Kosa gani unalijutia na limeharibu maisha yako?

huyu mwanamke ni nuksi.
Nakusikitikia kwa kuwa una mawazo ya namna hii. Chunga sana kauli unazozitoa maana hicho ndicho ulichokipanda ndani yako.

Nina baba yangu mdogo huu uzi ni kama pia unamuhusu. Alikuja kumuacha mama Janeth, bado maisha yakawa magumu. Akadai yule mwanamke alimwachia nuksi

Mama wa watu kaenda huko alikoolewa kazan na watoto wazuri. Kawa mzuri zaidi, huku jamaa anadai bado alimwachia kigundu

Sad.
 
Acha kufuru, yamewezekana wewe ndiyo mwenye hiyo nuksi na unampitisha binti wa watu kwenye matatizo.
Kama wewe umeweza kupata watoto wa nje, hebu mruhusu na yeye atoke na kidume kingine huone kama hashiki mimba.
Usimpe stress mkeo, zidisha upendo na Mwenyezi Mungu atawajalia mtoto. Kuna watu wamepata watoto baada ya miaka 10 ndoani, wewe unalalamika miaka 6!
 
Maisha bhana, unaona unateseka sanaaaa kutokuwa na mtoto wa ndani ya ndoa Ila humfikirii huyo ambaye hana na pengine analea mtoto wako ambaye kila siku anamkumbusha kuwa yeye ndiye mwenye tatizo..

Mkuu unastahili kumuhurumia mkeo kuliko unavyomnyanyapaa kwa sababu anapitia makubwa kukuliko. Lakini pia usimseme mtu kwa kitu ambacho ni nature imekubariki nacho. Kwa sababu Si kama ukiingia kitandani huwa unafanya chochote EXTRA zaidi ya kumimina mbegu ili upate mtoto,

ni kwa kudra tu unapata..

Hivyo usitukane kiumbe wa Mungu kwa kuona ni kosa lake kutokupata watoto maana kama vile nature ilikupa watoto bhasi inaweza kuchukua na usipate tena. Kuwa makini mkuu πŸ™πŸ½
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…