Kosa la mwaka 1960-1975 linajirudia mwaka 2015

Kosa la mwaka 1960-1975 linajirudia mwaka 2015

Mkuu umenena ila serikali hasa kupitia bunge ambalo lina wawakilishi wa ccm wengi limekuwa halina usikivu hata pale panapotakiwa kuweka uchama pembeni na kuweka maslahi ya taifa mbele kazi kubwa ya waTz kufanya sasa ni kuhakikisha ccm imetoka madarakani ili tuwe huru kuandaa katiba itakayotufaa waTz kwa pamoja
 
Yericko,

Kwa faida ya JF tufahamishe PhD ya Dr. Vedasto Kyaruzi alisoma wapi.

Acha sarakasi zako hizo huku ukiwa umejifunga msuli. JF ni darasa huru kama unafahamu historia ya Dr. Kyaruzi we tupia tu wala usianzishe ligi ya mchangani hapa.
 
wewe kweli kobe, umeelewa nini? Kweli unaamini wakati tunapata uhuru wasomi walikuwa wawili tu?

wewe ritz unamaanisha nini unapomwita mwenzio "kobe"tueleze wewe unayejua kwa details otherwise hata wewe.....umbile/shape ya maji huoneka ilivyo kulingana na chombo kilivyo.
 
Acha sarakasi zako hizo huku ukiwa umejifunga msuli. JF ni darasa huru kama unafahamu historia ya Dr. Kyaruzi we tupia tu wala usianzishe ligi ya mchangani hapa.
Wewe vipi! Mimi nimeuliza kujua hii ni forum wewe mbona umechangia hakuna aliyekuuliza.
 
wewe ritz unamaanisha nini unapomwita mwenzio "kobe"tueleze wewe unayejua kwa details otherwise hata wewe.....umbile/shape ya maji huoneka ilivyo kulingana na chombo kilivyo.
Jamaa anaitwa Kobe,
 
Last edited by a moderator:
Yericko,

Kwa faida ya JF tufahamishe PhD ya Dr. Vedasto Kyaruzi alisoma wapi.

nilitegemea ungejibu kwanza swali na ww ndo uulize swali kinyume chake umeuliza swali juu ya swali
 
Mkuu Ritz,

Kuna tatizo kubwa katika uelewa wako, ujengaji wa hoja na ujibuji wa hoja husika,

Kwanza nilikuuliza unitajie Watanganyika waliokuwa na elimu za juu zaidi ya Dr Kyaruzi na Nyerere,

Ukajibu hivi:

Unafamhamu Dr. Mutahangarwa? Unafahamu Dr. Lugaiza? Wapo wengi tuanze na hawa unajua elimu zao?

Nikakuomba utupatie wasifu wa hao madaktari kabla na baada ya uhuru,

Badala ya kujibu swali, Ukaja ukajibu hivi:

"Tuambie Dr Vedasto Kyaruzi alisomea wapi?"

Na hata nilipojarubu kukurudisha uendelee na mtiririko vizuri wa hoja, ukajibu hibu hivi:

Wewe ndiyo umekosa mwelekeo tena umeleta dharau umenipa na orodha ya watu nikawaulize.

Nimekuuliza Dr. Vedasto Kyaruzi kasomea wapi PhD?

Sasa pima mwenyewe mkuu,

Niendelee kujadiliana na wewe au nifanye mengine?
 
Mkuu Ritz,

Kuna tatizo kubwa katika uelewa wako, ujengaji wa hoja na ujibuji wa hoja husika,

Kwanza nilikuuliza unitajie Watanganyika waliokuwa na elimu za juu zaidi ya Dr Kyaruzi na Nyerere,

Ukajibu hivi:

Nikakuomba utupatie wasifu wa hao madaktari kabla na baada ya uhuru,

Badala ya kujibu swali, Ukaja ukajibu hivi:

"Tuambie Dr Vedasto Kyaruzi alisomea wapi?"

Na hata nilipojarubu kukurudisha uendelee na mtiririko vizuri wa hoja, ukajibu hibu hivi:

Sasa pima mwenyewe mkuu,

Niendelee kujadiliana na wewe au nifanye mengine?
Mbona haujaweka orodha ulioniambia nikawaulize kina gombesugu?

Mimi sijadiliani na wewe ninachofanya ni kuwapasha habari wasomaji kuwa siyo kweli kuwa wakati tunapata uhuru wasomi walikuwa wawili.
 
Mkuu Yericko Nyerere ahsante kwa bandiko hili lililoshiba. Umeandika jambo moja la msingi sana kwani watanzania wanaburuzwa tu na wanasiasa wa ccm ili kuwahadaa kuwa wananchi wametengeneza katiba mpya.

Ukweli ni kwamba ni wananchi wachache sana wanaoifahamu katiba ya zamani na hata hii rasimu ya katiba mpya.
Kosa kubwa lililofanywa na ccm na serikali yake ni kuanzisha mchakato wa katiba bila kutoa kwanza elimu kwa watanzania ili wawe na uelewa mpana na sahihi juu ya katiba na waweze kutoa maoni ambayo ni makini sana.
Kama wananchi wangeelimishwa vizuri ingewasaidia sana kuilinda katiba yao huku wakizitambua haki zao na ingekuwa rahisi kuzidai pale itakapotokea wamenyimwa haki hizo.

Kimsingi tunahitaji marekebisho ya sheria ya uchaguzi ili tupate tume huru ya uchaguzi itupitishe salama 2015 na mchakato wa katiba uende taratibu na kwa maridhiano baina ya makundi mbalimbali yenye mitazamo tofauti juu ya katiba mpya.

Kamanda karibu sana,

Tunahitaji fikra mpya na zenye nguvu katika suala hili,

Ninachofurahi maishani mwangu nikuwa huwa naamini siasa za leo hapa Tanzania Chadema ni makutano ya Watanzania wenye fikra huru!
 
Last edited by a moderator:
Mbona haujaweka orodha ulioniambia nikawaulize kina gombesugu?

Mimi sijadiliani na wewe ninachofanya ni kuwapasha habari wasomaji kuwa siyo kweli kuwa wakati tunapata uhuru wasomi walikuwa wawili.

Hapa ndipo unapopotosha,

Soma vizuri nilichoandika mkuu, kama hujui kusoma na kutafsiri maandiko omba ufafanuzi,

Nilichosema nikuwa Tanganyika haikuwa na wasomi "WA NGAZI" ya Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu zaidi ya watu wawili tu yani Daktari Vedasto Kyaruzi na Mwalimu Julius Nyerere,

Hivyo lete kile unachokijua nje ya nilicholeta mkuu,
 
nilitegemea ungejibu kwanza swali na ww ndo uulize swali kinyume chake umeuliza swali juu ya swali
Mkuu kama utakuwa hujamsoma mkuu wetu Ritz hapa jf, basi hilo ndio tatizo lake kuu,

Nimejadiliana nae mahala pengi sana ndani ya jukwaa hili hivyo ndivo alivyo!
 
Hapa ndipo unapopotosha,

Soma vizuri nilichoandika mkuu, kama hujui kusoma na kutafsiri maandiko omba ufafanuzi,

Nilichosema nikuwa Tanganyika haikuwa na wasomi "WA NGAZI" ya Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu zaidi ya watu wawili tu yani Daktari Vedasto Kyaruzi na Mwalimu Julius Nyerere,

Hivyo lete kile unachokijua nje ya nilicholeta mkuu,

Kiukweli huyu ritz simuelewi kabisa na inavyoonesha kuna jambo analijua if not basi kaamua kusumbua akili zetu.sasa basi wewe ritz utuambie orodha ya wasomi waliokuwepo b4 uhuru na wasifu wao hapo tutakuelewa.usichokifahamu plz mute/uliza ili upate elewa.
 
Natofautia na wewe kidogo kamanda,

Kwanza Kenya sio kipimo cha watanzania kupata katiba yao Mpya,

Mleta mada anachopendekeza nikuwa watanzania waendelee kupewa elimu, na anasema minyukano hii tunayoiona iendelee mpaka turidhiane kwa hekima kisha tuandike katiba mpya,

Kuhusu katiba ya kuongoza uchaguzi 2015, kamanda anatushauri kuwa turekebishe mapungufu ya kwenye katiba iliyopo ili ituongoze vema 2015,

Maneno ya wanasiasa uchwara huwa siipendi, watu wanayarudia kama kasuku. Elimu watu wanayo ila wanapotoshwa na CCm. Kama nia ya kutunga katiba mpya ingekuwepo kwa viongozi wa CCm kwa kutanguliza TAIFA KWANZA, mchakato ungekuwa ni mwepesi na rahisi sana. Watanzania wengi hawajitambui wanakaa kuwatazama viongozi wa CCm watakavyosema nao wanafuata kama mazuzu vile. Hawa hata ukiwaelimisha vipi hawaelewi kwani mitaala ya elimu ya nchi hii imevurugwa sana na Serikali ya CCm ili wananchi wasijitanbue. Katiba bora itatungwa na watu purely wanaotanguliza maslahi ya Taifa Kwanza hata kama ni wachache kuliko wajinga wengi wanaotanguliza maslahi ya chama.
 
Mnamo tarehe 9 Desemba 1961, Tanganyika ilipata Uhuru chini ya Waingereza waliokuwa waangalizi wetu tu,

Ni nyakati hizo ambapo mataifa ya Afrika yalikuwa kwenye vuguvugu la kupata uhuru wao kamili yakiongozwa na Nchi ya Gold Coast iliyojinyakulia uhuru kutoka kwa Uingereza mnamo tarehe 6 Machi 1957, na ikawa taifa la kwanza la Afrika Kusini mwa Sahara (Sub-Saharan Africa) kufanya hivyo japokuwa Gold Coast/Ghana haikuweza kutangaza uhuru wake kamili kutoka kwa Uingereza hadi tarehe 1 Julai 1960 ambapo pia nchi ilianza kujulikana kama Jamhuri ya Ghana.

Nchi ya Gold Coast ilianzishwa na Waigereza, "Gold Coast" ni nchi ya Ghana ya leo, Neno Ghana lina maana ya Shujaa Mfalme na lilikuwa ni jina la heshima walilopewa wafalme wa Himaya ya Ghana nyakati za kale za Afrika Magharibi.

Tangu Tanganyika ipate uhuru 09/12/1961 hadi kifo chake chenye utata 1964, ilitumia KATIBA ya chama cha Ukombozi cha TANU iliyoandikwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, pamoja na mahuisho mengi yaliyopita kama yale ya 1962, 1965, 1977, 1992 bado asili ya katiba hii tuliyonayo leo ni ya MKONO wa Julius Nyerere,

Marekebisho makubwa ya Katiba yalikuwa ni mwaka 1977, lakini asili ya KATIBA ile ya Mkono wa Nyerere imeendelea kuishi na kulitendea haki Taifa na wajihi wake!

Nchi ya Gold Coast ilipopata uhuru chini ya Kwame Nkrumah licha ya kubadili jina la nchi na kuitwa Ghana, bado iliendelea kutumia asili ya katiba ya Chama cha The Convention People's Party (CPP)

Labda kwa wale wasiojua niwafahamishe kuwa Katiba ya Tanganyika African National Union (TANU) ilinakiliwa kutoka chama rafiki cha The Convention People's Party (CPP)

Ni mashirikiano mema katika makutano ya fikra za kisiasa kati ya vijana wawili wasomi na imara ambao bara la Afrika halijapata kuwa nao kwa karne hivi sasa, si wengine ni Julius Nyerere na Kwame Nkrumah walipobadilishara fikra na kuzaa matunda ya Afrika na dunia tuyatafunayo sasa,

Nimekuwa na mtazamo hasi kabisa juu ya uhuru wa Afrika kwa mda mrefu sana hasa kwa matukio niyaonayo na niyasikiao toka Afrika,

Miaka ya 1955-1975 ni kipindi ambacho Afrika ilijitoa toka mikononi mwa mkoloni, mimi huwa naamini ni kipindi ambacho Afrika haikuwa na sifa za kuwa tayari kujitawala kwa maana ya kujipatia/kupewa UHURU,

1. Afrika haikuwa na Wasomi wakuongoza nchi

2. Waafrika walikuwa kwenye lindi la kutopea kwenye ujinga, hawakuwa tayari kwa kuupokea uhuru huo,

Mfano Tanganyika ilipata Uhuru ikiwa na wasomi wachache wenye ngazi ya shahada ya Uzamili (Masters) ambae ni Julius Nyerere, na Shahada ya Uzamivu (PHd) ni mmoja tu ambaye ni Dr Vedasto Kyaruzi,

Na hata wale waasisi waliokuwemo kwenye harakati za kupigania Uhuru ndani ya TANU hawakuwa wasomi wa ngazi za juu zaidi ya Julius Nyerere,

Wazee hawa ni Julius Kambarage Nyerere, Ali Sykes, Lameck Makaranga, Gosbert Milinga, Gelmandus Pacha, Joseph Kimalando, Japhet Kirilo, Abubakar Ilanga, Saadan Kandoro, Suleiman Kitwara, Kisunguta Kabara, Tewa Said Tewa, Dosa Aziz, Patrick Kunambi, Joseph Kasela-Bantu, John Rupia, Abdul Wahid Sykes.

Nchi ya Gold Coast/Ghana ilipopata uhuru haikuwa na wasomi wengi wa Shahada, Stashada na Shahada ya Uzamivu na uzamili,

Msomi wa ngazi ya juu alikuwa mmoja tu mwenye shahada ya Uzamili (Master of Science) ndugu Kwame Nkrumah

Japokuwa usomi wa ngazi ya juu kwa watawala sio tiketi ya uwezo wa kutawala katika nchi, Hili huwa naamini ni kosa la Afrika la 1960-1975 kudai Uhuru na kupewa MAPEMA huku Waafrika hawakuwa tayari kujitawala wenyewe,

Hatua hii hunifanya niamini kuwa Afrika haikuwa imepevuka kujitawala kwa ngazi ya karne ile ya 20, huwa naamini kuwa miaka 1975-1985 ndicho kipindi ambacho Afrika ingekuwa kwenye mapito sahihi ya kujitawala, nikipindi ambacho binadamu wa Afrika angekuwa amepevuka,

Sasa ni karne ya 21, kosa lile la Karne ya 20 linajirudia katika muundo uleule kasoro nadharia tu, nalo ni upatikanaji wa Katiba mpya ya Tanzania,

Hali hii ya uhitaji wa katiba mpya kwa Watanzani ni jambo la kupongezwa na kujivunia kwa kila mtanzania, kwakuwa imedhihirika kuwa sasa Taifa limekuwa kifikra, na zaidi idadi ya wasomi katika nchi imeongezeka maradufu,

Lakini jambo la hatari na lisilokubalika nikuwa Taifa limeaminishwa kuwa Katika Mpya itapatikana kabla ya 2015, huu ni ulaghai na wendawazimu wa wazi kabisa,

Katiba ya Watanzania haiwezi kupatikana kwa miaka mitano ama mmoja huu uliosalia, Katika inayohitaji maridhiano, katiba inayopita kwenye misigano ya kitaifa, katiba inayohitaji elimu kwa Watanzania kwanza kamwe haiwezi kupatikana kabla ya 2015, kitakachopatikana kabla ya 2015 kitaitwa katiba ya kisiasa sio katiba ya Watanzania,

Ninachokiamini nikuwa Watanzania tujipe muda, turuhusu fikra na mijadala huru iendelee juu ya upatikanaji wa Katiba mpya, turuhusu majibizano ya hoja ya endelee, turuhusu Watanzania wote wake kwa waume, Wazee kwa vijana wote watoe ya moyoni bila kuogopa mawazo yao,

Katiba bora ya kiraia yenye matakwa halisi ya Wananchi inaweza kuchukua hata miaka 10 mchakato wake mpaka kuipata, hivyo katiba hii ambayo mchakato wake unaendelea SIO lazima isimamie Uchaguzi wa 2015 kama wanasiasa wanavyotusukuma tuamini hivyo,

Nionavyo muhimu katika kipindi hiki nikuwa, Watanzania, wanaharakati na Wanasiasa waendele kusimamia mchakato uendelee lakini upande wa pili wageuzi fikra zao, uanzishwe mchakato wa marekebisho ya Katiba hii iliyopo ili tuingie nayo kwenye uchaguzi 2015.Kinyume na hapo ni kuwalaghai Watanzania kuwa katika itapatika kabla 2015,

Ikumbukwe kuwa Jakaya Kikwete ambae sasa ndiye rais wa Tanzania, katika historia ya siasa zake DUNIANI, hajawahi kuhitaji katiba mpya ya Tanzania wala kuizungumzia tu, hata serikali ya Chama chama Mapinduzi ambacho yeye ndiye Mwenyekiti hakijawahi kuhitaji Katiba Mpya ya Tanzania, na zaidi serikali ya Chama cha Mapinduzi iliyodumu kwa miaka 50 sasa haijawahi kuhitaji katiba Mpya ya Tanzania,

Vyama vya upinzani na Wanaharakati wa Tanzania ndio walioasisi mapambano ya kudai Katiba mpya, tena vikipita katika mapito magumu sana yenye kuhatarisha uhai wao,

Ni baada ya uchaguzi mkuu 2010 ndipo mbinyo wakudai katiba mpya ukiongozwa na chama kikuu cha upinzani nchini huku ccm na wahafidhina wake wakipinga katukatu kuwa Taifa halihitaji Katiba mpya,

Lakini KUFUMBA na KUFUMBUA Jakaya Kikwete alilitangazia Taifa kuwa linaanza mchakato wa Katiba, akitumia neno KUHUISHA katiba.

Tafakari Chukua Hatua, Busara ni mwanzo wa kukaribisha Hekima yenye nguvu za maliza tofauti katika nchi na kupata katiba ya kiraia yenye mkono wa Mtanzania,

Kwa kifupi, hili ni andiko zuri linaloonyesha weledi wako mkubwa katika kuchambua mambo yanayohusu historia na mustakabali wa nchi yetu na Afrika kwa ujumla. Hongera sana. Nakubaliana na hoja yako kuhusu mchakato wa katiba kuwa hupaswi kuharakishwa kwa matakwa ya wanasiasa wachache, bali unahitaji muda wa kutosha, elimu ya kutosha na ushiriki mpana wa wananchi wa makundi, rika, jinsia, dini zote katika kuandika katiba ya wananchi.

Hata hivyo, napata shida kidogo (au sana?) kuelewa hoja na mtazamo wako hasi kuwa Tanzania (wakati huo Tanganyika) na nchi nyingine za Kiafrika zilifanya makosa kudai na hatimaye kupata uhuru wakati zilikuwa hazijawa tayari kufanya hivyo. Binafsi nafikiri na ninaamini hivyo, kuwa tatizo si wakati gani nchi ilipata uhuru na wakati inapata uhuru ilikuwa imejiandaa vipi au vinginevyo. Tatizo ni sera za uchumi na maendeleo tulizoamua kufuata baada ya uhuru, na hata tunazoendelea nazo sasa zikichagizwa na mabwana wakubwa kama IFM, Benki ya Dunia na nchi wahisani. Sasa nafikiri huu ni mjadala mwingine mpana, na hakuna sababu ya kimsingi na kimantiki kuuunganisha na hili la katiba. Kwa sasa yotosha kusema, hongera sana kwa andiko lako!
 
Hapa ndipo unapopotosha,

Soma vizuri nilichoandika mkuu, kama hujui kusoma na kutafsiri maandiko omba ufafanuzi,

Nilichosema nikuwa Tanganyika haikuwa na wasomi "WA NGAZI" ya Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu zaidi ya watu wawili tu yani Daktari Vedasto Kyaruzi na Mwalimu Julius Nyerere,

Hivyo lete kile unachokijua nje ya nilicholeta mkuu,
Narudia tena siyo kweli, mimi naifahamu historia ya Tanganyika.

Labda wadanganye hawa pro-Chadema wenzako.

Nakupa home work kidogo wewe pamoja na wenzako tafuteni historia ya madaktari watano wasomi walijiunga na TANU mwaka 1950.

Achilia mbali kina Chifu Fundikila, Hamza Mwapachu huyu kasoma na Nyerere, Uganda kisha wakasoma Uingereza.
 
nilitegemea ungejibu kwanza swali na ww ndo uulize swali kinyume chake umeuliza swali juu ya swali
Nyie watu wa ajabu sana mnataka niwape darsa huku mnaleta jeuri.
 
Kwa hiyo hata Katiba ikichukuwa miaka 10 au zaidi chini ya CCM hakuna tatizo.
 
Kwa kifupi, hili ni andiko zuri linaloonyesha weledi wako mkubwa katika kuchambua mambo yanayohusu historia na mustakabali wa nchi yetu na Afrika kwa ujumla. Hongera sana. Nakubaliana na hoja yako kuhusu mchakato wa katiba kuwa hupaswi kuharakishwa kwa matakwa ya wanasiasa wachache, bali unahitaji muda wa kutosha, elimu ya kutosha na ushiriki mpana wa wananchi wa makundi, rika, jinsia, dini zote katika kuandika katiba ya wananchi.

Hata hivyo, napata shida kidogo (au sana?) kuelewa hoja na mtazamo wako hasi kuwa Tanzania (wakati huo Tanganyika) na nchi nyingine za Kiafrika zilifanya makosa kudai na hatimaye kupata uhuru wakati zilikuwa hazijawa tayari kufanya hivyo. Binafsi nafikiri na ninaamini hivyo, kuwa tatizo si wakati gani nchi ilipata uhuru na wakati inapata uhuru ilikuwa imejiandaa vipi au vinginevyo. Tatizo ni sera za uchumi na maendeleo tulizoamua kufuata baada ya uhuru, na hata tunazoendelea nazo sasa zikichagizwa na mabwana wakubwa kama IFM, Benki ya Dunia na nchi wahisani. Sasa nafikiri huu ni mjadala mwingine mpana, na hakuna sababu ya kimsingi na kimantiki kuuunganisha na hili la katiba. Kwa sasa yotosha kusema, hongera sana kwa andiko lako!

Mkuu nitumie fursa hiyo nami kukushukuru kwakutambua mchango wangu,

Mawazo yako ni muhimu na yamejaa hekima kubwa sana,

Asante sana na karibu mkuu wangu!
 
Narudia tena siyo kweli, mimi naifahamu historia ya Tanganyika.

Labda wadanganye hawa pro-Chadema wenzako.

Nakupa home work kidogo wewe pamoja na wenzako tafuteni historia ya madaktari watano wasomi walijiunga na TANU mwaka 1950.

Achilia mbali kina Chifu Fundikila, Hamza Mwapachu huyu kasoma na Nyerere, Uganda kisha wakasoma Uingereza.

Jf sio kijiwe cha mafumbo,

Wewe kama kuna unachojua mwaga hapa watu wale,

Sio kusingizia eti unawapa watu homework!

Nimekushauri mara nyingi sana Ritz kuwa kama unataka kuwa mchambuzi wa siasa na historia ya siasa hasa hizi za weusi, ni bora ubadilike,

Utajikuta unapishana na mambo muhimu kila palipo na mjadala wa maana,
 
Ni kweli kwakua wapinzani(CDM) ndio ambao walisukuma kuanzisha kwa mchakato huu wa katiba mpya,they take advantage iharakishwe ili 2015 ikiwezekana ccm ing'olewe kwa makali ya katiba mpya!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom