Kosa kubwa kuazimana gari au pikipiki yako, tukio gani limewahi kukukuta ulipoazima chombo chako cha moto?

Kosa kubwa kuazimana gari au pikipiki yako, tukio gani limewahi kukukuta ulipoazima chombo chako cha moto?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Experience yangu binafsi sio mara moja bali ni mara mbili niliazima gari kwa marafiki wawili tofauti, wa kwanza aligongesha bampa wa pili aligongesha karibu na mlango lakini hakuna alienijulisha kilichotokea pindi wanaponirudishia funguo za gari.

Nikiazima gari na ikirudi huwa lazima niikague kabla sijaitumia, wote nilipowauliza kuhusu kugongesha wakasema niliwapa gari hivyo hivyo.

Mara ya kwanza ilinikosti elf 70 kurekebisha, mara ya pili laki na 20, kuanzia hapo niliona kuazima gari kunaweza kuja kunigharimu zaidi, Imagine mtu umwazime gari aigongeshe uvunguni breki zifeli kukamata alafu asikwambie ?
 
Jau sana, kuna mtu nilimwazima chombo changu akaharibu kifaa na hakusema.

Sometimes ni bora kuwa Selfish ili mambo yaende!
 
Mwambie chombo hakina mafuta hata ya kufika sheli, maana ukimwambie yanafika sheli atakuambia mpe akaweke.

Kimsingi huwa ninapenda kumpa mtu chombo iwapo ninamfahamu na pili awe na chombo na chombo husika kiwe kinatunzwa.

Kama mtu humjui, au unamjua na ana chombo na chombo chake hakina matunzo mazuri, basi usitarajie akihurumie chombo chako.
 
Mtu unakuwa na akili za aina gani kuazimisha gari ya mtu utumie kama yako?

Kimsingi sio vema kuleta mazoea na mali za watu ambazo wamenunua kwa wasi wasi mkubwa na kujitoa kuliko pitiliza.

Imagine unachukua gari ya mtu halafu unataka ukalitumie kama la kwako wakati kuna uber na bolt kama shida ni kupata usafiri private

Tujifunze kuwa na subira kidogo linapokuja swala la kutamani vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wetu.
 
Experience yangu binafsi sio mara moja bali ni mara mbili niliazima gari kwa marafiki wawili tofauti...
Mimi bwana kuazima gari plus uongo ulinicost sana.

Kuna jamaa my first car ilikuwa gari ya masela maana nilikuwa bado chalii. Sasa akanipigia simu nakuja uniazime gari.

Mimi nikamdanganya nimesafiri ila nenda utamkuta dogo atakupa.

Jamaa akasema namtuma binam yangu. Jamaa kaja kumbe mimi niko room, kachukua gari kumbe kaenda kapiga mzinga halafu kaitoa kwakuwa inatembea akaipeleka hivyo hivyo kwa jamaa akamwambia nimempa gari ikiwa hivyo.

Sasa jamaa kesho yake ananitumia msg mbona umenipa gari bovu sana.

Mimi namwambia michubuko hiyo kidogo tu na uliichubua wewe. Jamaa anajibu siwez hata kutembea nayo.

Si akatuma picha whatsapp, gari imebondeka kushoto vioo vimepasuka kuna tundu hadi mtu wa ndani unamwona taa ya kushoto mbele imepasuka.
Kidogo nizimie.

Nikamwambia jamaa hakuchukua gari hivyo jamaa anasema alilikuta hivyo.

Jamaa akasema au dogo lako ndip aliliangusha. Hajui kuwa limechukuliwa nikiwa room.

Basi nlichukua gari nikaliuza na urafiki ukaishia hapo maana hakuamini kuwa jamaa yake alichukua gari likiwa salama
 
Back
Top Bottom