Kosa langu ni kuamua kuishi maisha yangu

Ndo binadamu walivyo,usigeuke nyuma...wengine tulitoswa na ndugu tukiwa wadogo kabisa!
Leo mtu umepambana una maisha yako wanaanza kujifanya wanajali, kwangu hata kwa maigizo tu siwezi kuwa karibu na watu wa aina hiyo!
Niliamua nitegeneze ndugu zangu ambao ni wanangu tu, ndugu wa kiafrica ni mtihani ukiwazidi mari ni kosa, ukisoma kuwazidi kosa ukioa mke mwenye maendeleo na mzuri kosa, ukisomesha wanao shule nzuri kosa ukiwa fukara kosa, dawa ni kuwa ignore na ku move on with your private life, tena kama unauwezo hama kabisa kijiji au mji ukae mbali nao.
 
Ndugu yangu mimi muhanga wa hilo nimeamua niishi stahili yako .nimeona faida yake kuna wanadamu ata ufanye wema sawa na bure cha msingi ni kuishi maisha yako na mungu wako
 
Ukiwajua binadam hawaumizi vichwaa
 
Mi marafili zangu wengi ni mtaani na napenda kuwa online kweny social media zote group za marafiki zangu ni o level tu basi maana wengi tulikaa mtaa mmoja ila kuanzia advance ,chuo mpaka kazini sina mzuka nao watu wake...

sikufichi nilijaribu kumingle na vijana na wengine watu wazima kwangu wanakaribia miaka 50 ila eti story zao ni ngono tu na kingine kwa maeneo ya kazini sitaki kujua lifestyle ya mtu sijui anaishi wapi...Kawaida na yote ila sijawahi kuingia kweny kesi wala kugombana na mtu .

Watu wale tunaoenda msikitini basi ndo inatokea tunaongoza mda wa kazi maana hata watu wakubwa wapo..

Shughuli za kijamii kama msiba naweza hata kuosha vyombo japo ni mwanaume ili mradi nishiriki na kusindiza jeneza ila harusi hata iwe ya ndugu au rafiki yangu ntatoa mchango ila kuhudhuria naona balaa.


Binafsi naona kuna faida kubwa sana na furaha yangu nimewekeza kweny familia yangu na jamaa wa kitaa tena hata wao wapo bussy ....Mimi ratiba zangu kuchek mpira hata movie sio sana
 
Subiri uugue uone hao kijiji cha tatu kama watachukua bicycle kuja kukuuguza au kukusaidia!
Kiufupi ishi na ndugu zako kiupendo pamoja na makandokando yao usiwatenge hata wakikutenga. Wajenge, waunge na wasaidie pia kuna siku watajirekebisha labda kama ni wachawi.
 
Ndo binadamu walivyo,usigeuke nyuma...wengine tulitoswa na ndugu tukiwa wadogo kabisa!
Leo mtu umepambana una maisha yako wanaanza kujifanya wanajali, kwangu hata kwa maigizo tu siwezi kuwa karibu na watu wa aina hiyo!
Usiseme binadamu walivyo sema tulivyo na we mojawapo kama binadamu mkuuu
 
Sawa elon musk 😁😁
 
Ndo binadamu walivyo,usigeuke nyuma...wengine tulitoswa na ndugu tukiwa wadogo kabisa!
Leo mtu umepambana una maisha yako wanaanza kujifanya wanajali, kwangu hata kwa maigizo tu siwezi kuwa karibu na watu wa aina hiyo!
I see!
Na wengi hawajui kama wakati wa utoto ndio wakati sahihi wa kupanda kile ulichokusudia. Kama ni upendo au chuki, haiwezi sahaulika hadi ukubwani
 
sijatenga ndugu,ukiugua nakuja kujulia hali,ukifiwa nahani msiba kwa kifupi kwenye masuala ya msingi nipo sana ila siyo tujuane sana tutaaribiana cv
 
Na usiwe muongeaji sana unapokuwa nao, nimeipenda hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…