Kosa kubwa la Malecela wa NIMR: Rais kaona mbali athari za ZIKA

Kosa kubwa la Malecela wa NIMR: Rais kaona mbali athari za ZIKA

Website ya CDC imeweka hii taarifa zamani sana, utafiti umefanyika zamani na hawa ndo wamereport so sioni ni kwa namna gani unaweza malaumu Mwele wakati Tanzania ipo listed kwenye website..........
 

Attachments

  • 1481968072023.png
    1481968072023.png
    54.3 KB · Views: 53
pia utafiti wake ulikuwa ni wa awali tuu na haukuwa wa kufanya hitimisho kuwa nchini kuna Zika.
We unaongea ivo kama nani?? Ile tu Nimr kua ni kituo cha tafti za magonjwa ya binadam inamaana tafiti zinafanywa na wanajirizisha kwanza kabla ya kuitoa
Sasa shida ya watz wengi kikitokea kitu wanaanza uhalali wa maamuz yaliyotolewa kulingana na mapenzi yao na serikal subrn mzuiliwe kulala na wake zenu kama Brazil huenda mkashtuka
 
TUNTEMEKE umeeleweka. Ikiwa muongozo unamtaka kuwashirikisha wadau wengine muhimu katika kutangaza na hakufanya hivyo, hakuna namna.
Hakuna walichosaidia tena saivi huo utafiti ndo utasambaa zaidi ingekua Hekima kama wangemwita wamalizane juu kwa juu sio unampiga mtu chini hajakushirikisha
 
Ni kweli, tunapaswa kujua ili tuchukue tahadhali. Lakini tulipaswa kujua kwa namna ambayo haitaleta image mbaya kwa jamii ya kimataifa.. unadhani ni vizuri uwekewe vikwazo vya kusafiri kwenda nje kwa sababu inch imejulikana kuwa na zika? watalii wote kubadilisha route na kuikacha Tanzania? wawekezaji kuikacha tz kisa zika, wakati imekuwemo siku nyiiiiiiiiiingi na wala haijaleta madhara makubwa? kwa nini wasingetumia njia nzuri kuwaambia watanzania na sio kuleta sintofahamu kwa jumuiya za kimataifa?
Ndo nyie ambao mnawaficha wake zenu kumbe mmezaa nje na Malaya eti kisa ndoa yako ina Amani ...
Na siku akijua timbwili lake hapana chezea (bora u mwambie msolve maisha yaendelee)
 
Suala ni kwamba hajaishirikisha Serikali ili kuipika taarifa na isingetangaza. Mi naona ni vema kujihami hasa kwa magonjwa mapya kumbukeni wenzetu walivyopata EBOLA madaktari wa Dunia nzima walienda kupiga kambi West Africa.
Nadhani anaandika kitu usichokijua.
NIMR ni taasisi ya Serikali. Unapozungumzia Kitengo cha M, tena kipo Wizara ya Afya Makao makuu. Kwa kifupi, ndani ya serikali, chombo kikuu kinachoweza kuzungumzia tafiti za Afya ni NIMR.
Sasa unaposema serikali haukuhusishwa katika kutolewa kwa matokeo ya utafiti ule unamaanisha nini?

Na kwa taarifa yako tu, matokeo ya utafiti ule yalishatolewa toka November, 2016, tena taasisi zote kubwa za tafiti za Afya duniani zinajua na hata watendaji wajuu wa wizara ilishajua pia.
Alichokifanya Dr.Mwele Malecella ni kutoa rasmi matokeo ya utafiti ule kwa umma wa wadau kwa niaba ya NIMR ambapo walihusika kufanya utafiti ule.
 
wanapewa madaraka ya nini kama hawaruhusiwi kutoa tafiti zake? basi taasisi zote ziongozwe na kurugenzi ya ikulu.
Hilo ss ni tatizo la uelewa na siasa ndani, mambo mengine ya kitaalmu yanatakiwa kujibiwa kitaalamu, na pia ndo maana yupo waziri afya, kwani ndo kazi yake, hicho unachotaka ww ni uropokaji.
 
Yeye katangaza tafiti ya kisayansi, na anatangazaga kila siku. Hivi mwananchi wa kawaida utataka kujua kuwa ugonjwa upo? au utataka kujua aliyesema ni nani? Kwangu ni bora nijue ugonjwa upo ili nichukue tahadhari, sio mnifiche kwa kigezo cha kuusubiria uwe epidemic ili mimi ndio niwe statistic
Bro. Sio kila kitu ni siasa, acha mambo ya kitaalamu yajibiwe kitaalamu, mwenye mamlaka hayo ni waziri wa afya.
 
wanapewa madaraka ya nini kama hawaruhusiwi kutoa tafiti zake? basi taasisi zote ziongozwe na kurugenzi ya ikulu.
Hata ukisoma parliament act ya mwaka 1979 iliyoanzisha NIMR..inatoa mamlaka ya wa wao NIMR kutangaza matokeo ya tafiti zao..huyu mama hajakurupuka kafanya vile sheria inamtaka kufanya ..Lakini kwa sababu serikali hii si ya utawala wa sheria matokeo yake ndo hayo.
 
Pumba , mwele atakuwa katolewa kwa sababu nyingine sio zika
Pumba?! Ni nani wewe Magufuli au mleta mada!? Ujue watu wengine mna majibu sana. Ungetakiwa ufafanuzi pumba ni ipi halafu Tully kufanyaje... Kuliko kumuita mtoa mada pumba kisha kumbe ww ndo pumbav
 
Kama kila tafiti lazima zipitie ofisi za wakubwa basi tafiti nyingi nzuri hatutazisikia kamwe!!
 
Zika na NIMR

Dk. Mwele Ntuli Malecela leo si Mkurugenzi tena wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Ikulu leo imemtangaza Profesa Yunus Mgaya kuwa mbadala wake.

Kwanini Mwele kaondolewa? Nimeulizwa hili swali na baadhi ya watu nami nikauliza hapa na pale ili kupata majibu. Na hili ndilo nililoambiwa.

Mosi, kwamba ugonjwa wa Zika upo Tanzania. Ugonjwa huu ulianzia Uganda na upo pia kwetu kwa muda mrefu. Ila upo katika hali iliyodhibitiwa, wataalamu wanaitwa Endemic. Si tatizo kubwa lakini upo.

Lakini Tanzania haina tatizo la ZIKA. Kwa jinsi tatizo la ugonjwa huo lilivyo kubwa, kabla halijatangazwa, kuna taratibu za kufuatwa ikiwamo kuhusisha Serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Imefanyika hivi kwa sababu madhara ya kutangaza ugonjwa huo kwa taifa ni makubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tatizo ni kwamba tangazo la Mwele halikufuata hizo taratibu. Na zaidi, halikuzingatia athari ambazo zingejitokeza kwa yeye kutoa taarifa kama zile.

Kwenye Kiswahili, tofauti ya maneno Endemic na Epidemic ( ugonjwa uliodhibitiwa na uliolipuka) ni ndogo. Ukisema Zika ipo, magazeti yatasema ZIKA imeingia.

Sasa, labda, Rais mwingine, kwenye Serikali nyingine, angeweza ˊkupotezea` tu kauli ile ya Mwele. Lakini binti huyu wa mzee John Malecela hakuwa amesoma vema alama za nyakati.

Hivyo, kwa maana ya kosa, Mwele alikosea. Ishu ya ZIKA haikuwa ya kutangazwa na taasisi yake pekee bila kuhusisha serikali na wadau wengine.

Hivyo, hapa, tatizo si serikali kukataa taarifa ya kitaalamu. Ni kwamba mhusika amekiuka taratibu ambazo zimewekwa. Na huo ugonjwa haujaja sasa hivi. Upo siku nyingi ila umedhibitiwa.
Mkuu TUNTEMEKE umeweka suala hili vyema kabisa. Athari kwa uchumi wa nchi yetu zitakuwa kubwa baada ya hilo tangazo. Kenya sasa hivi kila chombo cha habari kinatangaza kwamba Tanzania kuna ZIKA. Watalii wataikimbia Tanzania. Kenya sasa wanatumia rungu la Mwele kutuchapa sawia. Huyu mama nilimheshimu wakati anashughulikia magonjwa ya mtende na ngirimaji, labda angebaki hukohuko.
 
Magufuli yupo tiyari kutuona tukifa ila sio kutoa pesa kununua dawa. Bora tufe yeye anunue ndege amtambie jirani yake.
 
Back
Top Bottom