Uchaguzi 2020 Kosa watalolifanya wagombea wa upinzani kwenye kampeni za 2020

Nadhani sababu kubwa ilikuwa kuokoa hela za kupiga kampeni ziende kwenye miradi ya ujenzi wa miundombinu badala ya kuzunguuka nchi nzima kupiga kampeni.

Kama ni hivyo si ni bora wanasiasa wote waondolewe tuongozwe na jeshi tu.
 

Vinachanganywa vyote kuanzia sera za ccm, mpaka Magufuli mwenyewe. Kama Magufuli kajigeuza yeye ndio chama na ndio sera, anaachwaje kwa mfano?
 
Sasa chizi aliyebaki anajenga chatou ana msaada wowote huyu? Kama alichokifanya kama ni kizuri mbona wananchi wanamponda mbaguzi huyu? Ana kitete mpk anakataza tv kumuonyesha mbeba maomo.
B
 
Kama ni hivyo si ni bora wanasiasa wote waondolewe tuongozwe na jeshi tu.
Kaka shida kubwa ya CCM ilikuwa Ni kuhangaika na mambo ya watu wengine na kusahau mambo yetu yakiwemo ya Kiuchumi. Huyu JPM ameamua kwenda kinyume na siasa asili za CCM za kuhangaika na ya wengine badala yake ameamua kuhangaika na ya wananchi aliyoyaahidi. Zile kelele za huyoo huyooo mchinje mchinjee zinazopigwa na wapinzani hata baada ya mshindi kutangazwa ndizo zilizokuwa zikimkera JPM, zilikuwa zinalenga kumtoa kwenye reli ili aanze kuhangaika na kujibu mapigo badala ya kufanya ya wananchi
 

Kwahiyo nchi hii inaongozwa kwa utashi wa JPM na sio sheria na katiba? Sioni hata unaongea nini, tunaongea kitu kingine unaongea kitu kingine.
 
Alipokuwa anajinadi "Tanzania ya Magufuli" wewe ulikuwa wapi?
 
Sasa chizi aliyebaki anajenga chatou ana msaada wowote huyu? Kama alichokifanya kama ni kizuri mbona wananchi wanamponda mbaguzi huyu? Ana kitete mpk anakataza tv kumuonyesha mbeba maomo.

B
Mmmh! Jamani wakati Kilimanjaro barabara na umeme unapelekwa Hadi kwenye migomba wakati mikoa mingine haina barabara na umeme mbona hakukuwa na kelele? Kule Kilimanjaro barabara za lami zilikuwa zinaunganisha kata na kata wakati sehemu nyingine mkoa na mkoa ilikuwa ikiunganishwa kwa barabara za changarawe tu.
 
Wananchi wanahitaji kueleweshwa nini kingine kuhusu ubaya wa ccm ?

Kwanini uwapangie wapinzani cha kusema ?
 
Kwahiyo ndiyo maana miradi yote inapelekwa Chato?
 

Tunatwanga kote kote yaani CCM na JIWE kwa pamoja.
 
Alipokuwa anajinadi "Tanzania ya Magufuli" wewe ulikuwa wapi?
Alimaanisha kuwa CCM yake iliwafanyia makosa mengi watanzania huko nyuma, na ndio maana alikuwa anakataa kabisa kuwa Mwenyekiti wa CCM. Hii ndiyo maana hata CCM ya Sasa Ni nyingine kabisa. CCM ileee ya akina kinana na makamba mtu Kama polepole hawezi kuwemo humo.
 
Wananchi wanahitaji kueleweshwa nini kingine kuhusu ubaya wa ccm ?

Kwanini uwapangie wapinzani cha kusema ?
Siwapangii ninawashauri utu, Wana hiari kufuata au kuacha.
 
Yaani ccm unashauri wapinzani wafanye utu ?

Huna hata haya ?
Siwapangii Cha kusema ili Mimi Nina taaluma kubwa ya critical thinking, ninafahamu kuwa hata saa mbovu iliyosimama huwa inasema kweli angalau Mara 2 kwa siku hata Kama mishale yake imesimama.
 
Mkuu nakubaliana na wewe ila kuna kosa la kiufundi Chadema walilifanya mwaka jana baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa ambalo linaenda kuwalaza na viatu mwezi octoba.
Kama unavojua ule uchaguzi ulikumbwa na vitimbi na fitna za hali ya juu hali iliyopelekea wana chadema kuchukizwa na kama kuzilia utaratibu na mchakato wote wa uchaguzi.
Walionyesha kutoridhika na kuchukia kwa kuhamasishana kwa kutojiandikisha katika uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura matokeo ya kwamba bavicha wengi na wanachadema hawa ku update taarifa zao kwenye daftari so wengi wana kadi za mpiga kura za uchaguzi ulioisha.
Hawa wengi hawana vigezo vya kupiga kura kwa kuwa wengi wamehama maeneo waliyojiandikisha awali.
So wengi wanaojazana kwenye mikutano ya kuomba udhamini wa Mkenya Lissu wengi hawatapiga kura kwa kuwa wengi hawamo kwenye daftari la mpiga kura. Ccm wanapokwambia watashinda mapema sana kwa ushindi mzito wana uhakika na wanachokosema

Poleni bavicha, hasira ziliishinda busara, so subirini kugalagazwa
 
Mbinu hizi zinazofanywa Sasa zilifanywa pia na wakoloni dhidi ya akina Mwl. Nyerere na TANU ili kuhakikisha kuwa TANU haishindi uchaguzi. Lakini akina Nyerere hawa Hata akina Nyerere na Karume walikumbana na mbinu Kama hizi za kuwazuia kushinda uchaguzi, lakini wao hawakuhi kuchagua kususia kujiandikisha Wala kususia kushiriki uchangu, badala yake walitafuta mbinu Bora za kushinda uchaguzi kwenye chaguzi zilizofuata. Walizidi kuwashawishi na kuwaunganisha wananchi dhidi ya mbinu za mkoloni.

Wote lazima tukubaliane kuwa vyama vingi vyenye nguvu tunavihitaji kwaajili ya checks and balances, lakini ujasiri na sayansi vinahitajika pia katika kuvijenga vyama vingi. Sio kutukana na kulalamika tu lazima utumie nguvu nyingi dhidi ya mfumo na sio mtu Kama JPM. Kwakuwa hata JPM akimaliza muda wake CCM italeta mtu mwingine kwa kutumia taratibu zilezile zilizowaleta Marais wote 5.

Hivyo lazima ujue Ni wapi resources zako zitumike effectively. Mfano, Kama ukitumia resources nyingi kwenye uchaguzi ambao huna Imani ya tume ya uchaguzi na wasimamizi wa uchaguzi Ni kupoteza nguvu za wafuasi kwa maslahi yako ya kupata ruzuku na ubunge huku ukifahanu kuwa Tume haitakutangaza.
 
CCM wamekuwa dhaifu sana, JPM na genge lake wameona wajikite kwenye UHUNI na UHALIFU tu sasa. Hoja zimewaishia ni kutapatapata tu.
 
CCM wamekuwa dhaifu sana, JPM na genge lake wameona wajikite kwenye UHUNI na UHALIFU tu sasa. Hoja zimewaishia ni kutapatapata tu.
Ni kweli CCM imekata punzi tangu 2015, na haya Ni maneno ya Wana CCM wenyewe, ndio maana Rais JPM inaiita serikali ya Magufuli. CCM imemaliza kete zote za kusongeza inatumia kingi moja tu ya JPM. Ilala Sasa JPM Kama yeye anayo mazuri yake mengi kwa wananchi na mabaya yake Kama yeye ambayo yamejichimbia kwenye katiba
 
Usinipangie ukinipangia ndio unaharibu kabisa .
Sawa hutaki kupangiwa, lakini anaekuambia usikombe mboga anataka umalize ugali ushibe. Vyama vya upinzani miaka yote wanashiriki chaguzi tangu 1995 lakini hawafikii lengo, wanashindwa kuwashawishi wapiga kura ili waouone ukubwa wa tatizo la CCM, muda mwingi wanautumia kwa kufokafoka, kumlalamukia mtu, kutaja makosa ya watu binafsi na kubeza kila kitu badala ya kutumia muda mwingi kuongelea watakachofanya mara watakapoingia ikulu Tena kwa lugha rahisi inayoashiria amani, heshima na utulivu. Maana watanzania hawakuzoea lugha Kali, vurugu, Vita, na kejeli kwa viongozi. Muwaonyeshe kuwa amani yao waliyoizoea itaendelea kuwepo na kuboreka zaidi hata bila CCM kuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…