Kosa kubwa la Malecela wa NIMR: Rais kaona mbali athari za ZIKA

Kosa kubwa la Malecela wa NIMR: Rais kaona mbali athari za ZIKA

Kwahiyo kosa lake kusema ukweli? Ndiyo Maana mwenye kigoda wa kituo fulani alilsambaza madawa ya ukimwi fake watu wakafwa vibwaya lakini kwa kuwa ni mwenzetu no problem? One very good day ukweli na haki ya Mr God itajitokeza hadharani tu
 
Chifu, si useme tu! Kwa hiyo NIMR inawajibika kwa WHO pia? Na je, hilo lipo kwenye sekta ya afya tu?

..hivi mpaka huyu mama anatangaza matokeo ya huo utafiti serikali na vyombo vyake walikuwa hawana hizo habari?

..kwenye thread nyingine hapa JF wanadai utafiti huo umeshatolewa ktk moja ya scientific journal huko nje.

..ikulu, wizara ya afya, na nimr, hawajawahi kukaa pamoja na kupanga mkakati wa ku deal na suala hili baada ya kupata matokeo ya utafiti?
 
Zika na NIMR

Dk. Mwele Ntuli Malecela leo si Mkurugenzi tena wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Ikulu leo imemtangaza Profesa Yunus Mgaya kuwa mbadala wake.

Kwanini Mwele kaondolewa? Nimeulizwa hili swali na baadhi ya watu nami nikauliza hapa na pale ili kupata majibu. Na hili ndilo nililoambiwa.

Mosi, kwamba ugonjwa wa Zika upo Tanzania. Ugonjwa huu ulianzia Uganda na upo pia kwetu kwa muda mrefu. Ila upo katika hali iliyodhibitiwa, wataalamu wanaitwa Endemic. Si tatizo kubwa lakini upo.

Lakini Tanzania haina tatizo la ZIKA. Kwa jinsi tatizo la ugonjwa huo lilivyo kubwa, kabla halijatangazwa, kuna taratibu za kufuatwa ikiwamo kuhusisha Serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Imefanyika hivi kwa sababu madhara ya kutangaza ugonjwa huo kwa taifa ni makubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tatizo ni kwamba tangazo la Mwele halikufuata hizo taratibu. Na zaidi, halikuzingatia athari ambazo zingejitokeza kwa yeye kutoa taarifa kama zile.

Kwenye Kiswahili, tofauti ya maneno Endemic na Epidemic ( ugonjwa uliodhibitiwa na uliolipuka) ni ndogo. Ukisema Zika ipo, magazeti yatasema ZIKA imeingia.

Sasa, labda, Rais mwingine, kwenye Serikali nyingine, angeweza ˊkupotezea` tu kauli ile ya Mwele. Lakini binti huyu wa mzee John Malecela hakuwa amesoma vema alama za nyakati.

Hivyo, kwa maana ya kosa, Mwele alikosea. Ishu ya ZIKA haikuwa ya kutangazwa na taasisi yake pekee bila kuhusisha serikali na wadau wengine.

Hivyo, hapa, tatizo si serikali kukataa taarifa ya kitaalamu. Ni kwamba mhusika amekiuka taratibu ambazo zimewekwa. Na huo ugonjwa haujaja sasa hivi. Upo siku nyingi ila umedhibitiwa.

onyo haiwezekani??
 
Kama kila tafiti lazima zipitie ofisi za wakubwa basi tafiti nyingi nzuri hatutazisikia kamwe!!
Uelewa ndiyo tatizo. NIMR ni idara au taasisi ya selikari. Kwa hiyo mmiliki ni selikari. Wewe utumwe na mtu nifanyie kazi hii na ukishafanya wewe huyo huyo mbio kwa waandishi wa habari kutangaza kabla ya kumpa mrejesho aliekutuma. Ni sahihi?
 
Mkuu wamajeshi hatangazi vita hata siku moja. Ni kazi ya Rais ambaye Ni amir jeshi.
Mwele Ni mtaka sika. Ngazi aliyofikia na muda aliokaa kwenye nafasi yake, aliases kujua hayo. Kama hakujua, hakustahili nafasi hiyo.
Uamuzi wa kumtungua Ni sahihi kabisa.

Lakini tusisahau : Free MaxenceMelo at once!
 
Shida kubwa iko kwenye utaratibu wa kugawana vyeo, hiyo nafasi ilipaswa kutangazwa na watu waombe ili atakayepatikana ajue ana ripoti kwa nini?

Sasa waziri wa Afya anateuliwa na Raisi na Dr Mwele kateuliwa Raisi hapo wote wana ndevu, Dr. mwele ataripoti kwa nani?
Comment yako ya mwisho imenifanya nicheke.
 
Sidhan atua alizochukuliwa ni stahili.
Ilipaswa watafute siku nyingine waweke Mambo sawa.

Sasa sipati picha ugonjwaa huu ukilipuka sijui huyo Pogba atasema nini?


Mbona hapo Uganda inatambulika ZIKA ipo lkn mnayosema sijui matatizo ya kiuchumi, kijamii hatuyaoni?

Tuache Ushamba!!

Tena ni ushamba wa kiwango cha lami. Sasa kama Dr. Mwele Malecela anasema kuwepo kwa Zika ni kwa mujibu wa utafiti; halafu wao serikali mara wanasema Zika haipo mara tena waseme Zika ipo ila imedhibitiwa. Halafu wanakuja na sababu nyingine ya kipuuzi eti kutangaza Zika kuwepo kunahatarisha uchumi etc. Yaani ina maana hawaelewi kwamba afya ni muhimu zaidi ya uchumi. Upuuzi mtupu.
 
Hv huyu Dr. Mwele alikuwa hafahamu taratibu au kimemkuta nn? au jinamizi limeikuta familia hii. Kwani angekaa kimya ingekuwaje
Binti wa kigogo alijisahau kidogo. Teheheheheeeee. Si unafahamu aligombea Urahisi? Alidhani ndo keshakuwa so anaweza fanya hayo alofanya.
 
hakuna kosa lolote alilofanya zaidi ya kudidimiza ubunivu na kujituma kwa wafanyakazi wetu , na hii si dalili njema kwa watendaji wa serikali
Lumumba naona leo umeamua kuweka ushabiki pembeni na kuamua kuongea point
 
Mkuu TUNTEMEKE umeweka suala hili vyema kabisa. Athari kwa uchumi wa nchi yetu zitakuwa kubwa baada ya hilo tangazo. Kenya sasa hivi kila chombo cha habari kinatangaza kwamba Tanzania kuna ZIKA. Watalii wataikimbia Tanzania. Kenya sasa wanatumia rungu la Mwele kutuchapa sawia. Huyu mama nilimheshimu wakati anashughulikia magonjwa ya mtende na ngirimaji, labda angebaki hukohuko.
watalii sual la uwepo wa virusi Tz walilijua zamanii, sisi tu ndiyo tulikuwa gizani. kumtumbua Mwele ndiyo wamechochea moto, kila sehemu wanaongelea zika.
 
Kwahiyo kumbe hata afya zetu watu wanazifanyia Siasa na Propaganda.????? Kwani Japani, Brazili, china wanavyo tangazaga hawajui adhari zake kiuchumi?
 
Back
Top Bottom