Kosea vyote lakini sio kuoa au kuolewa. Najuta


Pole mkuu ila wanawake 6 wote unaachana nao means tatizo lipo kwako.
 
Hakuna ndoa rahisi, uvumilivu wa hali ya juu unahitajika. Jifunze kuishi na madhaifu yake. Usije kuoa mwingine, mambo yakajirudia.
 
Kasoro ya mke jeuri au kiburi inaboa sana! Haivumiliki kirahisi
 
Duh furaha iko complex namna hii kumbe😅
 
😅😅😅😅😅😅 mke alikuwa anataka akutese kwa mgongo wa ndoa huyo,,, sema tupe dodoso kwamba ni nini alikuwa akifanya huyo mke
 
Ukimuacha, watoto watalelewa na Nani? Umeona mapungufu yake wewe huna mapungufu???

Kesi hii haiwezi kuamuliwa kwa malalamiko ya upande mmoja!

Madhara ya kuachana yatawakuta watoto ambao ugomvi wenu wala hauwahusu!
Kwahio unatetea kutoachana? Ndoa nzuri ni ile ya co-parenting tu kwa miaka ya sasa. Mke akae kwake na wewe ukae kwako muwe mnazaa na kulea tu ili kuepusha kero 😅 in case ukipata mwanamke atakaelikubali hili ni raha sana!
 
Simama na Mungu pekee ndiye atayekupatia amani ya roho na utulivu wa maisha.

AYUBU 22:21.

Job 22:21

"Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia."
 
[emoji1][emoji1]
 
Siupendi huu ushauri....there is always second chance.
Umekaa kibinafsi sana, unaweza jifunga kwa mtu ambaye sio stahili yako ukawa unateseka tu kumbe Mungu ana makusudi yake mbeleni!
 
Tuvumiliane tu hakuna aliekamilika chini ya jua na hautampata kamwe.
 
Kuna jamaa yangu, mke wake alimsumbua sana, nilimpa ushauri ambao leo ananishukuru sana, nilimwambia aende mahakani afanye process zote za talaka huku anamuangalia mwenendo wake, alifumgua shauri la kumpa talaka mke wake, mke wake hakuamini siku analetewa wito wa kufika kwenye shauri, alilia sana.

Alipungua uzito mpaka huruma ilinijia ila nilimwambia dogo komaa hawa watu sio wakiwaonea huruma kirahisi hivyo, shauri liliendelea mpaka talaka ikatoka siku hiyo ilikuwa ngumu sana kwa mwanmke alizimia, hakuamini walikuja ndugu kibao wa mwanamke kumuombea msamaha.

Basi tuliongea na hakimu tukamweleza tunaomba mahama ihold hukumu wakati tunafuatilia mwenendo wa mke wake, mahakama ilikubali, mpaka leo mwamke amebadilika sana sana.

Sikushauri sana hili ila wewe angalia la kufanya
 
Huyo unaweza kuuwa, ukaishia gerezani bure, piga chini chukua mwingine.
 
Pole mkuu ila wanawake 6 wote unaachana nao means tatizo lipo kwako.
🤣🤣 kabisa.
sijui ujana ndiyo ulikuwa unasumbua na uhakika wa Ndululu ndogo ndogo unatupa vibuli sana vijana.
kwasabubu mtu anazingua kidogo tu nitachukua nguo zangu naacha kila kitu, kesho nenda shop nitachukua mazaga kama yote.
ilikuwa kama vile nimepigwa pumbao, ghafla nikama vile pumbao limenitoka ninaanza jistukia vile time nimepotezana pesa nyingi sana.
 
umewahi kuyajua hya yote! hongera sana..! kila marefu yana ncha mkuu! furaha ya kweli ni kumcha mungu! maana yeye ndio atatia nuru ya furaha kwenye nafsi yko..! hyo mengine ya pesa magari na nyumba ni ya shetani🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…