Kosa kubwa la Malecela wa NIMR: Rais kaona mbali athari za ZIKA

Zika na NIMR

Dk. Mwele Ntuli Malecela leo si Mkurugenzi tena wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Ikulu leo imemtangaza Profesa Yunus Mgaya kuwa mbadala wake.

Kwanini Mwele kaondolewa? Nimeulizwa hili swali na baadhi ya watu nami nikauliza hapa na pale ili kupata majibu. Na hili ndilo nililoambiwa.

Mosi, kwamba ugonjwa wa Zika upo Tanzania. Ugonjwa huu ulianzia Uganda na upo pia kwetu kwa muda mrefu. Ila upo katika hali iliyodhibitiwa, wataalamu wanaitwa Endemic. Si tatizo kubwa lakini upo.

Lakini Tanzania haina tatizo la ZIKA. Kwa jinsi tatizo la ugonjwa huo lilivyo kubwa, kabla halijatangazwa, kuna taratibu za kufuatwa ikiwamo kuhusisha Serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Imefanyika hivi kwa sababu madhara ya kutangaza ugonjwa huo kwa taifa ni makubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tatizo ni kwamba tangazo la Mwele halikufuata hizo taratibu. Na zaidi, halikuzingatia athari ambazo zingejitokeza kwa yeye kutoa taarifa kama zile.

Kwenye Kiswahili, tofauti ya maneno Endemic na Epidemic ( ugonjwa uliodhibitiwa na uliolipuka) ni ndogo. Ukisema Zika ipo, magazeti yatasema ZIKA imeingia.

Sasa, labda, Rais mwingine, kwenye Serikali nyingine, angeweza ˊkupotezea` tu kauli ile ya Mwele. Lakini binti huyu wa mzee John Malecela hakuwa amesoma vema alama za nyakati.

Hivyo, kwa maana ya kosa, Mwele alikosea. Ishu ya ZIKA haikuwa ya kutangazwa na taasisi yake pekee bila kuhusisha serikali na wadau wengine.

Hivyo, hapa, tatizo si serikali kukataa taarifa ya kitaalamu. Ni kwamba mhusika amekiuka taratibu ambazo zimewekwa. Na huo ugonjwa haujaja sasa hivi. Upo siku nyingi ila umedhibitiwa.
Serikali imesema hakuna zika ....
 
vip kama angepewa onyo, kungekuwa na tatzo, au kila nayekosea utawala huu, lazima atumbuliwe?
 
Mbona yule waziri aliyetudanganya kuwa dawa zipo mahospitalini, na hapo hapo katibu mkuuwa wizara ya Afya anasema dawa hakuna...!MBONA HAJATUMBULIWA?
 
Tz nima sna. Mi niko pembeni ya ulingo
Endeleeni kicheza ngoma zenu. Mwishoe mshindi atajulikana.
 
Zika na NIMR

Dk. Mwele Ntuli Malecela leo si Mkurugenzi tena wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Ikulu leo imemtangaza Profesa Yunus Mgaya kuwa mbadala wake.

Kwanini Mwele kaondolewa? Nimeulizwa hili swali na baadhi ya watu nami nikauliza hapa na pale ili kupata majibu. Na hili ndilo nililoambiwa.

Mosi, kwamba ugonjwa wa Zika upo Tanzania. Ugonjwa huu ulianzia Uganda na upo pia kwetu kwa muda mrefu. Ila upo katika hali iliyodhibitiwa, wataalamu wanaitwa Endemic. Si tatizo kubwa lakini upo.

Lakini Tanzania haina tatizo la ZIKA. Kwa jinsi tatizo la ugonjwa huo lilivyo kubwa, kabla halijatangazwa, kuna taratibu za kufuatwa ikiwamo kuhusisha Serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Imefanyika hivi kwa sababu madhara ya kutangaza ugonjwa huo kwa taifa ni makubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tatizo ni kwamba tangazo la Mwele halikufuata hizo taratibu. Na zaidi, halikuzingatia athari ambazo zingejitokeza kwa yeye kutoa taarifa kama zile.

Kwenye Kiswahili, tofauti ya maneno Endemic na Epidemic ( ugonjwa uliodhibitiwa na uliolipuka) ni ndogo. Ukisema Zika ipo, magazeti yatasema ZIKA imeingia.

Sasa, labda, Rais mwingine, kwenye Serikali nyingine, angeweza ˊkupotezea` tu kauli ile ya Mwele. Lakini binti huyu wa mzee John Malecela hakuwa amesoma vema alama za nyakati.

Hivyo, kwa maana ya kosa, Mwele alikosea. Ishu ya ZIKA haikuwa ya kutangazwa na taasisi yake pekee bila kuhusisha serikali na wadau wengine.

Hivyo, hapa, tatizo si serikali kukataa taarifa ya kitaalamu. Ni kwamba mhusika amekiuka taratibu ambazo zimewekwa. Na huo ugonjwa haujaja sasa hivi. Upo siku nyingi ila umedhibitiwa.
Ili useme ugonjwa umeudhibiti lazima uwe na baseline data na trend yake ya ueneaji. Lazima useme hapo awali incidence ilikuwa X% kwa mwaka lakini baada ya hatua A,B na C za kuudhibiti sasa incidence yake ni Y%. Je, tafiti gani ilifanyika hapa nchini kuonyesha uwepo na ukubwa wa ZIKA? Je, hatua zipi za kiudhibiti zilizofanyika (lete na reference). Hii issue ni suala la siasa na kukomoana
 
Mkuu TUNTEMEKE umeweka suala hili vyema kabisa. Athari kwa uchumi wa nchi yetu zitakuwa kubwa baada ya hilo tangazo. Kenya sasa hivi kila chombo cha habari kinatangaza kwamba Tanzania kuna ZIKA. Watalii wataikimbia Tanzania. Kenya sasa wanatumia rungu la Mwele kutuchapa sawia. Huyu mama nilimheshimu wakati anashughulikia magonjwa ya mtende na ngirimaji, labda angebaki hukohuko.
Sasa ulitaka ukweli ufichwe au? ?sijakuelewa
 
Hv huyu Dr. Mwele alikuwa hafahamu taratibu au kimemkuta nn? au jinamizi limeikuta familia hii. Kwani angekaa kimya ingekuwaje
 
Mwele zilipendwa ameshateuliwa mr yunusu ndio mkurugenzi mkuu kwa sasa
 
Zika na NIMR

Dk. Mwele Ntuli Malecela leo si Mkurugenzi tena wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Ikulu leo imemtangaza Profesa Yunus Mgaya kuwa mbadala wake.

Kwanini Mwele kaondolewa? Nimeulizwa hili swali na baadhi ya watu nami nikauliza hapa na pale ili kupata majibu. Na hili ndilo nililoambiwa.

Mosi, kwamba ugonjwa wa Zika upo Tanzania. Ugonjwa huu ulianzia Uganda na upo pia kwetu kwa muda mrefu. Ila upo katika hali iliyodhibitiwa, wataalamu wanaitwa Endemic. Si tatizo kubwa lakini upo.

Lakini Tanzania haina tatizo la ZIKA. Kwa jinsi tatizo la ugonjwa huo lilivyo kubwa, kabla halijatangazwa, kuna taratibu za kufuatwa ikiwamo kuhusisha Serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Imefanyika hivi kwa sababu madhara ya kutangaza ugonjwa huo kwa taifa ni makubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tatizo ni kwamba tangazo la Mwele halikufuata hizo taratibu. Na zaidi, halikuzingatia athari ambazo zingejitokeza kwa yeye kutoa taarifa kama zile.

Kwenye Kiswahili, tofauti ya maneno Endemic na Epidemic ( ugonjwa uliodhibitiwa na uliolipuka) ni ndogo. Ukisema Zika ipo, magazeti yatasema ZIKA imeingia.

Sasa, labda, Rais mwingine, kwenye Serikali nyingine, angeweza ˊkupotezea` tu kauli ile ya Mwele. Lakini binti huyu wa mzee John Malecela hakuwa amesoma vema alama za nyakati.

Hivyo, kwa maana ya kosa, Mwele alikosea. Ishu ya ZIKA haikuwa ya kutangazwa na taasisi yake pekee bila kuhusisha serikali na wadau wengine.

Hivyo, hapa, tatizo si serikali kukataa taarifa ya kitaalamu. Ni kwamba mhusika amekiuka taratibu ambazo zimewekwa. Na huo ugonjwa haujaja sasa hivi. Upo siku nyingi ila umedhibitiwa.
Ufafanuzi Murua. Kosa hilo lipo kwenye Kifungu 9(1) Cha Sheria ifuatayo:
IMG-20161217-WA0012.jpg
 
Mbona na ww unakuwa mjinga kiasi hicho jamaa hapo katoa ufafanuzi mzuri kwamba kuna utaratibu unatakiwa kabla ya kutangaza tatizo kama hilo ikiwapo pamoja na kuijulisha serikali na WHO, watz mbona wengine uwezo wa kuelewa ni mdogo sana au unafurahi kuchangia bila hata kutafakari au ndiyo mlioajiriwa kukosoa kila kitu ? Very stupid
Mimi nadhan wewe ndio mjinga. Umerely kwenye mere words za mtoa ufafanuzi (Tuntemeke) Utadhan yeye ndio spokesman wa wizara. Usiwe mvivu, information za kazi ya NiMR zipo wazi, majukumu yake yapo wazi. Kukisaidia bofya hapa (NIMR Tanzania).

Hakuna popote palipoandikwa kuwa utafiti unapaswa upelekwe kwanza wizarani ndio uwe published. Wote nadhan mnajichanganya, mnachanganya kutoa taarifa ya utafiti juu ya Uwepo wa Zika na Taarifa ya Uwepo wa Zika. Alicho kifanya Dr. Mwele ni kutumia Lugha ambayo kila mtanzania ataielewa juu ya utafiti uliofanywa juu ya uwepo wa zika. Kimsingi kafafanua nini kipo ndan ya huo utafiti huo ambao yeye hakushiriki kuufanya in person.

Yeye km mkurugenz wa shirika hilo anayohaki yote kutangaza matokeo ya tafiti mbali mbali zinazohusiana na afya. Ni moja ya function za nimr.

Utaratibu wa kupublish research findings upo wazi co tu Tanzania Bali duniani. Kutaka watu wapitishe matokeo ya utafiti serikalin kabla ya kiyatangaza nadhan ni kutafuta kuziba midomo watafiti. Watafiti wanapaswa kufanya kazi independently. Kuwaingilia.ni kuparalyze brains za wataalam. Ni kuua fikra za taifa.
 
Ufafanuzi Murua. Kosa hilo lipo kwenye Kifungu 9(1) Cha Sheria ifuatayo:
View attachment 447335
Hili bandiko la kisheria umeliweka kwa kuwa umelielewa au ni ktk jitihada ya kumsulubisha Dr. Mwele? Hili ni la kutangaza uwepo wa magonjwa mbali mbali incl. Zika. Sio sheria ya kutangaza matokeo ya utafiti. Alichokifanya Dr. Mwele ni kutangaza matokeo ya utafiti uliokuwa presented kwenye scientific conference. Kazi za kutangaza ugonjwa co za Nimr, ni kazi ya wizara. Mbona tunajivuruga?
 
Zika na NIMR

Dk. Mwele Ntuli Malecela leo si Mkurugenzi tena wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Ikulu leo imemtangaza Profesa Yunus Mgaya kuwa mbadala wake.

Kwanini Mwele kaondolewa? Nimeulizwa hili swali na baadhi ya watu nami nikauliza hapa na pale ili kupata majibu. Na hili ndilo nililoambiwa.

Mosi, kwamba ugonjwa wa Zika upo Tanzania. Ugonjwa huu ulianzia Uganda na upo pia kwetu kwa muda mrefu. Ila upo katika hali iliyodhibitiwa, wataalamu wanaitwa Endemic. Si tatizo kubwa lakini upo.

Lakini Tanzania haina tatizo la ZIKA. Kwa jinsi tatizo la ugonjwa huo lilivyo kubwa, kabla halijatangazwa, kuna taratibu za kufuatwa ikiwamo kuhusisha Serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Imefanyika hivi kwa sababu madhara ya kutangaza ugonjwa huo kwa taifa ni makubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tatizo ni kwamba tangazo la Mwele halikufuata hizo taratibu. Na zaidi, halikuzingatia athari ambazo zingejitokeza kwa yeye kutoa taarifa kama zile.

Kwenye Kiswahili, tofauti ya maneno Endemic na Epidemic ( ugonjwa uliodhibitiwa na uliolipuka) ni ndogo. Ukisema Zika ipo, magazeti yatasema ZIKA imeingia.

Sasa, labda, Rais mwingine, kwenye Serikali nyingine, angeweza ˊkupotezea` tu kauli ile ya Mwele. Lakini binti huyu wa mzee John Malecela hakuwa amesoma vema alama za nyakati.

Hivyo, kwa maana ya kosa, Mwele alikosea. Ishu ya ZIKA haikuwa ya kutangazwa na taasisi yake pekee bila kuhusisha serikali na wadau wengine.

Hivyo, hapa, tatizo si serikali kukataa taarifa ya kitaalamu. Ni kwamba mhusika amekiuka taratibu ambazo zimewekwa. Na huo ugonjwa haujaja sasa hivi. Upo siku nyingi ila umedhibitiwa.
Amen RA
 
Patriote,
NIMR ingekuwa kama TWAWEZA, Dada yangu Mwele Ntuli alikuwa sahihi kutangaza matokeo kwa utaratibu alioutumia. Kwa upande wa Serikali, kuna taratibu zake. Nazo ni hizo zilizobainishwa kwenye kifungu tajwa na hususani kwenye suala la uwepo wa magonjwa.

Kwa mujibu sheria hiyo Dr. Mwele amekosea. Hata hivyo, kuna Sheria na Busara ya kawaida. Kwa busara ya kawaida kuna kujiuliza kama je, ilishatosha kosa hilo kumtengua Mwele au alistahili onyo? Nayo ni sehemu ya majadiliano.

Lasivyo, kwa kiasi kidogo ninacho mfahamu Dr. Mwele , ana hekima, uzoefu na ujuzi usiotiliwa shaka ktk tasnia hii ya magonjwa na tafiti. Tatizo lipo kwenye utaratibu wa kuuhabarisha umma.
 
wanapewa madaraka ya nini kama hawaruhusiwi kutoa tafiti zake? basi taasisi zote ziongozwe na kurugenzi ya ikulu.
Notifiable diseases,nationally and internationally kuna Sheria zake ndugu sivyo hivyo unavyotaka wewe.no shortcuts with international issues.
 
Back
Top Bottom