Life2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,387
- 4,880
Rest in Heaven ndugu zetu,Damu zenu zikalie masikioni mwa Mwenyezi Mungu.
Kama taifa tulishakosea kitambo sana, kuna mambo yalianza Kama utani ila kwa sasa ndo tunavuna matendo yake na litakuchukua muda kwisha mpaka waje viongozi wenye uchungu na nchi hii.
Kitendo cha kuanza kuwapa watu cheo cha ubunge Kama zawadi ni kosa kubwa sana lililofanyika.
Wabunge wa sasa hawapo na nchi bali wapo na watawala waliowapa hivyo vyeo Kama zawadi kanuni ni wewe sifia tu hata maovu mwisho wake utapewa cheo Kama cha Ubunge Kama zawadi.
Leo wabunge hawapo kusimamia mikataba yenye tija kwa taifa bali wapo kusaini mikataba ya kitu mtawala anataka.
Asilimia kubwa ya wabunge wa sasa sio chaguo la wananchi bali ni machaguo ya mtawala, wananchi hawana Chao.
Wewe piga kura yako kwa umtakaye ila mwisho wa siku amtakaye mtawala ndo atakua mbunge wako hata kwa viboko.
Aliyekua na mradi wa kununua wabunge wa wapinzani kwa imani yangu siruhusiwi kulaani hata kidogo zaidi ya kusema Mungu amsamehe na ajue hakika anatutesa Watanganyika mpaka leo.
Siku wakitambua wana deni kubwa sana na watanganyika na kufanya kazi zao kwa weledi ndipo siku tutatoka kwenye huu mkwamo.
Leo ukionekana upo upande wa watanganyika unasimama nao kuzungumza haki na ukweli tambua hutorudi tena bungeni.
Mungu endelea kututetea watanzania usikae kimya dhidi ya watesi wetu hawa wanaotaka kuturarua kwa makucha yao makali Kama Simba.