Kosa la mwaka 1960-1975 linajirudia mwaka 2015

Kosa la mwaka 1960-1975 linajirudia mwaka 2015

kikiubwa hapa naomba tujadili juu ya katiba mpya ninacho kiona mimi CCM CDM CUF na NCCR hawana mda mda na katiba ya kiraia wanachotaka wenyewe ni katiba ya kisiasa zaidi na ndoo maana ukingalia kwa kiasi kikubwa wanadeal na mambo ya muungano ,tume huru ya uchaguzi na mambo mengine ambayo wanaona yatawasaidia kupata madaraka ya kisiasa
 
Sikubaliana na wewe kwenye mitazamo inayoshibishwa na propaganda na fikra mgando za ki magharibi. Naendelea kuamini bila ukoloni labda afrika tungekuwa mbali kuliko hap watu wa magharibi na ushahidi upo
1. Mtu wa Kwanza duniani imethibitika anatoka Afrika -Tanganyika
2. Chuo kikuu cha kwanza cha hisabati na Physics kipo Afrika - Egypt
3. Kiwanda cha kwanza cha ngupo (barking cloth) kilikuwa afrika - Nigeria
4. Kiwanda cha kwanza cha chumvi kilikuwa Afrika -Tanganyika

Baada ya explorers, traders na missionaries kuja walitulazimisha kufuata mitazamo na fikra zao, wakatufanya tuone fahari zetu kuwa ujinga na tumechelewa, wakaita AFRIKA the DARK CONTINENT ili hali linavitu vingi vikidhibitsha uongo na ujinga wao.

Kuhusu elimu, naamini Afrika ilikuwa na elimu yake nzuri na bora kwa mazingira yake ila elimu ya magharibi imetufanya tuone elimu yetu ni ya kijinga, fikiria zamani wazee walifundishwa kuishi kutokana na mazingira yao wenyewe leo GEOGRAPHY inafundishwa ya ULAYA ili hali ya Mkuranga kwetu wenyewe hawafundishwi, leo HISTORIA na MASHUJAA WOTE ni wazungu ili hali babu zetu wengi tu wana dhihakiwa.

Nakubaliana mwishoni namna mchakato wa katiba mpya ulivyobakwa, namna wanasiasa wanavyotaka kufanikisha kwa maslahi yao wenyewe

Mkuu kwanza karibu kwenye mjadala huru, na nisamehe kama nimekukwaza popote katika andiko hili,

Pamoja na maelezo yako mazuri na yanayoturejesha kwenye historia kabla ya kristu kuzaliwa, yani enzi za dola ya farao,

Naomba nikuulize swali moja tu ili litufungue kwa mjadala,

Je ni sababu ipi ilipelekea Tanganyika tuwekwe chini ya Udhamini wa UNO-UK baada ya kupewa UHURU wetu baada ya Mjerumani kushindwa vita kuu ya pili ya dunia?
 
kikiubwa hapa naomba tujadili juu ya katiba mpya ninacho kiona mimi CCM CDM CUF na NCCR hawana mda mda na katiba ya kiraia wanachotaka wenyewe ni katiba ya kisiasa zaidi na ndoo maana ukingalia kwa kiasi kikubwa wanadeal na mambo ya muungano ,tume huru ya uchaguzi na mambo mengine ambayo wanaona yatawasaidia kupata madaraka ya kisiasa

Karibu mkuu wangu,

Ndicho tunachokifanya katika mjadala huu mkuu wangu,

Tunahitaji mawazo yako juu ya mada hii
 
Dr. Kyaruzi hakuwa na Masters wala PhD, endelea kuwadanganya pro-Chadema wenzako.
Wenye akili timama katika mijadala ya hoja,
Huwa hatukanushi tu kwa maneno mawili bali ufafanuzi na ukweli wake,
 
Dr. Kyaruzi hakuwa na Masters wala PhD, endelea kuwadanganya pro-Chadema wenzako.

Mkuu Ritz nakusoma kwa miwani ya 3D huku napata haluwa nimeamini jamaa anaugonjwa wa "Amnesia" na kumkosoa kote bado anajitoa ufahamu lakini tumetoka nae mbali huyu maharage ya Mbeya maji mara moja mlainiiii!
 
Wacha kulialia ufanunuzi wote uliopewa hutaki kukubali,
Yericko kama hujashiba kwenye sahani huwezishiba kwenye kijiko.

Karibu bwana Boko Haram,

Hakuna ufafanuzi alioutoa Ritz,

Amemleta Mwapachu akimaanisha alikuwa msomi wa ngazi ya PHd, lakini nikamweleza kuwa huyo alikuwa na Diploma tu,

Akamleta Fundikila kama msomi wa PHd, lakini nikamwambia kuwa Fundikila alikuwa na Degree tu,

Sasa Ritz kapotea, kila akisaka gogu na wikipidia nyaraka za kutetea hoja yake hapati kitu,

Sasa msaidie wewe, jibu hoja ama uliza chochote ujibiwe mkuu,

Nipo kwaajili yenu msiojua kitu,
 
Na hata wale waasisi waliokuwemo kwenye harakati za kupigania Uhuru ndani ya TANU hawakuwa wasomi wa ngazi za juu zaidi ya Julius Nyerere,

Wazee hawa ni Julius Kambarage Nyerere, Ali Sykes, Lameck Makaranga, Gosbert Milinga, Gelmandus Pacha, Joseph Kimalando, Japhet Kirilo, Abubakar Ilanga, Saadan Kandoro, Suleiman Kitwara, Kisunguta Kabara, Tewa Said Tewa, Dosa Aziz, Patrick Kunambi, Joseph Kasela-Bantu, John Rupia, Abdul Wahid Sykes.

Mtoto wa Nyerere wa kulazimisha, naomba nikuulize, kabla ya mengine.

Jee, ndio hao tu? na unaweza kutueleza hao "waasisi waliokuwemo kwenye harakati za kupigania Uhuru" uliowataja, kila mmoja wao ali"pigania" kivipi? "harakati za kupigania Uhuru"?
 
Mkuu Ritz nakusoma kwa miwani ya 3D huku napata haluwa nimeamini jamaa anaugonjwa wa "Amnesia" na kumkosoa kote bado anajitoa ufahamu lakini tumetoka nae mbali huyu maharage ya Mbeya maji mara moja mlainiiii!

Twende taratibu na kwa hekima mkuu,

Umeelewa nini katika andiko hilo?

Hujaelewa nini katika bandiko hili?

Uliza swali ama toa maoni
 
Ni kweli ccm hawakutaka katba mpya hapo kabla ila walipoona upepo unavuma kwa mwelekeo tofaut na wao wakaamua kujiunga na bahat mbaya sio kwa matakwa ya wengi

Hongera kwa CDM kwan ndo waasis wa katba mpya na wamefanya kaz ngumu xana ya kuwafumaua macho watz mpaka
Naunga mkono hoja
 
Mtoto wa Nyerere wa kulazimisha, naomba nikuulize, kabla ya mengine.

Jee, ndio hao tu? na unaweza kutueleza hao "waasisi waliokuwemo kwenye harakati za kupigania Uhuru" uliowataja, kila mmoja wao ali"pigania" kivipi? "harakati za kupigania Uhuru"?

Mkuu kwanza acha dharau na dhihaka,

Mimi sio mtoto wa Nyerere wa kulazimisha,

Mimi ni mtoto HALALI wa Yohanes Msambila Nyerere,

Kwenye swali lako naomba nisikujibu kwakifupi,

Nakujibu kwa kirefu,

Jibu lako linapatikana kwenye uzi huu hapa chini;

http://bit.ly/13eNz6k
 
Ni kweli ccm hawakutaka katba mpya hapo kabla ila walipoona upepo unavuma kwa mwelekeo tofaut na wao wakaamua kujiunga na bahat mbaya sio kwa matakwa ya wengi

Hongera kwa CDM kwan ndo waasis wa katba mpya na wamefanya kaz ngumu xana ya kuwafumaua macho watz mpaka
Naunga mkono hoja

Watanzania tusiruhusu siasa zituburuze katika kupata katiba yetu,

Vyama vitapita, lakini Tanzania itadumu daima,
 
Link bomu.

Msambile toka lini akawa Nyerere na huyo ni Mhehe?

Hehee maajabu,

Kama ndio fikra uliyonayo, basi leo Wamanyema-Wakongo wasingekuwepo Tanganyika, Wangoni-Wazulu wasingekuwepo Tanganyika, Wahehe-Wakushi wasingekuwepo Tanzania, Watusi-Wakushi wasingekuwepo Rwanda

Ndugu yangu funguka japo kidogo,

Hii mipaka katika dunia imewekwa na mabeberu tu,

Hiyo link niliyokupa ina majibu yote mtawalia
 
Unakumbuka uliposema Nyerere ni baba'ko mzazzi akaja mtoto wa kwanza wa Nyerere akakushikia bango kuanzia Msasani mpaka Butiama? au ni mfupi wa kumbukumbu tukushushie zile post?

Hivi jina la TANU nani alilibuni?
 
Unakumbuka uliposema Nyerere ni baba'ko mzazzi akja mtoto wa kwanza wa Nyerere akakushikia bango kuanzia Msasani mpaka Butiama? au ni mfupi wa kumbukumbu tukushushie zile post?

Hivi jina la TANU nani alilibuni?

Nitakujibu maswali yenye maana tu, hivyo vingine viroja mimi sina mda navyo,

Jina la TANU lilibuniwa na waasisi wa TANU wakiongozwa na Abdul Sykes
 
du!!!! hebu jipongeze na huu mpini kiduchu kisha tuendelee na mjadala.

Nimetulia tuli nakula zangu Faluda, teh teh teh...

Cc: kahtaan, THE BIG SHOW, Tayeb, gombesugu,

Mkuu Ritz, naona unaendelea kumpa darsa la ukweli huyo ndugu tehe tehe tehe tehe!

Tuko pamoja mkuu, mimi naendelea kukusoma hapa!
 
Last edited by a moderator:
Unakumbuka uliposema Nyerere ni baba'ko mzazzi akja mtoto wa kwanza wa Nyerere akakushikia bango kuanzia Msasani mpaka Butiama? au ni mfupi wa kumbukumbu tukushushie zile post?

Hivi jina la TANU nani alilibuni?
FaizaFoxy, unachokisema ni sahihi kabisa!

Nakumbuka huyu Ndugu Yericko Nyerere amewahi andika mahala hicho unachokisema!

Kuna somebody Nyerere alikuja hapa na kumtoa nishai tehe tehe tehe!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ritz, naona unaendelea kumpa darsa la ukweli huyo ndugu tehe tehe tehe tehe!

Tuko pamoja mkuu, mimi naendelea kukusoma hapa!

Unamaoni gani juu ya makala iliyopo?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom