Kosa langu ni kuamua kuishi maisha yangu

Kosa langu ni kuamua kuishi maisha yangu

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Kuna watu unaweza kuwa karibu nao lakini wasitambue umuhimu wako. Wanaweza kuwa ndugu, jamaa au marafiki. Na unapoamua kuachana nao na kuishi maisha yako,wanakuona kama umewatenga.

Binafsi nimewahi kupitia changamoto za kukataliwa na watu wangu wa karibu. Kila nilipojaribu kuwa mwema kwao, waliniona mbaya. Sasa nimeamua kuishi maisha yangu bila kutegemea sana hisia zao juu yangu.
Cha ajabu leo hii naonekana kama vile nimewatenga ilihali wao ndio walianza kuniumiza kwa maneno na matendo yako.

Najua wapo wengi kama mimi na wengine waliamua kuhama hadi nchi yao na pengine kubadili uraia wao. Ama kweli dunia ina mengi!
 
Aise kama ni ndugu ww endelea kuishi maisha yako hata wakikusema vibaya puuzia chief Tafta circle ya marafiki wa kweli wakusaidiana kwenye hali zote ...usitegemee sana misada kutoka kwa ndugu
Ishi vzuri ukimpendeza Jehova nasio kuishi dunia inavyotaka...

Punguza mazoea sana na hao ndugu kwenye matatizo ww fika wape poleee ondokaaa usikae sana karibu nao,na fanya namna yoyote ile wasikuelewe mishe zako yani kua mtu wa kutoeleweka na usiwe muongeaji sanaa unapokua nao
 
Principle ya kwanza ni ujifikirie wewe mwenyewe kwanza, ukiona wewe upo sehemu salama unaweza sasa kufikiria wengine lakini kamwe usijitoe ukapata shida ukashinda njaa kwa ajili ya mtu mwingine tofauti na mzazi wako, sababu ikifika zamu yao kufanya kwa ajili yako wengi hawawezi
 
Aise kama ni ndugu ww endelea kuishi maisha yako hata wakikusema vibaya puuzia chief
Tafta circle ya marafiki wa kweli wakusaidiana kwenye hali zote ...usitegemee sana misada kutoka kwa ndugu
Ishi vzuri ukimpendeza Jehova nasio kuishi dunia inavyotaka...
Punguza mazoea sana na hao ndugu kwenye matatizo ww fika wape poleee ondokaaa usikae sana karibu nao,na fanya namna yoyote ile wasikuelewe mishe zako yani kua mtu wa kutoeleweka na usiwe muongeaji sanaa unapokua nao

Ushauri mzuri
 
Ndo binadamu walivyo,usigeuke nyuma...wengine tulitoswa na ndugu tukiwa wadogo kabisa!
Leo mtu umepambana una maisha yako wanaanza kujifanya wanajali, kwangu hata kwa maigizo tu siwezi kuwa karibu na watu wa aina hiyo!
 
Nilidhania nipo pekee yangu,kumbe tupo wengi tu....mimi rafiki yangu ni jf na tv, tofauti na hapo napanda baiskeli kwenda kijiji cha tatu huko wasiponifahamu naenda kucheza michezo ya kila aina(Usisahau kutongoza 😋😋) ili mradi nifurahi.

Nikirudi maskani ni ndani na kazini tu
 
When u begin to mind your damn business huwa wanaanza kuchonga.

Mfano Mimi pia naonekanaga nimejitenga sana kwa baadhi ya ndugu.

Sifanyi hivyo kwa kupenda ila Kuna watu pengine wamenifosi niishi hivyo.

Mfano Kuna mmoja nilikuwa natembelea kwake wakati nikipata likizo kazini kumsababahi akawa analipa Hela Kila nikienda kama vile ananipa msaada Wala mimi sikumuomba nikawa najisikia vibaya najiona kama naenda kuomba msaada na huu utu uzima .

Nikaamua nikate mguu mazima Leo naonekana nimewasusa wako wengi sana.

Siku hizi naokana kwenye events tu msiba,ugonjwa (nikishirikishwa), sherehe(nikishirikishwa) otherwise huwa sitokei kokote kule.

Niko bize na maisha yangu na mbaya zaidi sinaga mambo ya kujikomba
 
Nilidhania nipo pekee yangu,kumbe tupo wengi tu....mimi rafiki yangu ni jf na tv, tofauti na hapo napanda baiskeli kwenda kijiji cha tatu huko wasiponifahamu naenda kucheza michezo ya kila aina(Usisahau kutongoza [emoji39][emoji39]) ili mradi nifurahi.

Nikirudi maskani ni ndani na kazini tu
Umekata shauri. Yan Haya mambo ya wanga hapa Bongo sijui kwa kwel. Kuna mtaa Uko Dar. Nahis wanga pale ndio Mlimani city kwao. Yan ni mwiko watu kuendelea ule mtaa. Vijana walisoma wakaishia ulevi wa pombe za wazee. Ni shida.

Kifup ukija kwa individuals unakuta wanawangiwa ukienda national level unakuta mafisadi na Uzembe wa makusudi kuzuia Maendeleo ya uhakika.
 
Watabadilika tu ata kama itachukua muda mrefu kuzoea
 
Back
Top Bottom