Kosa gani unalijutia hadi leo?

Una roho mbaya Sana wewe mwanaume....kwani mtoto Ni mwanamke anajitungishia mwenyewe tumboni au......shame on you
 
Vipi hapo awali alishabahatika kuzaa
 
Katika maisha jifunze Sana kuwa chanya ...Matatizo yapo kutujenga hivo njia pekee ya kutoboa ni kulitafutia ufumbuzi tatizo husika malalamiko hayajengi
 
Kwa mtizamo wangu naona kosa liko kwako na sio mwanamke , kwasababu maelezo ulioyasema ni vitu ambavyo viko nje yauwezo wa binaadamu ni kweli tunatafuta tiba ni kweli tunatafuta rizki ila mtoaji ni mungu na sio mtu . Ikiwa Leo hii kutokuzaa kwake imekua kosa kutokupona kwake kwako imekua mzigo we muite tu na umueleze ukweli kwamba mke wangu mimi nimekuchoka sikutaki kwasababu huzai na wala huponi matatizo yako ,na toka niko na wewe maisha yangu yameharibika hivyo tuachane .nenda kachukue hao uliozaa nao mmoja wapo owa uishi nae inawezekana hata wewe unampotezea muda wakupata mtu atakae mkubali alivyo , nachojua mungu akikupa ukilema atakupa na mwendo ila hili ni deni utalilipia hata katika uzao wako na mungu akupe umri mrefu ili siku moja uone ni wapi ulikosea ni hayo tu panapo makosa tusameaneni.
 
Tusipende sana kutupia lawama wengine bila kujikagua wapi tunakosea, unaweza kuta wewe ndio unamtia nuksi binti wa watu. Kama vipi muache akajitafutie maisha kwingine. Huna sifa ya mume bora.
 
TUlizana na mkeo huyo ni baraka kutoka kwa mungu ingawaje now unamuona nuksi endelea kusubiri utakuja pata malipo yalio mazuri mmno
 
Na kwenye ndoa mmekaa muda gani bila kupata mtoto.....nakuuliza HIV sababu nna same condition kama ya wife wako sometimes hua napatwa hofu
Usijali kama utakua na maswali mengi unaweza nitext Pm
Ten months now sema ana ujauzito wa two month kuna combination ya dawa tumetumia zimesaidia
 
Hali ya uchumi ya nchi na dunia nzima unaileta na kuifananisha na ndoa.Badili mifumo ya utafutaji unaweza solve tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…