Inafahamika kuwa nchi yetu imekuwa chini ya CCM tangu ipate Uhuru takilibani miaka 60 Sasa. Hivyo Kama Kuna mabaya au mazuri pongezi au lawama zozote Ni kwa CCM na sio kwa kiongozi wa awamu fulani.
Kama wapinzani watajikita kumlaumu kiongozi badala ya CCM kwa ujumla wake tangu Uhuru hadi Leo Basi watakosea na wanaweza wasiambulie kitu.
Waache kumkejeli, kumbeza na kumlaumu mgombea wajikite kwenye mazuri na mabaya ya CCM (Kama yapo) ya awamu zote. Angalau wananchi wataelewa kidogo wanachotaka kuongea. Mfano, Kama hawana maji, barabara, hospitali, shule, dawa hadi Leo tangu tupate Uhuru.