Kosa kubwa watu wengi wanafanya wakiharibikiwa gari.

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2020
Posts
3,381
Reaction score
9,744
Kukosa mtu sahihi wa kurekebisha tatizo la gari lako.

Moja kati ya makosa ambayo nimeyaona kwa kipindi kirefu ni hili.

Mtu anakuwa na mawazo kichwani kwamba Fundi mmoja anaweza kufix matatizo yote kwenye gari yake. (Sisemi kwamba hili haliwezekani, ila linawezekana kwa wale wenye magereji makubwa tu).

Kama mmekutana mtandaoni angalia kazi anazopost halafu linganisha na tatizo. Bila shaka utakuwa na majibu kama atakuwa mtu sahihi wa kusolve tatizo lako au lah.

Sasa watu wengi ataona kwa sababu mtu fulani alieleza kitu fulani vizuri then huyo mtu vitu vingi kwenye gari anaweza. Kitu ambacho siyo sawa.

Kwa mfano mimi ishu nyingi ninazodeal nazo zinahusu Check engine na warning lights zingine lakini kuna watu wanapiga anakuambia bhana gari yangu inagonga kwenye matairi, au nataka kubadilisha kioo cha mbele, au nataka kubadilisha kitasa na mambo mengine ambayo ni irrelevant kwangu.

Point yangu ni kwamba kuna siku utamueleza fundi shida yako ambayo haipo katika kazi ambazo ana ujuzi nazo. Kwa sababu ana shida ya hela atakuambia anaweza. Na huo ndio mwanzo wa kuharibiwa gari.

At least jitahidi kujua kitu fulani kwenye gari yako kikileta shida utampigia nani simu. Siyo tu kumpigia mtu yoyote.
 
Matangazo ya huyu ndugu yapo kimkakati sana sema sasa comment hajibu .... kama juzi nlimuliza kuhusu matumizi ya mafuta( isiyo kawaida inasabishwa na nni) kwenye gri IST ...kimya ..... haya na hii pia uta kaa kimya let's wait
 
Kuna baadhi ya mafundi hawezi kukwambia kama mambo ya wiring hajui lakini atajaribu mpaka aharibu. Au atajifanya anajua na kumpa mtu mwengine kazi nae hutia chake hapo kwenye malipo.

Mjini kuna mengi sana😂
 
Matangazo ya huyu ndugu yapo kimkakati sana sema sasa comment hajibu .... kama juzi nlimuliza kuhusu matumizi ya mafuta( isiyo kawaida inasabishwa na nni) kwenye gri IST ...kimya ..... haya na hii pia uta kaa kimya let's wait
Mkuu swali lako la ulaji wa mafuta unasababishwa na nini ni swali gumu sababu karibu kila kitu kwenye engine kikizingua kinaweza kupelekea hiyo shida, Spark plug, ignition coils, maf sensor, ect sensor, pump, nozzle, EVAP canister, Camshaft na crankshaft position sensor, iat sensor, vvt solenoid, Vacuum leak, n.k. hapo sijagusa gearbox na matakataka mengine.

So unaweza kujikuta umebadili kila kitu kwenye gari na shida yako isipone.

Kama umeshahangaika na ishu yako bado iko vilevile, njoo tucheck na sisi.
 
Naweza nikasema kuwa umekwiva huna tamaa yaani umeongea kitalaamu. Kwa kifupi haikutakiwa kuwa kwenye hizi assholes countries masikini ambazo mwanasiasa la saba Ni professional kwenye afya anamkosoa tabibu na kupima young moduli za various materials like block cement kwa kulipigiza chini. Mwishowe wataanza kucheki ishu za ndoa Kama unamnanihii vizuri mmeo mkeo sio ndio hapo wataanza kuwapima kwa kuishi nao mwezi mzima
 
Mkuu swali lako la ulaji wa mafuta unasababishwa na nini ni swali gumu sababu karibu kila kitu kwenye engine kikizingua kinaweza kupelekea hiyo shida, Spark plug, ignition coils, maf sensor, ect sensor, pump, nozzle, EVAP canister, Camshaft na crankshaft position sensor, iat sensor, vvt solenoid, Vacuum leak, n.k. hapo sijagusa gearbox na matakataka mengine.

So unaweza kujikuta umebadili kila kitu kwenye gari na shida yako isipone.

Kama umeshahangaika na ishu yako bado iko vilevile, njoo tucheck na sisi.
Upo wapi
 
Kukosa mtu sahihi wa kurekebisha tatizo la gari lako.

Moja kati ya makosa ambayo nimeyaona kwa kipindi kirefu ni hili.

Mtu anakuwa na mawazo kichwani kwamba Fundi mmoja anaweza kufix matatizo yote kwenye gari yake. (Sisemi kwamba hili haliwezekani, ila linawezekana kwa wale wenye magereji makubwa tu).

Kama mmekutana mtandaoni angalia kazi anazopost halafu linganisha na tatizo. Bila shaka utakuwa na majibu kama atakuwa mtu sahihi wa kusolve tatizo lako au lah.

Sasa watu wengi ataona kwa sababu mtu fulani alieleza kitu fulani vizuri then huyo mtu vitu vingi kwenye gari anaweza. Kitu ambacho siyo sawa.

Kwa mfano mimi ishu nyingi ninazodeal nazo zinahusu Check engine na warning lights zingine lakini kuna watu wanapiga anakuambia bhana gari yangu inagonga kwenye matairi, au nataka kubadilisha kioo cha mbele, au nataka kubadilisha kitasa na mambo mengine ambayo ni irrelevant kwangu.

Point yangu ni kwamba kuna siku utamueleza fundi shida yako ambayo haipo katika kazi ambazo ana ujuzi nazo. Kwa sababu ana shida ya hela atakuambia anaweza. Na huo ndio mwanzo wa kuharibiwa gari.

At least jitahidi kujua kitu fulani kwenye gari yako kikileta shida utampigia nani simu. Siyo tu kumpigia mtu yoyote.
Huna baya ka mkubwa
 
Back
Top Bottom