Nilikula Stiki za mama hadi basiii!!!nilikuwa mtoto mbishi na mtukutu sanaaaa!!Nikitumwa dukani lazima nianze kunung'unika kwanza na kujiliza kwanini natumwa mimi tu na kaka yangu yupo amekaa tu?!Yaani niende dukani halafu nirudi nioshe vyombo kweli hiyo haki?!mama ananitembezea fimbo na vyombo nitaosha[emoji23][emoji23][emoji23]
Kwetu ilikuwa karibu na bahari basi mi kuogelea ndio zangu,nikirudi shule tu najifanya kwenda madrasa kumbe tunaenda kuogelea baharini[emoji23]madrasa siendi..
Kwetu tumezaliwa mimi tu ndio wakike kwa mama,wengine ni wanaume.Lakini niliwazidi ukorofi,nimeshapigana na kaka zangu wote[emoji23]!
Nakumbuka kuna siku nilitumwa nikanunue maziwa mwezi wa ramadhani,ilikuwa saa kumi jioni na hapakua mbali na home,kama dakika 7 tu kwa mwendo wa miguu!!kufika njiani nikakuta wenzangu wanacheza rede,nami nikajiunga,cheza rede mpaka saa kumi na mbili jioni,kufika kwenye maziwa yameisha!narudi home nakuta watu wameshafuturu tayari halafu kulikuja wageni,wallah nilichapwa na baba(R.I.P) sitosahau[emoji23][emoji23]!asubuhi yake niliamka nikakusanya nguo zangu na viatu nikawaaga kwamba nahama!!naenda kuanza maisha mwenyewe,wakati huo nina miaka 11,mama alichekaaa[emoji23][emoji23],akaniambia safari njema mwanangu nakutakia maisha mema uendako!!
Nikaenda kwashangazi yangu(R.I.P) Kukaa,nikamuuliza shangazi hivi yule ni mama yangu mzazi kweli?!mbona ananipiga sana?!mbona kakazangu hawapigwi?!halafu mbona sijafanana na ile familia mimi pekeyangu ni mwembamba wao wote wanene mpaka kakazangu?![emoji23]
Jioni baba akanifata na pikipiki na kunirudisha home(baba alikuwa mpole sana,mpaka akishika fimbo ujue umepitiliza,Rip daddy[emoji24][emoji24])
Naomba mungu nisizae watoto wakorofi kama mimi[emoji38]!
Ahsante sana mama kwa fimbo zile,sasa hivi naona matokeo yake!!nakupenda saaaana,sasa hivi ni rafiki yangu mkubwa[emoji23][emoji23]