Kosa kubwa la watanzania na wafrika wote kwa ujumla ni kuabudu watu badala ya principles na integrity.

Kosa kubwa la watanzania na wafrika wote kwa ujumla ni kuabudu watu badala ya principles na integrity.

joseph2

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2015
Posts
458
Reaction score
1,032
ukiangaria siasa za Tanzania na afrika kwa ujumla kama ni mtu unaye fikiri vizuri utaona kunashida kubwa katika nchi zote za Africa.
Shida kubwa sio tu kwa viogozi wa Africa tu bali hata raia wa Africa wote walisha kuwa watu wa kuabudu watu badala ya kuwalazimisha kufuwata principles na integrity. Kwa vile mimi ni mtanzania acha nitumie watanzania kama mfano wa tamaduni za kuabudu watu badala ya kujiwekea utaratibu wa kufanya vitu vyao.
Hii tabia ya kuabudu watu inaigjarim taifa na bara Zima la afrika vibaya sana. Kwa Tanzania ndio kabisa hili suala limekuwa kubwa kwa kiwango cha kutisha. Mfano mzuri ni uchaguzi wa chadema wa kuchaguwa viongozi wa taifa kwenye chama hicho . Ukisikia supporters wa pande mbili wa Mbowe na Lisue wote ni waumini wa mtu, badala ya kuwa waumini wa sera za mtu. Kwa mfano Mbowe alivyo tangaza kugombea nafasi ya uenyekiti kwa mara ya tano hakutaja hata sera moja atakayo tekeleza andapo atachaguliwq tena. Pamoja na kutotaja sera yoyote, waumini wake wanaamini kuwa ndiye mtu sahihi wa kuongoza chama. Maana wafuwasi wake wanamuamini kama wa fuwasi wa yesu wanavyo mwamini yesu kuwa atakuja kuwaokowa.
Wafuwasi wa Lissu pamoja na kwamba kuwa yeye alisema sera zake ni za kufanya mabadiliko kwenye chama ikiwemo sera ya kuweka term limit kwa kila nafasi ya uongozi ndani ya chama. Ila ukisikiliza wafuwasi wake wengi wanajikita kumsifia zadi badala ya kuelezea namna atakavyo tekeleza sera zake.

Mfano mwingini ni wafuwasi wa ccm . Ukisoma katiba ya ccm imejaa sera zuri nyingi sana . Lakini huwezi kusikia mwanachama wa ccm hata mmoja akiuza sera za chama. Wengi utawasikia wakisifia viogozi zaidi . Mpaka wengine wamefikia hatuwa ya kujiita chawa wa viongozi.

Tukitoka kwenye siasa ukija kwenye makanisa watu hawaendi tena kwenye majuba ya kuabudia kuabudu muumba wao wanakwenda kuabudu viongozi au wamiliki wa majumba ya kuabudia. Watu wanatambulisha mazehebu yao kwa majina ya viongozi wa majumba ya kuabudia badala ya imani zao. Kwa mfano utasikia mimi nasali kwa kakobe, au kwa mzee wa upako nk. Sasa unajiuliza hivi hao viogozi wa majumba ya kuabudia wanatafauti gani na watu wengine mpaka mtu afikiri kuwa wanauwezo wa kuongea na muumba wa dunia kuliko watu wengine.?

Shida ya kuabudu watu ilianza kabula ya ukoloni ila kabla ya ukoloni watu walio kuwa wanaabudiwa walikuwa kweli ni watu wema ambao walikuwa na maono makubwa kwaajiri jamimi zao . Na walikuwa wanaheshimika kwa kuwa na mienendo mizuri sana. Pia walikuwa sio watu wa kupenda kujinufaisha wao wenyewe. Walikuwa ni watu wa jamii. Watu waliwamini sana na watu waliwatii bila kulazimishwa. Na kweli afrika nzima kabla ya wageni kuingia kulikuwa hamna uhalifu wowote. Kama kungetokea uhalifu . Kiongozi aliita watu wote kukusanyika pamoja na kuamlisha aliye tenda uhalifu akiri uhalifu wake .

Na mara moja mhalifu alitoka mbele na kuadhibiwq mbele ya watu wote. Na kamwe asinge rudia tena. Sasa warabu na wazungu walivyo ingia afrika wakashangaa sana kuona wafrika wote wanaishi kwa amani na utulivu bila hata kuwa na majeshi.

Kwasababu wazungu na warabu kwao walisha zowea kuuwana kwa kunyanganyana mali, wakawa hawaelewi kwanini wafrika wana mali nyingi lakini hawagombani. Hilo likawafanya watafute njia za kuiba mali za wafrika. Na katika kufanikisha hilo ikabidi watumiae imani za kiafrika walizo zikuta ila kuzibadilisha maudhui na makusudi yake .

Thana ya ya kijamii ikaomdolewa. Ikawa dhana ya diniutwalaawala wa serikali za kikoloni. Na kwasababu wafirika tiayari tulisha zowea kuamini viongozi wetu basi wazungu na waarabu wakaanza kutengeneza manabiii wa dini zao . Kina yesu na mhamadi wakawa ndio pekee wanao faa kuabudiwa.

Warabu na wazungu wakaanza kudharilisha viongozi wetu wa kiafrika na kuwaita wapagani au witchcraft men. Wao wakaanza kujifanya kuwa ndio watu wazuri kumbe nia yao ni kuiba mali za waafrika. Basi wakaendelea hivyo kwa miaka mingi sana hata mitaala ya elimu kwa watoto ikawa ya kuabdu wazungu na kuona waafrika kama watu duni wasio juwa chochote.

Kibaya zaidi hata wapigania uhuru kwasababu walikuwa ni mazao ya elimu za kikoloni na kitumwa .
Viongozi wa kiafrika, Walivyo kabidhiwa uhuru wa nchi zao ,wengi wao walikuwa hawajui maana ya kujitawala walifikiri kujitawala ni wao kuwa viongozi wa kudumu. Na karibia kila kiongozi alichukuwa madaraka baada ya ukoloni eidha alifia madarakani au alipiduliwa . Pili viongozi wengi walio kabidhiwa uhuru hawakubadilisha mifumo ya utawala, wala mifumo ya elimu.

Uhuru wa Afrika ulikuwa ni uhuru wa kubadilisha rangi ya watawala. Yaani kutoka kutawaliwa na wazungu na warabu na kutawaliwa na watu weusi kama sisi kwa kutumia njia zilezele za kikoloni. Wageni walivyo ondoka waliacha mifumo yao ya elimu na kiutawala ikiendelea kufanya kazi kwaajiri ya faidi ya nchi za kikoloni. Ndio maana mpaka leo vitabu vya kufundishia kwenye shule zetu vingi vimetungwa uraya .

Ili kuhakikisha hilo linafanikiwa waliondowa viondowa wanasiasa wao na wakarudisha wamishenari. Amboa walihakikisha utamaduni wa wafrika unazikwa . Utamaduni wa kiarabu na kizungu unashamiri Afrika nzima, kwa njia ya dini zao. Leo Inteendelea.
 
Back
Top Bottom