Kosa gani unalijutia na limeharibu maisha yako?

Kosa gani unalijutia na limeharibu maisha yako?

huyu mwanamke ni nuksi.
Nakusikitikia kwa kuwa una mawazo ya namna hii. Chunga sana kauli unazozitoa maana hicho ndicho ulichokipanda ndani yako.

Nina baba yangu mdogo huu uzi ni kama pia unamuhusu. Alikuja kumuacha mama Janeth, bado maisha yakawa magumu. Akadai yule mwanamke alimwachia nuksi

Mama wa watu kaenda huko alikoolewa kazan na watoto wazuri. Kawa mzuri zaidi, huku jamaa anadai bado alimwachia kigundu

Sad.
 
Mimi najuta kwanini nilioa mapema tena huyu mwanamke ni nuksi. Toka nimeoa kila kitu kinaenda mrama, hapati mtoto mwaka wa 6 sasa, biashara tulianza zimekufa, kiufupi maisha yameharibika na nimepoteza mwelekeo kabisa.

Tumepima afya yake wanasema hormones imbalance, ametumia dawa za kila aina, za hospital na kienyeji ila bado.

Kumbukebi mimi Kabla ya kumuoa tayari nilishakuwa na mtoto ambaye kwa sasa ana 10 years. Pia baada ya kuona yeye hapati mtoto kuna mchepuko nilidate nae, nikapata nae mtoto. So ninao watoto wawili wa mama tofauti. Wazuri wanafanana, ila siipendi hii hali ya kuwa na watoto nje ya mke wangu na Bado nataka watoto.

Nifanyaje hapa wadau. Nina mpenda huyu mke, ni wife material ndiye anayelea mtoto wangu wa kwanza. Shida ndio hiyo haoni siku kabisa na hashiki mimba

Najuta, kutoka nashindwa. Nifanyaje?
Acha kufuru, yamewezekana wewe ndiyo mwenye hiyo nuksi na unampitisha binti wa watu kwenye matatizo.
Kama wewe umeweza kupata watoto wa nje, hebu mruhusu na yeye atoke na kidume kingine huone kama hashiki mimba.
Usimpe stress mkeo, zidisha upendo na Mwenyezi Mungu atawajalia mtoto. Kuna watu wamepata watoto baada ya miaka 10 ndoani, wewe unalalamika miaka 6!
 
Maisha bhana, unaona unateseka sanaaaa kutokuwa na mtoto wa ndani ya ndoa Ila humfikirii huyo ambaye hana na pengine analea mtoto wako ambaye kila siku anamkumbusha kuwa yeye ndiye mwenye tatizo..

Mkuu unastahili kumuhurumia mkeo kuliko unavyomnyanyapaa kwa sababu anapitia makubwa kukuliko. Lakini pia usimseme mtu kwa kitu ambacho ni nature imekubariki nacho. Kwa sababu Si kama ukiingia kitandani huwa unafanya chochote EXTRA zaidi ya kumimina mbegu ili upate mtoto,

ni kwa kudra tu unapata..

Hivyo usitukane kiumbe wa Mungu kwa kuona ni kosa lake kutokupata watoto maana kama vile nature ilikupa watoto bhasi inaweza kuchukua na usipate tena. Kuwa makini mkuu ๐Ÿ™๐Ÿฝ
 
Back
Top Bottom