Kosa la Adolph Hitler la Septemba mosi 1939 linataka kurudiwa na Vladimir Putin

Kosa la Adolph Hitler la Septemba mosi 1939 linataka kurudiwa na Vladimir Putin

Mkuu Rais wa Ukraine ni myahudi. Kumbuka hawa watu waliuliwa zaidi ya milioni moja kule Poland hivyo tangu wakati huo wana umoja wa ajabu.

Kuvamia nchi nyingine kwa sababu zisizoingia kichwani ni ngumu sana. Ni kweli si Saddam lakini udikteta wa Hitler kwa karne hakuna atakayeuvumilia.
Us alipoingia Libya, Iraq, Afghan na kuua mamilion ya watu ilikua sawa?
 
Wamarekani/Wazungu hawana ubavu wa kuingia vitani na Warusi.

Sanasana watamwekea vikwazo vya kiuchumi tu na mwisho wataufyata.

After all Warusi hawawategemei sana Wamarekani/Wazungu.

Kwahiyo Warusi wameupiga mwingi.
 
Hao wayahudi wako bila mbeleko ya huyo tapeli marekani wana nini?!

Au na wewe ni mmoja wa wanaoamini kuwa hawa matapeli wanaojiita wayahudi ndilo lile tunalosoma kwenye Biblia kama taifa teule la Mungu?
Dunia inaangalia mchango wako ni upi. Substance ya kwako ni ipi. Myahudi anao mchango kuanzia masuala ya teknolojia mpaka yale ya muziki.

Kulialia tu na kulalamika ni sifa ya mwafrika, ambaye siku zote anahisi kuwa anaonewa, ukiwa na mchango katika uhai hutalia kuonewa, unachokichangia ndio kitakachokupa heshima.
 
Hayo maneno yamezoeleka kwa wakongwe.Walianza chawa wa Saddam kupiga kelele na kujidai USA hawezi kuwafanya lolote.
Wakafuata vimbwenerehi wa Afghanistan huku wakiwa na magobole yao milimani Torabora na Kandahar.Mwishowe walitoa mlio wa huzuni.
Fact. Hao warusi wa mtogole wenyewe ni kushabikia uongo tu. Utasikia hapo USA hagusi. Lakini ikianza wanaanza kulialia tu oooh...! Anaonea tu.
 
Biden kila akipiga calculations za siasa USA, mahesabu yanakataa kabisa kuzama mazima kwny huu mgogoro, anajua akifanya mahesabu vibaya uchaguzi ujao anangolewa mapema sana, tofauti na Putin ambaye kwa sasa hana msukumo huo, ndiyo maana kashatia miguu kabisa. Kwhy Biden ni kuchgua aingie mazima au aendelee na danadana ili abaki madarakani.
 
Wanasiasa hufanya makosa mengi sana wakiwa madarakani. Wanapoyafanya huwa hawana uwezo wa kupima ukubwa na madhara ya wanachokusudia kukifanya. Ni pale wanapokuwa wanapokea lawama nyingi ndio hujisumbua kuangalia kwa kina namna ambavyo wangeweza kuzuia kile walichokifanya, wangefanya hivi na wakafanya vile ndio huwa ni wazo lililochelewa wakati wake. Wanapokuwa wakiamua kufanya maamuzi yanayoongozwa na upofu au ulevi wa madaraka huwa wamezungukwa na wapambe wanaosema kitu wanachotaka kukisikia. Wao kuwa na maamuzi ya mwisho wakati mwingine huwanyima ile busara ya kuwa mawazo yao sio kila wakati huwa ndio ya kutekelezwa na yakaja na jibu lililokusudiwa na lenye faida.

Rais wa Russia Vladmir Putin anataka kufanya kosa litakalompa umaarufu mbovu kama ule aliokuwa nao Adolph Hitler mwaka 1939. Putin anataka kufanya kosa kama lile alilolifanya Idd Amin mwaka 1978 kwa kuivamia sehemu ya mkoa wa Kagera, kipigo alichokipata kilimpoteza kabisa miongoni mwa viongozi wa mataifa waliostahili heshima kila walipokatiza. Putin ameiangalia Ukraine katika udogo wake kwa kuilinganisha na Russia hivyo anaamini kwamba anaweza kufanya lolote na dunia ya sasa ikatulia tu na kumtazama. Kitakachompata kitakuwa ni fedheha kama ile iliyomkuta Hitler ambaye aliishia kujinyonga baada ya vita kumalizika akiwa ameshindwa vibaya.

Anatakiwa kukumbushwa kuwa Volodymyr Zelensky licha ya kuwa ni rais wa Ukraine taifa huru lenye maamuzi huru kama ilivyo Russia pia ni myahudi. Kwa asili ya wayahudi huwa ni watu wenye mtandao ulio hai na makini siku zote. Wayahudi wanajuana popote walipo, na mwanasiasa ambaye hata kama upande wa Mama ndio wayahudi huwa wanamchukulia kama ni mtoto wao. Wayahudi wanalinda ushawishi walionao duniani kote. Na ni rahisi kwao kumpachika jina la 'anti semitic' yoyote yule anayekwenda kinyume na falsafa zao au anayewakejeli.

Sembuse maamuzi ya Putin kuivamia nchi huru ya Ukraine inayoongozwa na myahudi mwenzao!!. Putin anakosa washauri wenye kutazama mbali, wenye ushawishi wa kidunia. Atumie busara sana kwani anachofikiria dhidi ya Ukraine kinaweza kumpoteza kabisa na yale yote aliyokwisha kuyafanya tangu 1999 alipoanza kuongoza Russia yakafunikwa na huu 'ujinga' anaouwazia kwa sauti ya juu.

Ulimwengu wa 1939 wakati Hitler akiivamia Austria sio huu wa 2022. Zimetungwa sheria nyingi za kimataifa zinazolinda uhuru wa kila taifa. Wamezaliwa wanasiasa wenye maarifa mazito ya kuongoza. Sayansi haijabaki nyuma zimeundwa silaha za hatari zenye kuweza kuangamiza kila kilichopo juu ya uso wa dunia ndani ya saa chache tu. Anaumizwa sana na ushawishi wa USA kwa jirani yake wa karibu, lakini nguvu nyingi hutumiwa na mwenye maarifa madogo ya uongozi.
CcDotworld
 
Russia hawezi kupigwa na NATO hata siku moja uliona alivyoliokota jimbo la Crimea ?
 
Mkuu Rais wa Ukraine ni myahudi. Kumbuka hawa watu waliuliwa zaidi ya milioni moja kule Poland hivyo tangu wakati huo wana umoja wa ajabu.

Kuvamia nchi nyingine kwa sababu zisizoingia kichwani ni ngumu sana. Ni kweli si Saddam lakini udikteta wa Hitler kwa karne hakuna atakayeuvumilia.
Last time i checked crimea was part of ukraine.


Ila huyuhuyu Putin aliichukua na Us wakaingia mitini.
 
Biden kila akipiga calculations za siasa USA, mahesabu yanakataa kabisa kuzama mazima kwny huu mgogoro, anajua akifanya mahesabu vibaya uchaguzi ujao anangolewa mapema sana, tofauti na Putin ambaye kwa sasa hana msukumo huo, ndiyo maana kashatia miguu kabisa. Kwhy Biden ni kuchgua aingie mazima au aendelee na danadana ili abaki madarakani.
Marekani haitegemei maamuzi ya mtu mmoja haswa yale maamuzi yanayolenga masirahi mapana ya taifa.

Ambacho wengi hamkijui ni kuwa hakuna nchi inayopenda vita kati ya hizo zote na zaidi marekani,maana marekani siku zote hayupo kwaajili ya hasara isipokuwa faida tu!. Vita ni hasara na kwasasa ukiingia vitani na taifa kubwa Kama Russia haitakuwa Vita ya kizembe hata Kama utashinda vita hiyo ila utatoka ukiwa kilema!.

Marekani anauhasama na mataifa mengi so kuingia vitani ni sawa na kuwapa cheko adui zake wajiunge na wamtifue!..

Hao wanaoshabikia uyahudi waache kushikwa akili kijinga hivyo!,achaneni na propaganda za myahudi ametapakaa damu tupu so siamini taifa la Mungu linaweza kutapakaa damu kiasi hiki,imani ni ugonjwa Tena ni ugonjwa zaidi usipojua imani yako ipoje.
 
Back
Top Bottom