Wanasema kosea vyote lakini sio kuoa au kuolewa
Nipo kwenye ndoa nae mwaka wa sita huu lakini sasa ni mtihani mtupu
Mke wangu ana kiburi cha asili,gubu na wivu wa kijinga sana na kwenye ndoa tuna watoto watatu
Hakuna kitu anachokosa huyu mwanamke kila kitu namtimizia
Hakuna anachokosa natimiza wajibu wangu kama mume, sijikwezi lakini ukweli mke wangu ni miongoni mwa wanawake walio kwenye ndoa wanaopata kila hitaji bila kusita au kucheleweshewa
Lakini hataki kubadilika ana mambo ya kipumbavu kabisa hapa naandika nikiwa na hasira sana nitamuacha tu nioe mke mwengine kama mke wa pili mpuuzi huyu
Unaweza kuoa ukakuta huyo uliyemuoa ndiye mwenye Tabia mbaya kuliko huyo wa kwanza, alafu kuoa mke wa pili ni dhambi mbele za Mungu, unajikatia tiketi ya moja kwa moja kwenda jehannum ya moto! Hapo mwenye matatizo ni wewe wala sio huyo mwanamke , mwanamke yupo chini mwanaume siku zote, umesema unamtimizia kila kitu hapo ndo kosa lako lilipo mkuu! Mwanamke lazima kuishi Naye kwa akili mno! Na ujitahidi asikusome jinsi ulivyo! Wewe huyo mwanamke wako umemzoesha vibaya na amekusoma kuwa wewe ni baba usiye na maamuzi, huna msimamo, mpole mno, hivyo yeye amechukua nafasi yako, ukiwa mwanaume lazima uweke sheria za nyumba yako au familia yako na zifuatwe mkuu!! Haijalishi ni mwanamke wa namna gani akikuona wewe hutabiriki atakuheshimu tu! Mfano
1;Mwanamke ana marafiki wa ajabuajabu na wewe upo tu unaangalia
2: mwanamke kila mara anaenda kwao au kwa ndugu zake hili ni tatizo kubwa mkuu ukiliruhusu tu umeisha
3: mwanamke kila sherehe anaenda hata sherehe ambazo hazina maana anaenda ukimruhusu mwanamke wako kufanya hivyo umeisha mkuu
4: vikundi mbalimbali, mfano vikoba hivyi vikundi ni vizuri lakini ukimwendeleza mke wako kwa kila kikundi anaingia umeishi mkuu
5: jitahidi kufanya kile unachopenda wewe hata kama yeye hataki mzoeshe hivyo mfano mda wa kurudi nyumbani
6: sio kila hela Akiomba lazima mpe zingine jaribu kumute alafu unakuja unampa siku ambayo hajakuomba!
Alafu mkuu Simamia sheria zako! Wanawake wote wanafanana tatizo ni uongozi tu wa mwanaume!