Kosa la mwaka 1960-1975 linajirudia mwaka 2015

Mkuu umenena ila serikali hasa kupitia bunge ambalo lina wawakilishi wa ccm wengi limekuwa halina usikivu hata pale panapotakiwa kuweka uchama pembeni na kuweka maslahi ya taifa mbele kazi kubwa ya waTz kufanya sasa ni kuhakikisha ccm imetoka madarakani ili tuwe huru kuandaa katiba itakayotufaa waTz kwa pamoja
 
Yericko,

Kwa faida ya JF tufahamishe PhD ya Dr. Vedasto Kyaruzi alisoma wapi.

Acha sarakasi zako hizo huku ukiwa umejifunga msuli. JF ni darasa huru kama unafahamu historia ya Dr. Kyaruzi we tupia tu wala usianzishe ligi ya mchangani hapa.
 
wewe kweli kobe, umeelewa nini? Kweli unaamini wakati tunapata uhuru wasomi walikuwa wawili tu?

wewe ritz unamaanisha nini unapomwita mwenzio "kobe"tueleze wewe unayejua kwa details otherwise hata wewe.....umbile/shape ya maji huoneka ilivyo kulingana na chombo kilivyo.
 
Acha sarakasi zako hizo huku ukiwa umejifunga msuli. JF ni darasa huru kama unafahamu historia ya Dr. Kyaruzi we tupia tu wala usianzishe ligi ya mchangani hapa.
Wewe vipi! Mimi nimeuliza kujua hii ni forum wewe mbona umechangia hakuna aliyekuuliza.
 
wewe ritz unamaanisha nini unapomwita mwenzio "kobe"tueleze wewe unayejua kwa details otherwise hata wewe.....umbile/shape ya maji huoneka ilivyo kulingana na chombo kilivyo.
Jamaa anaitwa Kobe,
 
Last edited by a moderator:
Yericko,

Kwa faida ya JF tufahamishe PhD ya Dr. Vedasto Kyaruzi alisoma wapi.

nilitegemea ungejibu kwanza swali na ww ndo uulize swali kinyume chake umeuliza swali juu ya swali
 
Mkuu Ritz,

Kuna tatizo kubwa katika uelewa wako, ujengaji wa hoja na ujibuji wa hoja husika,

Kwanza nilikuuliza unitajie Watanganyika waliokuwa na elimu za juu zaidi ya Dr Kyaruzi na Nyerere,


Ukajibu hivi:

Unafamhamu Dr. Mutahangarwa? Unafahamu Dr. Lugaiza? Wapo wengi tuanze na hawa unajua elimu zao?

Nikakuomba utupatie wasifu wa hao madaktari kabla na baada ya uhuru,

Badala ya kujibu swali, Ukaja ukajibu hivi:

"Tuambie Dr Vedasto Kyaruzi alisomea wapi?"

Na hata nilipojarubu kukurudisha uendelee na mtiririko vizuri wa hoja, ukajibu hibu hivi:

Wewe ndiyo umekosa mwelekeo tena umeleta dharau umenipa na orodha ya watu nikawaulize.

Nimekuuliza Dr. Vedasto Kyaruzi kasomea wapi PhD?

Sasa pima mwenyewe mkuu,

Niendelee kujadiliana na wewe au nifanye mengine?
 
Mbona haujaweka orodha ulioniambia nikawaulize kina gombesugu?

Mimi sijadiliani na wewe ninachofanya ni kuwapasha habari wasomaji kuwa siyo kweli kuwa wakati tunapata uhuru wasomi walikuwa wawili.
 

Kamanda karibu sana,

Tunahitaji fikra mpya na zenye nguvu katika suala hili,

Ninachofurahi maishani mwangu nikuwa huwa naamini siasa za leo hapa Tanzania Chadema ni makutano ya Watanzania wenye fikra huru!
 
Last edited by a moderator:
Mbona haujaweka orodha ulioniambia nikawaulize kina gombesugu?

Mimi sijadiliani na wewe ninachofanya ni kuwapasha habari wasomaji kuwa siyo kweli kuwa wakati tunapata uhuru wasomi walikuwa wawili.

Hapa ndipo unapopotosha,

Soma vizuri nilichoandika mkuu, kama hujui kusoma na kutafsiri maandiko omba ufafanuzi,

Nilichosema nikuwa Tanganyika haikuwa na wasomi "WA NGAZI" ya Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu zaidi ya watu wawili tu yani Daktari Vedasto Kyaruzi na Mwalimu Julius Nyerere,

Hivyo lete kile unachokijua nje ya nilicholeta mkuu,
 
nilitegemea ungejibu kwanza swali na ww ndo uulize swali kinyume chake umeuliza swali juu ya swali
Mkuu kama utakuwa hujamsoma mkuu wetu Ritz hapa jf, basi hilo ndio tatizo lake kuu,

Nimejadiliana nae mahala pengi sana ndani ya jukwaa hili hivyo ndivo alivyo!
 

Kiukweli huyu ritz simuelewi kabisa na inavyoonesha kuna jambo analijua if not basi kaamua kusumbua akili zetu.sasa basi wewe ritz utuambie orodha ya wasomi waliokuwepo b4 uhuru na wasifu wao hapo tutakuelewa.usichokifahamu plz mute/uliza ili upate elewa.
 

Maneno ya wanasiasa uchwara huwa siipendi, watu wanayarudia kama kasuku. Elimu watu wanayo ila wanapotoshwa na CCm. Kama nia ya kutunga katiba mpya ingekuwepo kwa viongozi wa CCm kwa kutanguliza TAIFA KWANZA, mchakato ungekuwa ni mwepesi na rahisi sana. Watanzania wengi hawajitambui wanakaa kuwatazama viongozi wa CCm watakavyosema nao wanafuata kama mazuzu vile. Hawa hata ukiwaelimisha vipi hawaelewi kwani mitaala ya elimu ya nchi hii imevurugwa sana na Serikali ya CCm ili wananchi wasijitanbue. Katiba bora itatungwa na watu purely wanaotanguliza maslahi ya Taifa Kwanza hata kama ni wachache kuliko wajinga wengi wanaotanguliza maslahi ya chama.
 

Kwa kifupi, hili ni andiko zuri linaloonyesha weledi wako mkubwa katika kuchambua mambo yanayohusu historia na mustakabali wa nchi yetu na Afrika kwa ujumla. Hongera sana. Nakubaliana na hoja yako kuhusu mchakato wa katiba kuwa hupaswi kuharakishwa kwa matakwa ya wanasiasa wachache, bali unahitaji muda wa kutosha, elimu ya kutosha na ushiriki mpana wa wananchi wa makundi, rika, jinsia, dini zote katika kuandika katiba ya wananchi.

Hata hivyo, napata shida kidogo (au sana?) kuelewa hoja na mtazamo wako hasi kuwa Tanzania (wakati huo Tanganyika) na nchi nyingine za Kiafrika zilifanya makosa kudai na hatimaye kupata uhuru wakati zilikuwa hazijawa tayari kufanya hivyo. Binafsi nafikiri na ninaamini hivyo, kuwa tatizo si wakati gani nchi ilipata uhuru na wakati inapata uhuru ilikuwa imejiandaa vipi au vinginevyo. Tatizo ni sera za uchumi na maendeleo tulizoamua kufuata baada ya uhuru, na hata tunazoendelea nazo sasa zikichagizwa na mabwana wakubwa kama IFM, Benki ya Dunia na nchi wahisani. Sasa nafikiri huu ni mjadala mwingine mpana, na hakuna sababu ya kimsingi na kimantiki kuuunganisha na hili la katiba. Kwa sasa yotosha kusema, hongera sana kwa andiko lako!
 
Narudia tena siyo kweli, mimi naifahamu historia ya Tanganyika.

Labda wadanganye hawa pro-Chadema wenzako.

Nakupa home work kidogo wewe pamoja na wenzako tafuteni historia ya madaktari watano wasomi walijiunga na TANU mwaka 1950.

Achilia mbali kina Chifu Fundikila, Hamza Mwapachu huyu kasoma na Nyerere, Uganda kisha wakasoma Uingereza.
 
nilitegemea ungejibu kwanza swali na ww ndo uulize swali kinyume chake umeuliza swali juu ya swali
Nyie watu wa ajabu sana mnataka niwape darsa huku mnaleta jeuri.
 
Kwa hiyo hata Katiba ikichukuwa miaka 10 au zaidi chini ya CCM hakuna tatizo.
 

Mkuu nitumie fursa hiyo nami kukushukuru kwakutambua mchango wangu,

Mawazo yako ni muhimu na yamejaa hekima kubwa sana,

Asante sana na karibu mkuu wangu!
 

Jf sio kijiwe cha mafumbo,

Wewe kama kuna unachojua mwaga hapa watu wale,

Sio kusingizia eti unawapa watu homework!

Nimekushauri mara nyingi sana Ritz kuwa kama unataka kuwa mchambuzi wa siasa na historia ya siasa hasa hizi za weusi, ni bora ubadilike,

Utajikuta unapishana na mambo muhimu kila palipo na mjadala wa maana,
 
Ni kweli kwakua wapinzani(CDM) ndio ambao walisukuma kuanzisha kwa mchakato huu wa katiba mpya,they take advantage iharakishwe ili 2015 ikiwezekana ccm ing'olewe kwa makali ya katiba mpya!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…