Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Wanasiasa hufanya makosa mengi sana wakiwa madarakani. Wanapoyafanya huwa hawana uwezo wa kupima ukubwa na madhara ya wanachokusudia kukifanya. Ni pale wanapokuwa wanapokea lawama nyingi ndio hujisumbua kuangalia kwa kina namna ambavyo wangeweza kuzuia kile walichokifanya, wangefanya hivi na wakafanya vile ndio huwa ni wazo lililochelewa wakati wake. Wanapokuwa wakiamua kufanya maamuzi yanayoongozwa na upofu au ulevi wa madaraka huwa wamezungukwa na wapambe wanaosema kitu wanachotaka kukisikia. Wao kuwa na maamuzi ya mwisho wakati mwingine huwanyima ile busara ya kuwa mawazo yao sio kila wakati huwa ndio ya kutekelezwa na yakaja na jibu lililokusudiwa na lenye faida.
Rais wa Russia Vladmir Putin anataka kufanya kosa litakalompa umaarufu mbovu kama ule aliokuwa nao Adolph Hitler mwaka 1939. Putin anataka kufanya kosa kama lile alilolifanya Idd Amin mwaka 1978 kwa kuivamia sehemu ya mkoa wa Kagera, kipigo alichokipata kilimpoteza kabisa miongoni mwa viongozi wa mataifa waliostahili heshima kila walipokatiza. Putin ameiangalia Ukraine katika udogo wake kwa kuilinganisha na Russia hivyo anaamini kwamba anaweza kufanya lolote na dunia ya sasa ikatulia tu na kumtazama. Kitakachompata kitakuwa ni fedheha kama ile iliyomkuta Hitler ambaye aliishia kujinyonga baada ya vita kumalizika akiwa ameshindwa vibaya.
Anatakiwa kukumbushwa kuwa Volodymyr Zelensky licha ya kuwa ni rais wa Ukraine taifa huru lenye maamuzi huru kama ilivyo Russia pia ni myahudi. Kwa asili ya wayahudi huwa ni watu wenye mtandao ulio hai na makini siku zote. Wayahudi wanajuana popote walipo, na mwanasiasa ambaye hata kama upande wa Mama ndio wayahudi huwa wanamchukulia kama ni mtoto wao. Wayahudi wanalinda ushawishi walionao duniani kote. Na ni rahisi kwao kumpachika jina la 'anti semitic' yoyote yule anayekwenda kinyume na falsafa zao au anayewakejeli.
Sembuse maamuzi ya Putin kuivamia nchi huru ya Ukraine inayoongozwa na myahudi mwenzao!!. Putin anakosa washauri wenye kutazama mbali, wenye ushawishi wa kidunia. Atumie busara sana kwani anachofikiria dhidi ya Ukraine kinaweza kumpoteza kabisa na yale yote aliyokwisha kuyafanya tangu 1999 alipoanza kuongoza Russia yakafunikwa na huu 'ujinga' anaouwazia kwa sauti ya juu.
Ulimwengu wa 1939 wakati Hitler akiivamia Austria sio huu wa 2022. Zimetungwa sheria nyingi za kimataifa zinazolinda uhuru wa kila taifa. Wamezaliwa wanasiasa wenye maarifa mazito ya kuongoza. Sayansi haijabaki nyuma zimeundwa silaha za hatari zenye kuweza kuangamiza kila kilichopo juu ya uso wa dunia ndani ya saa chache tu. Anaumizwa sana na ushawishi wa USA kwa jirani yake wa karibu, lakini nguvu nyingi hutumiwa na mwenye maarifa madogo ya uongozi.