Kosa gani ulimfanyia mama yako hadi likasababisha akuchape au kukuadhibu?

Kosa gani ulimfanyia mama yako hadi likasababisha akuchape au kukuadhibu?

Kuchelewa kurudi home mkuu..nilikuwa nachezea stiki za kutosha
 
Mama yangu ni mpole sanaaa! Ata kumfanyia kosa utaona aibu. Ila kuna siku aliniudhi nikamnunia... Nikaenda kwenye migomba na kukaa huko mpaka giza likaingia. Baba aliporudi mama akanisemelea eti nimemnunia sababu amenisema (ata sikumbuki alinisema nini)... Baba akaja kunisema zaidi. [emoji1][emoji1] eti kwa nini unamliza mama yako? Akanitaka nikaombe msamaha. Nikaenda kishingo upande na kweli nikamkuta mama macho mekunduu huku anajishughulisha jikoni. Akawa hanitumi kumsaidia chochote... Nikapiga magoti kumuomba msamaha, na kujiliza juu ndo akarudi katika hali ya kawaida.
Asee hata mimi ishanitokea,ivo...unakuta sometimes wew ndio umemuudh mama then unakasirika,au kununa wew afu mama badae anaamua kwenda kushtaki kwa baba il mambo yaishe,nyie mama anaupendo mkubwa sana kwa mwanae acha tu.
 
Saana! Yaani sasa ivi sipendi kumuudhi kabisa! Ukimuudhi tu analia!
 
Niliiba hela nikaenda movie, tivoli mwanza,nilichezea kichapo cha mbwa
 
Nilikula Stiki za mama hadi basiii!!!nilikuwa mtoto mbishi na mtukutu sanaaaa!!Nikitumwa dukani lazima nianze kunung'unika kwanza na kujiliza kwanini natumwa mimi tu na kaka yangu yupo amekaa tu?!Yaani niende dukani halafu nirudi nioshe vyombo kweli hiyo haki?!mama ananitembezea fimbo na vyombo nitaosha[emoji23][emoji23][emoji23]

Kwetu ilikuwa karibu na bahari basi mi kuogelea ndio zangu,nikirudi shule tu najifanya kwenda madrasa kumbe tunaenda kuogelea baharini[emoji23]madrasa siendi..
Kwetu tumezaliwa mimi tu ndio wakike kwa mama,wengine ni wanaume.Lakini niliwazidi ukorofi,nimeshapigana na kaka zangu wote[emoji23]!

Nakumbuka kuna siku nilitumwa nikanunue maziwa mwezi wa ramadhani,ilikuwa saa kumi jioni na hapakua mbali na home,kama dakika 7 tu kwa mwendo wa miguu!!kufika njiani nikakuta wenzangu wanacheza rede,nami nikajiunga,cheza rede mpaka saa kumi na mbili jioni,kufika kwenye maziwa yameisha!narudi home nakuta watu wameshafuturu tayari halafu kulikuja wageni,wallah nilichapwa na baba(R.I.P) sitosahau[emoji23][emoji23]!asubuhi yake niliamka nikakusanya nguo zangu na viatu nikawaaga kwamba nahama!!naenda kuanza maisha mwenyewe,wakati huo nina miaka 11,mama alichekaaa[emoji23][emoji23],akaniambia safari njema mwanangu nakutakia maisha mema uendako!!

Nikaenda kwashangazi yangu(R.I.P) Kukaa,nikamuuliza shangazi hivi yule ni mama yangu mzazi kweli?!mbona ananipiga sana?!mbona kakazangu hawapigwi?!halafu mbona sijafanana na ile familia mimi pekeyangu ni mwembamba wao wote wanene mpaka kakazangu?![emoji23]
Jioni baba akanifata na pikipiki na kunirudisha home(baba alikuwa mpole sana,mpaka akishika fimbo ujue umepitiliza,Rip daddy[emoji24][emoji24])
Naomba mungu nisizae watoto wakorofi kama mimi[emoji38]!

Ahsante sana mama kwa fimbo zile,sasa hivi naona matokeo yake!!nakupenda saaaana,sasa hivi ni rafiki yangu mkubwa[emoji23][emoji23]
 
Ule ukauzu wa mabimkubwa wetu ukiu apply kwa kizazi hiki jela inakuita maana kulikuwa na vile visosi vya udongo vigumu hivi kuna siku dogo kamkorofisha bimkubwa basi alikirusha kile kama wale jamaa wa olimpic dogo akainama kikachimba ukuta nacho kikameguka kidogo.
 
Mara kwa mara kabla sijaanza shule, washkaji zangu nyumba za jirani walikuwa wananialika kwa breakfast na lunch, bahati mbaya Mama yangu akatafsiri vibaya kwamba "nakula kwa watu" [emoji3] mpaka leo at 20's ukinialika lunch nafikiria mara 2, sio kwa fimbo zile za miaka ya 90.
 
hahah...bhas si kwa kichapo achokupa mama siku izooo ase.
 
Mim nilipoteza mbuzi zikala mashamba ya watu mama akalipa weeeeee hahaha ile fimbo maarufu ya kuchungia mbuzi ilinirudia
 
Ule ukauzu wa mabimkubwa wetu ukiu apply kwa kizazi hiki jela inakuita maana kulikuwa na vile visosi vya udongo vigumu hivi kuna siku dogo kamkorofisha bimkubwa basi alikirusha kile kama wale jamaa wa olimpic dogo akainama kikachimba ukuta nacho kikameguka kidogo.
hahaha....mama yenu alikuwa kauzu mbayaa ase,ulipona sana bhas vipigo ivooo
 
Mim nilipoteza mbuzi zikala mashamba ya watu mama akalipa weeeeee hahaha ile fimbo maarufu ya kuchungia mbuzi ilinirudia
hhaha...pole mkuu,kweli inakuaga ivo ukipoteza mali ya watu mama au baba atalipa vizur tuu ila anaenda kukupa kipigo homee hatar...sema mi nilipona mana nishaga pasua kioo kwa nyumba ya watu nikiwa najarbu kumbonda na jiwe ndege alikuwa kwenye maua,ase nikaenda home kuwaambia,huku nikiwa na wasi2 kweli yani kwamba siku iyo nafwaa kwa chapo...good luck baba na mama nikakuta wamelipa kioo cha watu kiroho safi hata hawakuniadhibu wala kunisema.
 
kuna siku nikiwa mbeya tulikwenda na mother kusaka kuni. mimi nilikuwa kiburi sana nadhani. nilikuwa nyuma katika msafara wa kurudi na kuni kichwani. nikadhani wamenionea wamenibebesha kuni nyingi. basi nikaamua kuzitua na kuanza kuwafuata. kilichofuata baada ya kufika maskani nakijua mwenyewe
 
hahaha...nadhani mama alikupa ulichostahili ase......
 
Back
Top Bottom