Kosa kubwa la Malecela wa NIMR: Rais kaona mbali athari za ZIKA

'Kukaa gizani na kusema mimi sitak kujua hata kama ugonjwa upo haitusaidii' Dr.Mwele Malecela kwenye video ya Mwananchi online
 
Asante kwa taarifa na ufafanuzi Mubashara.
 
Patriote,
NIMR ingekuwa kama TWAWEZA, Dada yangu Mwele Ntuli alikuwa sahihi kutangaza matokeo kwa utaratibu alioutumia. Kwa upande wa Serikali, kuna taratibu zake. Nazo ni hizo zilizobainishwa kwenye kifungu tajwa na hususani kwenye suala la uwepo wa magonjwa.

Kwa mujibu sheria hiyo Dr. Mwele amekosea. Hata hivyo, kuna Sheria na Busara ya kawaida. Kwa busara ya kawaida kuna kujiuliza kama je, ilishatosha kosa hilo kumtengua Mwele au alistahili onyo? Nayo ni sehemu ya majadiliano.

Lasivyo, kwa kiasi kidogo ninacho mfahamu Dr. Mwele , ana hekima, uzoefu na ujuzi usiotiliwa shaka ktk tasnia hii ya magonjwa na tafiti. Tatizo lipo kwenye utaratibu wa kuuhabarisha umma.
Taratibu za serikali za kutangaza matokeo ya utafiti ni zipi mkuu?
 
Zika na NIMR

Dk. Mwele Ntuli Malecela leo si Mkurugenzi tena wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Ikulu leo imemtangaza Profesa Yunus Mgaya kuwa mbadala wake.

Kwanini Mwele kaondolewa? Nimeulizwa hili swali na baadhi ya watu nami nikauliza hapa na pale ili kupata majibu. Na hili ndilo nililoambiwa.

Mosi, kwamba ugonjwa wa Zika upo Tanzania. Ugonjwa huu ulianzia Uganda na upo pia kwetu kwa muda mrefu. Ila upo katika hali iliyodhibitiwa, wataalamu wanaitwa Endemic. Si tatizo kubwa lakini upo.

Lakini Tanzania haina tatizo la ZIKA. Kwa jinsi tatizo la ugonjwa huo lilivyo kubwa, kabla halijatangazwa, kuna taratibu za kufuatwa ikiwamo kuhusisha Serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Imefanyika hivi kwa sababu madhara ya kutangaza ugonjwa huo kwa taifa ni makubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tatizo ni kwamba tangazo la Mwele halikufuata hizo taratibu. Na zaidi, halikuzingatia athari ambazo zingejitokeza kwa yeye kutoa taarifa kama zile.

Kwenye Kiswahili, tofauti ya maneno Endemic na Epidemic ( ugonjwa uliodhibitiwa na uliolipuka) ni ndogo. Ukisema Zika ipo, magazeti yatasema ZIKA imeingia.

Sasa, labda, Rais mwingine, kwenye Serikali nyingine, angeweza ˊkupotezea` tu kauli ile ya Mwele. Lakini binti huyu wa mzee John Malecela hakuwa amesoma vema alama za nyakati.

Hivyo, kwa maana ya kosa, Mwele alikosea. Ishu ya ZIKA haikuwa ya kutangazwa na taasisi yake pekee bila kuhusisha serikali na wadau wengine.

Hivyo, hapa, tatizo si serikali kukataa taarifa ya kitaalamu. Ni kwamba mhusika amekiuka taratibu ambazo zimewekwa. Na huo ugonjwa haujaja sasa hivi. Upo siku nyingi ila umedhibitiwa.
We huo utaft wako umeufanyia WAP?nawew utaka cheo nin man huko siokujipendekeza had kumepitiliza..mijitu mingne bana
 
1481981938150.jpg
 
Labda tusaidiwe zika inasabishwa na nini?

Kama ni mbu ndio wanaosambaza virus, ukisema una control ina maana kuna chanjo au hao mbu umewadhibiti.

Sasa what is stopping the epidemic bila ya jitihada zozote za kupambana na zika, au labda tafiti zao zinasema katika watu 5000 watakaong'atwa na mmbu mmoja tu ndio anaweza pata.

Vinginevyo it does not make sense on how it is not a national problem given the nature of its causes and on what little has been done to control it.
 
Huyu Prof Yunus Mgaya si alikuwa Udsm? Sasa kila ma-prof wanakuwa wakurugenzi wa taasisi za umma ,who gonna teach at university? Aau Ma T.A
 
Zika na NIMR

Dk. Mwele Ntuli Malecela leo si Mkurugenzi tena wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Ikulu leo imemtangaza Profesa Yunus Mgaya kuwa mbadala wake.

Kwanini Mwele kaondolewa? Nimeulizwa hili swali na baadhi ya watu nami nikauliza hapa na pale ili kupata majibu. Na hili ndilo nililoambiwa.

Mosi, kwamba ugonjwa wa Zika upo Tanzania. Ugonjwa huu ulianzia Uganda na upo pia kwetu kwa muda mrefu. Ila upo katika hali iliyodhibitiwa, wataalamu wanaitwa Endemic. Si tatizo kubwa lakini upo.

Lakini Tanzania haina tatizo la ZIKA. Kwa jinsi tatizo la ugonjwa huo lilivyo kubwa, kabla halijatangazwa, kuna taratibu za kufuatwa ikiwamo kuhusisha Serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Imefanyika hivi kwa sababu madhara ya kutangaza ugonjwa huo kwa taifa ni makubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tatizo ni kwamba tangazo la Mwele halikufuata hizo taratibu. Na zaidi, halikuzingatia athari ambazo zingejitokeza kwa yeye kutoa taarifa kama zile.

Kwenye Kiswahili, tofauti ya maneno Endemic na Epidemic ( ugonjwa uliodhibitiwa na uliolipuka) ni ndogo. Ukisema Zika ipo, magazeti yatasema ZIKA imeingia.

Sasa, labda, Rais mwingine, kwenye Serikali nyingine, angeweza ˊkupotezea` tu kauli ile ya Mwele. Lakini binti huyu wa mzee John Malecela hakuwa amesoma vema alama za nyakati.

Hivyo, kwa maana ya kosa, Mwele alikosea. Ishu ya ZIKA haikuwa ya kutangazwa na taasisi yake pekee bila kuhusisha serikali na wadau wengine.

Hivyo, hapa, tatizo si serikali kukataa taarifa ya kitaalamu. Ni kwamba mhusika amekiuka taratibu ambazo zimewekwa. Na huo ugonjwa haujaja sasa hivi. Upo siku nyingi ila umedhibitiwa.
Huo ndio ukweli mtupu. sasa wenye hasira na serikali na jpm in particular utawasikia wanavyobwabwaja.
 
Yeye katangaza tafiti ya kisayansi, na anatangazaga kila siku. Hivi mwananchi wa kawaida utataka kujua kuwa ugonjwa upo? au utataka kujua aliyesema ni nani? Kwangu ni bora nijue ugonjwa upo ili nichukue tahadhari, sio mnifiche kwa kigezo cha kuusubiria uwe epidemic ili mimi ndio niwe statistic
Kaka utaratibu ndio unaozungumziwa. Soma uelewe usibishe tu kila kitu
 
..lakini kumfukuza kazi ndiyo kumezua taharuki kubwa na kusababisha athari/ damage kubwa zaidi.

..at least wangempa nafasi Dr.Mwele kama mtafiti afafanue atolee maelezo matokeo ya utafiti wake.

..kwa hatua ya kumfukuza haraka haraka Mkurugenzi mkuu wa NIMR kunajenga picha kwamba serikali inaficha ukweli.

..wizara na serikali kwa ujumla wanatakiwa wewe very careful na habari hizi. Wanatakiwa wachukue hatua za haraka na tahadhari ili kuepusha nchi kuingia ktk mlipuko wa zika.

Cc TUNTEMEKE
 
Zika na NIMR

Dk. Mwele Ntuli Malecela leo si Mkurugenzi tena wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR). Ikulu leo imemtangaza Profesa Yunus Mgaya kuwa mbadala wake.

Kwanini Mwele kaondolewa? Nimeulizwa hili swali na baadhi ya watu nami nikauliza hapa na pale ili kupata majibu. Na hili ndilo nililoambiwa.

Mosi, kwamba ugonjwa wa Zika upo Tanzania. Ugonjwa huu ulianzia Uganda na upo pia kwetu kwa muda mrefu. Ila upo katika hali iliyodhibitiwa, wataalamu wanaitwa Endemic. Si tatizo kubwa lakini upo.

Lakini Tanzania haina tatizo la ZIKA. Kwa jinsi tatizo la ugonjwa huo lilivyo kubwa, kabla halijatangazwa, kuna taratibu za kufuatwa ikiwamo kuhusisha Serikali na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Imefanyika hivi kwa sababu madhara ya kutangaza ugonjwa huo kwa taifa ni makubwa kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Tatizo ni kwamba tangazo la Mwele halikufuata hizo taratibu. Na zaidi, halikuzingatia athari ambazo zingejitokeza kwa yeye kutoa taarifa kama zile.

Kwenye Kiswahili, tofauti ya maneno Endemic na Epidemic ( ugonjwa uliodhibitiwa na uliolipuka) ni ndogo. Ukisema Zika ipo, magazeti yatasema ZIKA imeingia.

Sasa, labda, Rais mwingine, kwenye Serikali nyingine, angeweza ˊkupotezea` tu kauli ile ya Mwele. Lakini binti huyu wa mzee John Malecela hakuwa amesoma vema alama za nyakati.

Hivyo, kwa maana ya kosa, Mwele alikosea. Ishu ya ZIKA haikuwa ya kutangazwa na taasisi yake pekee bila kuhusisha serikali na wadau wengine.

Hivyo, hapa, tatizo si serikali kukataa taarifa ya kitaalamu. Ni kwamba mhusika amekiuka taratibu ambazo zimewekwa. Na huo ugonjwa haujaja sasa hivi. Upo siku nyingi ila umedhibitiwa.

Shida kubwa iko kwenye utaratibu wa kugawana vyeo, hiyo nafasi ilipaswa kutangazwa na watu waombe ili atakayepatikana ajue ana ripoti kwa nini?

Sasa waziri wa Afya anateuliwa na Raisi na Dr Mwele kateuliwa Raisi hapo wote wana ndevu, Dr. mwele ataripoti kwa nani?
 
inawezekana ni kweli amekiuka taratibu lkn najaribu kuwaza zaidi.hivi huyu Dr Mwele si ni mtoto wa mzee Malecela ambaye ni miongoni mwa waasisi wa chama anachokiongoza mh Rais?ni hivi karibuni tu huyu huyu mtukufu alitengua uteuzi wa mke wa mzee Malecela mama Anne Kilango.kibinadamu inaonekana ni kama maamuzi ya mtukufu yanailenga moja kwa moja familia ya mzee huyu na inaweza ikawa na madhara makubwa kibinadamu.ilitosha kumuonya badala ya hatua kama aliyofanya mtukufu.hata hao ni binadamu wenye nyama na damu na mioyo inayosikia uchungu.
 
Back
Top Bottom