Kosa kubwa la Malecela wa NIMR: Rais kaona mbali athari za ZIKA

Kosa kubwa la Malecela wa NIMR: Rais kaona mbali athari za ZIKA

Dah,, shemeji ako kantibua sana leo... Ila kwa Hili imebidi nicheke Teh Teh Teh..
[HASHTAG]#borakukaakimyakulikokusemaukweli[/HASHTAG]
duuhh.. pole mzazi, mi mwenyewe nilishindwa kujizuia ndio nikajikuta naanza kuamini hivi
 
Mimi nadhan wewe ndio mjinga. Umerely kwenye mere words za mtoa ufafanuzi (Tuntemeke) Utadhan yeye ndio spokesman wa wizara. Usiwe mvivu, information za kazi ya NiMR zipo wazi, majukumu yake yapo wazi. Kukisaidia bofya hapa (NIMR Tanzania).

Hakuna popote palipoandikwa kuwa utafiti unapaswa upelekwe kwanza wizarani ndio uwe published. Wote nadhan mnajichanganya, mnachanganya kutoa taarifa ya utafiti juu ya Uwepo wa Zika na Taarifa ya Uwepo wa Zika. Alicho kifanya Dr. Mwele ni kutumia Lugha ambayo kila mtanzania ataielewa juu ya utafiti uliofanywa juu ya uwepo wa zika. Kimsingi kafafanua nini kipo ndan ya huo utafiti huo ambao yeye hakushiriki kuufanya in person.

Yeye km mkurugenz wa shirika hilo anayohaki yote kutangaza matokeo ya tafiti mbali mbali zinazohusiana na afya. Ni moja ya function za nimr.

Utaratibu wa kupublish research findings upo wazi co tu Tanzania Bali duniani. Kutaka watu wapitishe matokeo ya utafiti serikalin kabla ya kiyatangaza nadhan ni kutafuta kuziba midomo watafiti. Watafiti wanapaswa kufanya kazi independently. Kuwaingilia.ni kuparalyze brains za wataalam. Ni kuua fikra za taifa.
Mkuu kuna suala la impact ya ujumbe unaotangazwa na huyo mfanya utafiti.

Kila baada ya wiki ukiangalia habari jioni utaona rais anampokea mgeni mwekezaji fulani, sasa unapoitangazia dunia juu ya zika maana yake wale wawekezaji unawaambia "jamani eeh bakini kwenu mkija huku mtaondoka na ugonjwa".

Inaweza ikawa ipo ndani ya mipaka ya kazi ya Dr Mwele, lakini wakati mwingine madhara mapana ya uwasilishaji wa tafiti yanaweza kuharibu hata mipango ya muda mfupi na mrefu ya serikali.
 
Nahisi kama vile kuna uwepo wa kupimana nguvu kati ya dada wa kitanga aliyepoteza Baba mzazi mwaka huu na yule aliyetumbuliwa majuzi.

Kunaweza kuwepo vita ya chini kwa chini inayoongozwa na jeuri ya usomi, kwa upande wa wote wawili.

Kwa sababu kama matakwa ya kutangaza uwepo wa ugonjwa yanamtaka mfanya tafiti ashirikishe wadau wengine, upo uwezekano wa uwepo wa ile jeuri ya kisomi. Kujiona kana kwamba mimi mzoefu na ninastahili hiyo nafasi yako wewe.

Ndio maana wamarekani walimchambua sana Mama Clinton kabla ya kumpiga chini siku ya uchaguzi, yapo mengi ambayo humpa mtu sifa ya kuwa kiongozi mwenye dhamana inayogusa maisha ya wengi.
 
Back
Top Bottom