Experience yangu binafsi sio mara moja bali ni mara mbili niliazima gari kwa marafiki wawili tofauti...
Mimi bwana kuazima gari plus uongo ulinicost sana.
Kuna jamaa my first car ilikuwa gari ya masela maana nilikuwa bado chalii. Sasa akanipigia simu nakuja uniazime gari.
Mimi nikamdanganya nimesafiri ila nenda utamkuta dogo atakupa.
Jamaa akasema namtuma binam yangu. Jamaa kaja kumbe mimi niko room, kachukua gari kumbe kaenda kapiga mzinga halafu kaitoa kwakuwa inatembea akaipeleka hivyo hivyo kwa jamaa akamwambia nimempa gari ikiwa hivyo.
Sasa jamaa kesho yake ananitumia msg mbona umenipa gari bovu sana.
Mimi namwambia michubuko hiyo kidogo tu na uliichubua wewe. Jamaa anajibu siwez hata kutembea nayo.
Si akatuma picha whatsapp, gari imebondeka kushoto vioo vimepasuka kuna tundu hadi mtu wa ndani unamwona taa ya kushoto mbele imepasuka.
Kidogo nizimie.
Nikamwambia jamaa hakuchukua gari hivyo jamaa anasema alilikuta hivyo.
Jamaa akasema au dogo lako ndip aliliangusha. Hajui kuwa limechukuliwa nikiwa room.
Basi nlichukua gari nikaliuza na urafiki ukaishia hapo maana hakuamini kuwa jamaa yake alichukua gari likiwa salama