Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Ndio nimeamka sasa hivi Hapa, nikaota na kuambiwa kuwa JPM alipambana na maadui Bandia huku akiwaacha Maadui halisi wakipeta. Ndoto hiyo ambayo nina uhakika nayo Kwa Asilimia Mia moja inanipa tafsiri kuwa JPM alishindwa kutambua maadui wake halisi na Hilo kwenye uwanja wa vita ni kushindwa vita na kupigwa na adui.
Ni Sawa uwe unaumwa UKIMWI alafu utumie Dawa za Mseto kupambana na Malaria ukidhani unaumwa malaria kumbe unaumwa UKIMWI.
Hii ni fundisho Kwa wengine ambao mtaingia madarakani iwe leo au miaka ishirini ijayo. Kabla hamjaanza mapambano hakikisheni mnawafahamu maadui zenu halisi. Ili kuepuka kupoteza muda na mapambano kijinga.
Haiwezekani unapambana na adui zako unajitahidi kuwamaliza lakini wanazidi kuongezeka. Hiyo haiwezekan.
Haiwezekani mipango yako mnapanga Kwa Siri alafu kesho asubuhi unakuta ipo hewani hiyo pekee inatakiwa kukushtua kuwa tatizo lipo ndani na wala sio nje.
Ndoto hii inawataka watawala wawe makini zaidi na Wale wasiopiga kelele dhidi Yao kuliko Wale wapiga makelele.
JPM alipambana zaidi na Wale waliokuwa wanapiga makelele akijua HAO ndio adui zake lakini ndoto imeniambia kuwa walikuwa maadui bandia.
Adui halisi alikuwa kwenye mahandaki wamejificha.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam