Kosa la mwaka 1960-1975 linajirudia mwaka 2015

Kwa hiyo hata Katiba ikichukuwa miaka 10 au zaidi chini ya CCM hakuna tatizo.

Acha kupotosha nilichosema Ritz,

Mbona unakuwa mzabizabina ndugu yangu?

Nimesema kuwa mchakato hata uchukue miaka kumi mbele, lakini kwa sasa mda uliosalia kwa uchaguzi 2015, tufanye marekebisho ya katiba iliyopo ili ituongoze kwenye uchaguzi mkuu 2015,

Chama chochote kitakachokuwa madarakani kitakuwa na wajibu wa kuendeleza mchakato uliopo,

Sasa spinning unazofanya ni za kitoto ndugu,
 
Basi kama ndiyo hivyo basi maoni yako yatafanyiwa kazi na serikali ya CCM.

Nakumbuka Mwalimu Nyerere alishawahi kusema hii katiba inamfanya rais kuwa dikteta kama akiamua kuitumia kama ilivyo sasa wewe unataka endelee kutumika hata miaka 10 mbele na zaidi.

Yericko Nyerere, mbona unakuwa mzabinazabina, unaweza kutupa ushahidi kama hii Katiba imeandikwa kwa mikono ya Nyerere kama unavyodai.

Kwanza Mwalimu Nyerere hakuwa mwanasheria sijui hiyo Katiba aliiandika vipi.
 
Last edited by a moderator:
Kuna mambo ya msingi yanayohusu uchaguzi kama daftari la wapiga kura, mgombea binafsi, tume huru ya uchaguzi yanaweza kufanyiwa mabadiliko ya msingi kabla ya 2015 election, lakini mambo mengine yaendelee kujadiliwa kabla katiba mpya haijaandikwa. Kwamba kenya walichukua muda mfupi, nasikitika kusema umekosea sana kihistoria. Unafahamu kitu kinaitwa bomas au Prof. Yash Ghai Draft ya 2000-2004 katika historia ya mchakato wa katiba ya Kenya? Katiba ya Kenya imechukua zaidi ya muongo mmoja kupatikana tena kwa gharama kubwa ikiwamo maisha ya watu. Kwa nini mchakato uchukue muda mrefu? Hii itawasaidia walevi wa madaraka kama akina Chikawe, Wasira, Lukuvi, Werema, Ndugai, Sophia Simba na wengine ambao ni wazito kuelewa kwa muda mfupi nini mana ya katiba ya wananchi waweze kuelewa japo kiasi. Kwani wao hawaelewi kitu kingine zaidi ya CCM duniani hapa.
 

Nitaendelea kukukosoa mda wote,

Hakuna niliposema katika hii tuliyonayo iendelee kutuongoza kama ilivyo,

Nilichosema nikuwa ifanyiwe marekebisho kwenye maeneo muhimu ili ituongoze kwenye uchaguzi 2015,

Kuhusu katiba ya TANU kuandikwa na Julius Nyerere hilo sihitaji hata kukufundisha upya, kwani nilishakufundisha sana huko nyuma,

Na kwamba katiba ya Tanganyika ilihuishwa ile ya TANU hilo nalo elewa hivyo mkuu,
 
Mwenzetu huyo huenda anakipaji maalumu,

Akiona sentensi moja tu basi huelewa mada nzima,

Sio kosa lake ndio kizazi cha bongo movies

exactly! Ndio maana huwa najiapiza kwamba, ni bora niitwe baba dicteta au mkoloni lakini kamwe sitaacha my daughter awe addicted na Bongo Movies! For the benefit of her thinking capacity!
 

Naaaam naaaam naaam

Mkuu umetoa elimu pana sana hasa kwa wahafidhina wa vyama badala ya taifa
 
Unafamhamu Dr. Mutahangarwa? Unafahamu Dr. Lugaiza? Wapo wengi tuanze na hawa unajua elimu zao?

duh nimeshtukaje!!,mkuu nilivyona maneno Dr. nikadhani yataishia na ali,muhamed...aise kumbe watu wa tz bara including nyerere ndo walikuwa wasomi wa mwanzo tz.?!
 

Mimi naamini tunaweza kufanya marekebisho madogo kwenye hii katiba tuliyonayo natukafanya uchaguzi ulio haki na huru,ili tupate katiba bora ya wananchi tunahitaji muda.
 
Yericko Nyerere,

Ukileta babandiko yako lazima huwe tayari kuyatetea kwa hoja siyo kwa viroja.
Hakuna niliposema katika hii tuliyonayo iendelee kutuongoza kama ilivyo,

Nilichosema nikuwa ifanyiwe marekebisho kwenye maeneo muhimu ili ituongoze kwenye uchaguzi 2015,
Hebu jisome mwenywe hapa chini kutoka kwenye bandiko lako.
Sijui ulikuwa na maana gani hapo.
Kwa faida ya Wanaukumbi ungetupa ushahidi siyo kuja na maneno matupu hapo kwenye bold siyo kweli.
 
Last edited by a moderator:
duh nimeshtukaje!!,mkuu nilivyona maneno Dr. nikadhani yataishia na ali,muhamed...aise kumbe watu wa tz bara including nyerere ndo walikuwa wasomi wa mwanzo tz.?!
du!!!! hebu jipongeze na huu mpini kiduchu kisha tuendelee na mjadala.
Nimetulia tuli nakula zangu Faluda, teh teh teh...

Cc: kahtaan, THE BIG SHOW, Tayeb, gombesugu,
 
Last edited by a moderator:
exactly! Ndio maana huwa najiapiza kwamba, ni bora niitwe baba dicteta au mkoloni lakini kamwe sitaacha my daughter awe addicted na Bongo Movies! For the benefit of her thinking capacity!

Daaah nimecheka sana mkuu!

Hahaha aisee
 
du!!!! hebu jipongeze na huu mpini kiduchu kisha tuendelee na mjadala.

Nimetulia tuli nakula zangu Faluda, teh teh teh...

Cc: kahtaan, THE BIG SHOW, Tayeb, gombesugu,

Kuna uwezekano mkubwa ama hujui kusoma, ama hujui mantiki ya mada iliyopo,

Habari ya Mwapachu na elimu yake inamalizikia hapa chini,

Thus in 1947 he quit medical practice and joined the University College of South Wales at Cardiff to read a Diploma in Social Work.

Sasa nieleze, Mwapachu alikuwa na Masters?

Alikuwa na PhD?

Nilichoona na ninachofahamu amefariki akiwa na Diploma in Social Work.

Kama kuna habari zingine mpya juu yake hebu zilete hapa wanajamvi wakusome
 
Last edited by a moderator:
Yericko Nyerere,

Endelea kuwadanganya jamaa zako najua hauwezi kutoa majibu ninachofanya ni kuwasaidia wana JF wasimeze pumba kama hizi hapa.
Mfano Tanganyika ilipata Uhuru ikiwa na wasomi wachache wenye ngazi ya shahada ya Uzamili (Masters) ambae ni Julius Nyerere, na Shahada ya Uzamivu (PHd) ni mmoja tu ambaye ni Dr Vedasto Kyaruzi,
Hebu msome huyu hapa chini.
Taratibu takuwa nakupa darsa....
 
Last edited by a moderator:

Hili tayari nimeshalitolea ufafanuzi ndani ya makala hiyo hiyo, usiwe mvivu mkuu tulia soma,
 
Last edited by a moderator:
Yericko Nyerere,

Endelea kuwadanganya jamaa zako najua hauwezi kutoa majibu ninachofanya ni kuwasaidia wana JF wasimeze pumba kama hizi hapa.

Hebu msome huyu hapa chini.

Taratibu takuwa nakupa darsa....

Mkuu unapoteza mda tu,

Fundikila amefariki akiwa na Degree toka Makerere tu, hakuwa na Masters wala PHD,
 
Last edited by a moderator:
Sikubaliana na wewe kwenye mitazamo inayoshibishwa na propaganda na fikra mgando za ki magharibi. Naendelea kuamini bila ukoloni labda afrika tungekuwa mbali kuliko hap watu wa magharibi na ushahidi upo
1. Mtu wa Kwanza duniani imethibitika anatoka Afrika -Tanganyika
2. Chuo kikuu cha kwanza cha hisabati na Physics kipo Afrika - Egypt
3. Kiwanda cha kwanza cha ngupo (barking cloth) kilikuwa afrika - Nigeria
4. Kiwanda cha kwanza cha chumvi kilikuwa Afrika -Tanganyika

Baada ya explorers, traders na missionaries kuja walitulazimisha kufuata mitazamo na fikra zao, wakatufanya tuone fahari zetu kuwa ujinga na tumechelewa, wakaita AFRIKA the DARK CONTINENT ili hali linavitu vingi vikidhibitsha uongo na ujinga wao.

Kuhusu elimu, naamini Afrika ilikuwa na elimu yake nzuri na bora kwa mazingira yake ila elimu ya magharibi imetufanya tuone elimu yetu ni ya kijinga, fikiria zamani wazee walifundishwa kuishi kutokana na mazingira yao wenyewe leo GEOGRAPHY inafundishwa ya ULAYA ili hali ya Mkuranga kwetu wenyewe hawafundishwi, leo HISTORIA na MASHUJAA WOTE ni wazungu ili hali babu zetu wengi tu wana dhihakiwa.

Nakubaliana mwishoni namna mchakato wa katiba mpya ulivyobakwa, namna wanasiasa wanavyotaka kufanikisha kwa maslahi yao wenyewe


 
Nimejifunza mambo mengi sana kwenye uzi huu,

Kumbe mada nzuri, nzito na za kizalendo, wale pro ccm akina Hamy-D, MwanaDiwani, Chris Lukosi, Mwigulu Nchemba, Nape Nauye na wengine huwa hawagusi kabisa,

Wao mahala pau ni uzi za vurugu na uchochezi tu,

Heko sana kamanda Yeriko,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…