Uchaguzi 2020 Kosa watalolifanya wagombea wa upinzani kwenye kampeni za 2020

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Inafahamika kuwa nchi yetu imekuwa chini ya CCM tangu ipate Uhuru takilibani miaka 60 Sasa. Hivyo Kama Kuna mabaya au mazuri pongezi au lawama zozote Ni kwa CCM na sio kwa kiongozi wa awamu fulani.

Kama wapinzani watajikita kumlaumu kiongozi badala ya CCM kwa ujumla wake tangu Uhuru hadi Leo Basi watakosea na wanaweza wasiambulie kitu.

Waache kumkejeli, kumbeza na kumlaumu mgombea wajikite kwenye mazuri na mabaya ya CCM (Kama yapo) ya awamu zote. Angalau wananchi watawaelewa kidogo wanachotaka kuongea. Mfano, Kama wananchi hawana maji, barabara, hospitali, shule, dawa hadi Leo tangu tupate Uhuru hilo Ni kosa la CCM kwa ujumla sio la mgombea.

Mh. Rais anayo mengi aliyoyafanya ambayo yaliwafuraha baadhi ya wananchi, lakini anayo pia ambayo hayakuwafurahisha baadhi ya wananchi. Sasa mgombea makini lazima atenganishe Yale ya CCM, ya katiba, ya awamu ya tano na yale ya mgombea Kama mtu.
 
Mbona mnajihami sana na huyo mungu wenu!?
Tunawaonea huruma msije mkajichanganya na kupata kura 2 o'clock, huyu jamaa Ni wa new CCM, sio CCM ile tunayoifahamu. Huyu jamaa Kama utakazania kumrushia madogo unaweza kupingwa na wengi waliokwenda Xmas kwa kutumia treni mwaka Jana
 
Waache kumkejeli, kumbeza na kumlaumu mgombea wajikite kwenye mazuri na mabaya ya CCM
Ushauri potofu huu. Unajifanya unatoa ushauri kumbe una lengo la kumlinda jpm asipewe spana za uso. Acha alinywe alilo likoroga.
 
Sawa ushauri potovu, lakini utakuwa na kazi ngumu sana kwenda Dodoma na kusema JPM hafai hata baada ya kuwatengenezea mji wao. Nasikia treni ya mizigo imefika Arusha, nasikia Usafiri wa meli wa Mwanza kwenda Bukoba umezinduliwa. Umeme mwingi unakuja kutoka rufiji, IPTL, greko hazipo tena.

Msije mkajikuta mnazomewa kwa kumsema JPM vibaya. Ushauri wangu wa bure Ongeeni kuhusu CCM sio JPM
 
KIMENUKAAA!!! SIRI ZA ANTLISA ZAVUJAAA

Hii inatusaidia tu kufahamu kuwa Chadema ndio chama halisi Cha upinzani kilichobakia strong. Mti wenye matunda utarushiwa vigongo vingi Sana vya aina mbalimbali. Hadithi Ni nzuri lakini muda inayotolewa na guesture ya anayehadithia utaona tu Ni mwendelezo wa kuunga juhudi
 
Inafahamika kuwa nchi yetu imekuwa chini ya CCM tangu ipate Uhuru takilibani miaka 60 Sasa. Hivyo Kama Kuna mabaya au mazuri pongezi au lawama zozote Ni kwa CCM na sio kwa kiongozi wa awamu fulani.

Kama wapinzani watajikita kumlaumu kiongozi badala ya CCM kwa ujumla wake tangu Uhuru hadi Leo Basi watakosea na wanaweza wasiambulie kitu.

Waache kumkejeli, kumbeza na kumlaumu mgombea wajikite kwenye mazuri na mabaya ya CCM (Kama yapo) ya awamu zote. Angalau wananchi wataelewa kidogo wanachotaka kuongea. Mfano, Kama hawana maji, barabara, hospitali, shule, dawa hadi Leo tangu tupate Uhuru.
We nawe,. Nyie mnapelekwa na upepo, kabla mlisema CDM imekufa ghafla mmeanza kuwa washauri wa CDM,

Mikutano ya siasaa ilikatazwa na kampeni bado unawashwa washwa Nini?
 
Tunawaonea huruma msije mkajichanganya na kupata kura 2 o'clock, huyu jamaa Ni wa new CCM, sio CCM ile tunayoifahamu. Huyu jamaa Kama utakazania kumrushia madogo unaweza kupingwa na wengi waliokwenda Xmas kwa kutumia treni mwaka Jana
Jidanganye
 
Inafahamika kuwa nchi yetu imekuwa chini ya CCM tangu ipate Uhuru takilibani miaka 60 Sasa. Hivyo Kama Kuna mabaya au mazuri pongezi au lawama zozote Ni kwa CCM na sio kwa kiongozi wa awamu fulani.

Kama wapinzani watajikita kumlaumu kiongozi badala ya CCM kwa ujumla wake tangu Uhuru hadi Leo Basi watakosea na wanaweza wasiambulie kitu.

Waache kumkejeli, kumbeza na kumlaumu mgombea wajikite kwenye mazuri na mabaya ya CCM (Kama yapo) ya awamu zote. Angalau wananchi wataelewa kidogo wanachotaka kuongea. Mfano, Kama hawana maji, barabara, hospitali, shule, dawa hadi Leo tangu tupate Uhuru.
kama wananchi hawana maji safi na huduma bora za afya alafu kuna mtu katumia billions of money bila ridhaa ya bunge kujijengea uwanja wa ndege nyumbani kwake hapo tunabagaza muhusika na chama chake full stop.

Asante kwa kushiriki.
 
Ushauri potofu huu. Unajifanya unatoa ushauri kumbe una lengo la kumlinda jpm asipewe spana za uso. Acha alinywe alilo likoroga.
Hizi ndivyo akili za upinzani zilivyo kumpa spana jp ndio kutakupa kura wapiga kura wanataka kujua wewe ukiingia utafanya nini na sio kushambulia mwengine ila kwenye siasa hilo hutokea japo kidogo lakini halina nafasi kubwa tafauti na linavyochukuliwa na wanasiasa hapa tz
 
Ninawaonya Kama watajikita kwenye kumlalamukia JPM badala ya kutoa njia mbadala za kupata ndege zetu wenyewe, flyovers, meli, barabara, umeme, maji kwa wote, elimu kwa wote, afya kwa wote, na kuvitaja vyanzo vya Mapato ya kutekeleza hayo watagonga mwamba hakiya nani. Hizi shule za kata zimetusaidia angalau kupata wapiga kura wengi hadi vijijini ambao wanaweza kufikiria, sio Kama zamani. Mfano, wapiga kura wote wanafahamu kuwa wale waliokwenda kuunga juhudi walipewa kitu sio bure.
 
Inafahamika kuwa nchi yetu imekuwa chini ya CCM tangu ipate Uhuru takilibani miaka 60 Sasa. Hivyo Kama Kuna mabaya au mazuri pongezi au lawama zozote Ni kwa CCM na sio kwa kiongozi wa awamu fulani.

Kama wapinzani watajikita kumlaumu kiongozi badala ya CCM kwa ujumla wake tangu Uhuru hadi Leo Basi watakosea na wanaweza wasiambulie kitu.

Waache kumkejeli, kumbeza na kumlaumu mgombea wajikite kwenye mazuri na mabaya ya CCM (Kama yapo) ya awamu zote. Angalau wananchi wataelewa kidogo wanachotaka kuongea. Mfano, Kama hawana maji, barabara, hospitali, shule, dawa hadi Leo tangu tupate Uhuru.

Sikiliza uchaguzi wa US, Trump anapewa ukweli wake wazi wazi bila kujali kuwa ni wa Republican. Kama umekuja kutoa muongozo watu waongee nini kwenye kampeni, basi umeukalia.
 
Ninawaonya Kama watajikita kwenye kumlalamukia JPM badala ya kutoa njia mbadala za kupata ndege zetu wenyewe, flyovers, meli, barabara, umeme, maji kwa wote, elimu kwa wote, afya kwa wote, na kuvitaja vyanzo vya Mapato ya kutekeleza hayo watagonga mwamba hakiya nani. Hizi shule za kata zimetusaidia angalau kupata wapiga kura wengi hadi vijijini ambao wanaweza kufikiria, sio Kama zamani. Mfano, wapiga kura wote wanafahamu kuwa wale waliokwenda kuunga juhudi walipewa kitu sio bure.

Kama ccm inaamini hicho unachotaka kusema hapa, ni kwanini chaguzi zote za marudio na uchaguzi wa SM ulinajisiwa? Mbona hawakuacha watu wachague kwa utashi wao?
 
Sikiliza uchaguzi wa US, Trump anapewa ukweli wake wazi wazi bila kujali kuwa ni wa Republican. Kama umekuja kutoa muongozo watu waongee nini kwenye kampeni, basi umeukalia.
Usimlinganishe Trump na JPM, aliyoyafanya Trump kwa watu wake na aliyoyafanya JPM kwa watu wake Ni vitu 2 tofauti kabisa. Trump hana Cha maana alichowafanyia wamerakani. Nakuonya Tena lazima muwe more strategic katika kampeni zenu maana vile vijiji vilivyopata umeme Sasa wananyoa viduku salon hukohuko vijijini hawatawaelewa Kama mtamtukana JPM aliyewapa huo umeme
 
Hizi ndivyo akili za upinzani zilivyo kumpa spana jp ndio kutakupa kura wapiga kura wanataka kujua wewe ukiingia utafanya nini na sio kushambulia mwengine ila kwenye siasa hilo hutokea japo kidogo lakini halina nafasi kubwa tafauti na linavyochukuliwa na wanasiasa hapa tz
Ungeanza kumpa ushauri huu jpm. Vinginevyo kaa utulie hayakuhusu.
 
Kama ccm inaamini hicho unachotaka kusema hapa, ni kwanini chaguzi zote za marudio na uchaguzi wa SM ulinajisiwa? Mbona hawakuacha watu wachague kwa utashi wao?
Nadhani sababu kubwa ilikuwa kuokoa hela za kupiga kampeni ziende kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu badala ya kuzunguuka nchi nzima kupiga kampeni.
 
vile vijiji vilivyopata umeme Sasa wananyoa viduku
Bado una picha ya kizamani sana kuhusu watu wa vijijini. Unadhani wanaishi mambumbumbu. Na wao wanataka maisha bora, siyo kuwapa umeme ambao hata elfu tano ya kulipia bili hawana.
 
Usimlinganishe Trump na JPM, aliyoyafanya Trump kwa watu wake na aliyoyafanya JPM kwa watu wake Ni vitu 2 tofauti kabisa. Trump hana Cha maana alichowafanyia wamerakani. Nakuonya Tena lazima muwe more strategic katika kampeni zenu maana vile vijiji vilivyopata umeme Sasa wananyoa viduku salon hukohuko vijijini hawatawaelewa Kama mtamtukana JPM aliyewapa huo umeme

JPM hajampa mtu yoyote umeme, bali hizo ni kodi za wananchi, na kiongozi yoyote akiingia madarakani ana wajibu wa kupeleka umeme, maana kila ukinunua umeme kuna makato ya REA. Hakuna popote atatatukanwa bali, ukweli utawekwa wazi ili watu wachague kwa usahihi. Trump hajafanya lolote wakati katengeneza ajira za kutosha, ama hujui unaloongea?
 
Bado una picha ya kizamani sana kuhusu watu wa vijijini. Unadhani wanaishi mambumbumbu. Na wao wanataka maisha bora, siyo kuwapa umeme ambao hata elfu tano ya kulipia bili hawana.
Kwahiyo wewe ukienda ikulu utawapa hela ili wawe na maisha bora au utafanyaje na Corona hii. Wewe si ulikimbia bungeni kuogopa corona ukaenda kujilockdown. Ina maana ukishinda uchaguzi utaamrisha lockdown tujikinge na CORONA.

Nakuonya kwa Mara ingine kuwa kete yenu Ni kusema ubora wa Sera za chama chenu dhidi ya ubaya wa Sera za CCM tangu Uhuru hadi Sasa Kama upo badala ya kupoteza nguvu kumzungumzia JPM Kama JPM
 
Back
Top Bottom