Kosa wanalofanya watu wengi ni kuitupa fimbo iliyowasaidia walipokuwa Vipofu.

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
KOSA WANALOFANYA WATU WENGI NI KUITUPA FIMBO ILIYOWASAIDIA WALIPOKUWA VIPOFU.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Unakuta kijana kasoma kimazabe kutokea shule za kayumba, mwalimu mmoja, hakuna maabara wala maktaba. Lakini kijana akakaza akafaulu na hatimaye alifika chuo kikuu na kuhitimu shahada yake.

Unakuta kijana mwingine yeye hakufanikiwa kusoma kwa maana ya kufika chuo kikuu. Lakini alipofeli kidato cha nne akajitathmini na kuona tayari amepuyanga. Hana njia nyingine zaidi ya kupambana kitaa Kwa jasho na damu.
Amepiga vibarua vya hapa na pale hatimaye akaweza kujitegemea angalau kwa kupanga chumba kimoja au hata viwili. Anavitu vidogo vya ndani vinavyomtosha kuendesha maisha yake bila kumtegemea MTU mwingine.

Kosa kubwa wanalolifanya vijana wengu hawa ni kutupa fimbo waliyoitumia wakati walipokuwa vipofu.
Unajua vipofu wengi siku wanapopata bahati ya kuona Jambo la Kwanza wengi wao hutupa gongo au fimbo lililokuwa linawasaidia kutembea. Hilo ni kosa kubwa.

Taikon Master ninakushauri kama kijana usiwe kama vipofu wengi ambao pindi wakiona hutupa fimbo zao zilizowaongoza.

Nitakupa mifano ya Fimbo au gongo ambalo huwaongoza vijana wengi walipokuwa vipofu;

1. Nidhamu na kujituma.
Hii ni fimbo ambayo vijana wengi vipofu huwa nayo kipindi wakiwa down, vipofu wasio na hili wala lile.
Embu fikiria kama uliweza kufaulu darasani kwenye shule isiyo na waalimu, maabara, na maktaba. Ukafanya juhudi, ukajituma na kuwa na nidhamu ukafaulu. Ni nini kinakushinda sasa hivi kwenye maisha ya kawaida?
Usiseme ujobless, au kukosa connection.
Kukosa connection ni sawa na mwanafunzi kufaulu pasipo Mwalimu.
Fimbo uliyoitupa baada ya kumaliza chuo ni kukosa nidhamu na umepunguza ari ya kujituma. Na sio kukosa kazi au kukosa connection.

2. Kumcha Mungu na kuheshimu Watu.
Wakati upon kijana mdogo ulikuwa unamheshimu Mungu. Ukipatwa na changamoto unamlilia Mungu. Ikifika siku za mitihani ya shule unamlilia Mungu. Tena wengine mlikuwa mnafunga, wengine mnaenda kwa watumishi wa dini zenu, mnaombewa. Na kweli mnapita katika mitihani mliyokuwa nayo.
Kwa wale ambao hawajafika mbali kielimu, wakati unaanza maisha ulikuwa unamuomba Mungu akusaidie angalau utoke kijiji chenu ufike Mjini. Ili utafute fursa.
Mungu akakusaidia, hata kama ulipitia magumu lakini alikusaidia ukafike mjini.
Ukapambana mpaka ukaweza kujitegemea hata kwa chumba kimoja.

Leo umefika chuo ukahitimu unamsahau Mungu Yule aliyekusaidia, fimbo iliyokuongoza kipindi ukiwa kipofu umeitupa.
Leo kisa umepanga chumba au nyumba nzima umemsahau Mungu wako. Seriously!
Leo kisa umefika Mjini Dar es salaam au umeenda Marekani sijui wapi Leo wewe ni wakumkana Mungu kweli? Umesahau ulipotoka?
Unaleta usaliti kwa Mungu wako.
Inafikia hatua unasema hakuna Mungu, umesahau yote uliyopitia, umesahau ulivyokuwa unamlilia Mungu akusaidie. Kweli?

Umefanikiwa kidogo unadharau watu waliokusaidia wakati ukiwa huna lolote. Ngazi ulizotumia kupanda Leo unazitupa na kuziletea dharau. Hayo ni Makosa unafanya kijana.

Kamwe usiitupe fimbo uliyoitumia ulipokuwa kipofu kwa sababu hata kama sasa unaona kuna siku utaitumia kwenye Giza. Na kuona Leo haimaanishi utaona milele.

3. Kutoa Sadaka na Kusaidia wengine.
Moja ya msingi wa kufanikiwa kwako ni kutoa zaka na sadaka. Kusaidia wengine lakini pia kutoa zaka kwa Miungu yako.
Kuna sheikhe au mchungaji au mganga au kuhani ambaye unamuamini Sana basi peleka dhabihu au zaka huko ukamtolee Mungu wako. Yaani huyo kuhani akale.

Wewe sio muda wote utakuwa ukimuwaza Mungu. Sio muda wote utafuatilia habari za miungu yako. Lakini wapo watu wa KAZI hizo.
Mfano were ni fundi magari katika Gereji, hivyo shughuli zako zitahusu mambo ya magari. Hivyo wenye vyombo vya Moto wao watakuwa wanakuletea wewe magari na hawatakuwa watu wa kufuatilia mambo ya magari kwani hiyo sio KAZI yao.

Mambo ya kidaktari utamuuliza daktari.
Mambo ya Sheria utawauliza wanasheria.
Vivyohivyo, lazima utoe dhabihu au zaka kwa wale watumishi uliowachagua au dini au dhehebu ambalo watakuwa wanakuombea na hiyo ndio KAZI yao.

Kusanya pesa kwa Mwaka, sehemu ya kumi ya mapato yako, peleka kwa miungu yako. Kama unahisi hutakuwa na nidhamu ya pesa basi unaweza kupeleka kila wiki au kila mwezi.
Hakikisha kuhani anakuombea sio upeleke tuu.
Ikiwezekana uwe unamualika nyumbani kwako, ukiwa umeandaa vyakula vya heshima kwaajili ya kuhani au sheikhe au mganga wako afurahie.

Usiwe mjinga.
Mafanikio yako lazima uyalinde kiroho.
Lazima uhakikishe unafanikiwa na mafanikio yako yanakuwa na ulinzi QA kiroho.
Sio unakazi nzuri au pesa alafu mkeo anakusumbua au watoto wanakusumbua. Huna furaha.
Au unapesa lakini magonjwa yanaiandama familia yako. Huna furaha.
Au unamke mzuri na pesa lakini humridhishi kitandani. Huna furaha.

Au watu wanakudharau, licha ya kuwa unakila kitu.
Watibeli hatupo hivyo.

Mwanamke mzuri huolewi, na ukiolewa unateseka.
Mwanamke mzuri unajiingiza kwenye ufeminist hiyo ni dalili umeshafeli. Hakuna mwanamke aliyefanikiwa kimaisha mwenye furaha akawa feminist huyo mwanamke hayupo.

Kijana mdogo kila siku unaoa, wanawake wanakushinda, kuna fimbo umeitupa. Unaoaje wanawake kila siku kama sio unatatizo la msingi.
Kikawaida Mke ni Mmoja tuu ambaye mnaishi kwa furaha na hiyo ni moja ya ishara kuwa umebarikiwa.
Changamoto ndogondogo zinaweza kujitokeza lakini haziwi maudhui ya ndoa yenu.

Ni lazima utoe zaka na sadaka kwa ulinzi wa mafanikio yako. Ili uzidi kustawi.

4. Usiitupe Familia yako. Family First.
Kwenye maisha yako baada ya Mungu kinachofuata ni KAZI, kisha Familia.
Yaani huyo Mkeo/mumeo na watoto hao ndio wawe kipaombele chako.
Kisha familia uliyotoka wewe na familia ya mkeo.

Sio unajali watu back kuliko familia.
Kuna watu wanajali marafiki kuliko familia zap.
Kwenye historia ya Marehemu watakaotajwa ni Mkeo na watoto.
Hao ndio wataendeleza au kuharibu legacy yako. Rafiki zako hawatakuwepo.

Umepata kipesa kidogo unaanza kumsumbua Mkeo.
Unatelekeza watoto wako. Kweli?
Na wapo wanawake wamepata pesa kidogo wanaanza kuleta shida kwa waume zao.

Ndugu zangu, watibeli hatupo hivyo.
Tunatafuta pesa kwaajili ya Wake zetu. Na Wake zetu hutafuta pesa kwaajili yetu.
Mafanikio yoyote kwetu lazima yajengwe katika kufurahisha Wake zetu na watoto wetu.

Inaweza kutokea kuachana lakini kamwe usiishi na mkeo/mumeo kwa kuogopa IPO siku mtaachana. Utajikosesha Raha ya maisha na familia yako itakuwa kwenye tabu.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa SASA Dar es saaam
 
Mi naogopa kugongewa sijaoa hadi am 35, miaka kadhaa ilyopita Nilipokuwa below 25 nilikuwa nagonga wake Za watu naogopa sana kuoa
 
Kwa nini ulikuwa unagonga Wake za watu tena kwa Makusudi?

Kuchukua mali au kitu au wazo au mke au Jambo lolote lisilo lako hiyo ni dhulma
 
Back
Top Bottom