Korogwe: Bodaboda wadaiwa kuchoma basi la Saibaba baada ya mwenzao kugongwa

Korogwe: Bodaboda wadaiwa kuchoma basi la Saibaba baada ya mwenzao kugongwa

Ikithibika kwamba bodaboda ndio waliochoma hilo basi nashauri vijiwe vya boda vilivyopo karibu na eneo la tukio wajipe likizo au watafute pahala pengine pa kufanyia shughuli zao kwa muda.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
Sio likizo tu wahame ila haitowasaidia watakamatwa kama kuku
 
Basi la Kampuni ya Sai Baba linalofanya Safari kutoka Dar es Salaam kuelekea Mkoani Arusha limeteketezwa kwa Moto mara baada ya kusababisha Ajali kwa kumgonga Dereva wa Bodaboda na kudaiwa kusababisha kifo kwa dereva huyo wa Bodaboda katika eneo la Msambiazi wilayani Korogwe mkoani Tanga leo Februari 27, 2024.

Waendesha Pikipiki (Bodaboda) katika eneo hilo wamejichukulia sheria mkononi mara baada ya kushuhudia ajali hiyo ikitokea kwa kulichoma basi hilo moto kwa kutumia mafuta ya Petro
daaahhh,mbona boda mmefika mbali sana
 
Kwakua ,Masikini Hana Haki katika mahakama zetu, sana sana Mmliki wa Bus Hilo bado angetafuta kunyonya Ndugu wa marehem, yaaan umegonga, umeuua, na Bado ulipwe fidia wewe.

Niwapongeze Bodaboda Kwa Hatua hii nzurii na ushirikiani wao Hadi kufanikisha Kuchomwa na kuteketea teketeke Kwa Bus hili

Ndiooo masikini tuna Roho mbaya😅👌

Pumzika Kwa Aman Degree Holder, ulosomeshwa, Ajira hamna, ukaamua kujiajiri na sasa umeondoka.
 
Maua upewe
 
Sawa hao bodaboda wamekosea kuchoma hilo basi ila madereva wa mabasi ni washenzi sana yaani wanacheza rafu barabarani hatari. mimi nikiona basi naweka chombo yangu pembeni namuachia njia nyeupe.
kweli kabisa, wana vurugu za speed bila kuangalia wako wapi
 
Hao wapuuzi sana. Juzi kuna mmoja kaja kunigonga mi nikiwa na gari. Jamaa nimemuona toka mbali akikimbiza pikipiki pamoja na kumpungia mkono kuashiria apunguze mwendo bado kaja nivaa.

Siku wakinigonga na kujifanya kutaka choma gari au nipiga mawe, mtasikia jamaa kaua Bodaboda 20 kwa kuwagonga na gari. Mapuuzi sana, hayajui sheria yenyewe ni kukimbia na kujichomeka kila sehemu.
oya ilishatokea kigamboni jamaa aligongwa na bonda taa za nyuma zikapasuka alikua na crown boda akataka kusepa jamaa akampelekea ngoma basi boda wakaanza kumkimbiza alikua anawafuta anakimbiza anawasubiri wakitaka kumpita anawapeleka mtaroni tukio lilikua usiku road ya kutoka mikadi mpka mji mwema kile kipande watu walilazwa sana mtaroni ....
jamaa wa crown alitoa sadaka maana kagongwa akaona bora apeleke moto nilikua naenda ferry tukio lilikua kama movie ilibidi niingie lembeni ya barabara kupisha maana nilikua naona toka mbali wanavyopigwa pembeni
 
Basi la Kampuni ya Sai Baba linalofanya Safari kutoka Dar es Salaam kuelekea Mkoani Arusha limeteketezwa kwa Moto mara baada ya kusababisha Ajali kwa kumgonga Dereva wa Bodaboda na kudaiwa kusababisha kifo kwa dereva huyo wa Bodaboda katika eneo la Msambiazi wilayani Korogwe mkoani Tanga leo Februari 27, 2024.

Waendesha Pikipiki (Bodaboda) katika eneo hilo wamejichukulia sheria mkononi mara baada ya kushuhudia ajali hiyo ikitokea kwa kulichoma basi hilo moto kwa kutumia mafuta ya Petroli.

View attachment 2918376View attachment 2918378View attachment 2918377
Wakikamatwa wakalipe watauziwa hadi viwanja vya babu zao
 
jamaa mwingine alitaka kusababisha ajali lakini haikutokea akashuka akaomba msamaha boda wakaona wanamuweza wakazuia gari yake jamaa akaona hakuna tena amani gari imeanza kupigwa bodi inagongwa gongwa akafungua kioo akapiga ngoma juu mbili tu boda walitawanyika nilicheka sana siku hiyo japo jamaa alikua msataarabu ila boda wakaona sio kweli hatimaye wakatawanywa 😂😂😂😂

kuchukua sheria mkononi kwa boda ni kawaida sana wanahasira za ghafla wanaona kama kundi linaloonewa sana inabidi serikali wairasimishe hii kazi na waweke misingi ya kuwabana vituko ni vingi na wengi wanaishia kuumia hata kwenye sheria bado wanaumia...

unakuta boda kakugonga hata leseni hana hiyo bima ndio hajui inarangi gani mambo ni mengi ila serikali iache kuwatumia kipindi cha uchagizi wawarasimishe watu wafanye kazi
 
Basi la Kampuni ya Sai Baba linalofanya Safari kutoka Dar es Salaam kuelekea Mkoani Arusha limeteketezwa kwa Moto mara baada ya kusababisha Ajali kwa kumgonga Dereva wa Bodaboda na kudaiwa kusababisha kifo kwa dereva huyo wa Bodaboda katika eneo la Msambiazi wilayani Korogwe mkoani Tanga leo Februari 27, 2024.

Waendesha Pikipiki (Bodaboda) katika eneo hilo wamejichukulia sheria mkononi mara baada ya kushuhudia ajali hiyo ikitokea kwa kulichoma basi hilo moto kwa kutumia mafuta ya Petroli.

View attachment 2918376View attachment 2918378View attachment 2918377
Haki ikikosekana mahakamani, yanayofuata ni haya.
 
Kwahiyo hapa abiria wakashuka wakala pembeni wakishudia Maafisa Ubashiri wakifanya Yao, mpaka wanashusha mizigo hakuna hata alieonyesha juhudi ya kuita polisi maana pale Msambiazi ni hatua chache toka Korogwe stand wangeweka road block Kwa boda zote zinazotoka Msambiazi labda kama waamue kwenda Mombo nako wangekamatwa
 
Back
Top Bottom