kifo cha mwendesha bodaboda, wenzake walijikusanya na kulizingira basi hilo, wakawaamuru abiria wote kushuka na kushusha mizigo yao kabla ya kuliteketeza kwa moto.
Wakibaki hakuna rangi wataacha kuona!Hao boda boda nawashauri wakimbie
Wana mwita mwalimu "nilisikia sehemu"Hasira
hao waendesha bodaboda ni wajeuri barabarani hawajali wanaingia barabarani vile wanataka wakipata ajali wanadai wanaonewa na magari inatakiwa wachapwe hasa maana ajali nyingi wao ndio sababuHao ni waalifu kama waalifu wengine wakamatwe na washtakiwe tabia nyingine sio za kuzivumilia kuna siku watakamata gari la kiongozi na kulichoma.
Basi la Kampuni ya Sai Baba linalofanya Safari kutoka Dar es Salaam kuelekea Mkoani Arusha limeteketezwa kwa Moto mara baada ya kusababisha Ajali kwa kumgonga Dereva wa Bodaboda na kudaiwa kusababisha kifo kwa dereva huyo wa Bodaboda katika eneo la Msambiazi wilayani Korogwe mkoani Tanga leo Februari 27, 2024.
Waendesha Pikipiki (Bodaboda) katika eneo hilo wamejichukulia sheria mkononi mara baada ya kushuhudia ajali hiyo ikitokea kwa kulichoma basi hilo moto kwa kutumia mafuta ya Petroli.
View attachment 2918376View attachment 2918378View attachment 2918377
Hakuna cha kujichokea wala nini, yaani boda wanavuta bangii na mipombe mikali balaa. Wenye unafuu na rika fulani lenye familia na hata vijiweni hawachangamani.Watu washajichokea mkuu
No E ni boda boda sio gariSaibaba na magari yake mabovu kadunduliza kapata namba E wamechoma? Hawa sio watu
Yani hao wahuni sjui watajificha wapi.Ikithibika kwamba bodaboda ndio waliochoma hilo basi nashauri vijiwe vya boda vilivyopo karibu na eneo la tukio wajipe likizo au watafute pahala pengine pa kufanyia shughuli zao kwa muda.
Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
Mkuu usiombee hivyo hayo majamaa mapuuzi sana sijui yanavutaga bangi? Yanaweza kukudhibiti yakakuchoma pamoja na gari! Kuna jirani yetu mtaa wa tatu yalimpiga mawe mpaka kupelekea kifo chake! Kosa alilolifanya ni kutoa bastola na kupiga hewani baada ya dereva kuchoropoka!Hao wapuuzi sana. Juzi kuna mmoja kaja kunigonga mi nikiwa na gari. Jamaa nimemuona toka mbali akikimbiza pikipiki pamoja na kumpungia mkono kuashiria apunguze mwendo bado kaja nivaa.
Siku wakinigonga na kujifanya kutaka choma gari au nipiga mawe, mtasikia jamaa kaua Bodaboda 20 kwa kuwagonga na gari. Mapuuzi sana, hayajui sheria yenyewe ni kukimbia na kujichomeka kila sehemu.