Kosea vyote, usikosee mume

Japo mie ni mwanaume but umesema kweli tupu

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 

Wanaume wengi wa namna hiyo ni wale waliolelewa na single mother, wanaharakati ambao kwenye ndoa zao wao ndio waume na wanawake, hawa wanakuwa wanataka kuhakikisha kama vile mtoto huyo hakui. Mama anataka ku control kila kitu cha mwanawe kwa kuwa yeye ndio alimsomesha, alimlea, anaona kama mke ni wakuja tu hatakiwi kufaidi matunda.

NB: Sio single mothers wote wanapenda huo ujinga ila asilimia kubwa ni wasumbufu sana kwenye ndoa za watoto wao wote.
 
Wazazi hao hao ndo wamefanya huyo jamaa afike hapo na akutane na ww.

Kama unaona huwezi toboa nae unaondoka unatafuta sehemu ambapo hakuna shida kama hizo.

Mbona simpo tuu.
 
Huyo mdau ana matatizo,usahihi wa mambo ukipata hela kwanza mpe mkeo kisha wazazi wako,kisha wengine.

Ila wake zetu nyinyi pia huwa mna matatizo sana hasa ubinafsi. Kuna muda huwa hamtaki tuwape ndugu zetu bali hata wazazi wetu.
 
Tafuta Pesa Dada. Lea Wanao kwa upendo na katika hofu ya Mungu.
 
Shukran kwa kumjibu kiungwana.
 
Kwenye haya maisha ya ndoa, mwanamke unapokuwa huna kipato kabisa unategemea kila kitu kitoke kwa mumeo, utaishi maisha ya ajabu na ya mateso sana.

Wanawake tujishughulishe, tuwe na vipato pia hata Kama ni kiasi kidogo, kwa juhudi na maarifa kipato kitaongezeka.
 
Jackline, kama umeolewa tathmini nafasi yako (mchango wako kihali na mali) katika hiyo ndoa. Kama hujaolewa, namshauri mchumba wako (kama unaye) akujue vizuri kwanza
 
Kama ni kweli nyie ni wanandoa hamfanyi fair coz ni kama mnaanika madhaifu yenu tuyajue tu basi
 
Mimi ukiigusa familia yangu yaani watoto wangu na mke wangu hakika umenigusa mimi,hata kama ni ndugu yangu wa damu hatutaweza kuelewena abadan!Mama na baba wanayonafasi lakini yenye mipaka.Nitatoa huduma kwa kumshirikisha mke wangu au yeye mke wangu huduma azifikishe kwa wakwe zake.Mama akitaka kuja kuniona mwanawe lazima nijipange kama nina chumba na sebule siwezi kumlaza mama yangu sebuleni ateseke lazima alale chumbani tena chumba comfortable,sasa kama chumba ni kimoja mama yangu hatokuja kwangu labda kuwe kuna mama ndani ya nyumba mwenye heshima zake na stara nimuombee mama yangu kukaa hapo kwa muda specified!Kama hayo hayawezekani na mama haji kwa ajili ya matibabu basi mama akae kwa kutulia kijijini!Akija mzazi kama ni kwa uzima tu na kupumzika lazima waje wakae hotelini hata ya 25,000/=kwa siku hapo Dar!
 
Huenda choyo ndicho kinachokusumbua!

Halafu ukute nduguzo wanakuja hapo na wanahudumiwa na huyo mume unaona ni sawa ila ndugu wa mume tena wazazi inakuuma?’

Ukiona mwanamke hataki wageni tatizo huwa ni choyo.

Imeandikwa: “iweni wakarimu kwa wageni sababu kwa kufanya hivyo wengine wameweza kuwakaribisha Malaika wa Mungu.

Na ujue Malaika wa Mungu akija faida zake ni nyingi.
 
Kwaiyo akikutembelea ndo alale hapo ??
Yaan wewe na mke wako mmelala kitandani alafu Mama yako naye amejikunja chini hapo, ukimshika tako mkeo bi mdashi anajifunika uso [emoji23][emoji23][emoji23]
Teh teh teh teh....nyie raia bhana haaa haaa ahaaa😂😂
 
Hv unazani mama mkwe ali hustle vip na mwanae mpka kawa hvyo mnakutana ukubwani, acha mother afaidi matunda ya mwanae kwanza.
Mtoa mada pitia maoni ya hawa wadau.

Vipi na wewe mama yako hujawahi kumleta hapo.
 
Yaani wanaume huwa wanakuwa rational and logical until mama zao wakitajwa.

Yaani hata aambiwe mama alimshikia mkewe kisu kooni ataishia kusema mke kamshikisha mama kisu.

Kukushauri mleta mada; fight battles utakazowezana nazo. Kuna tabia huwezi zijua hadi uolewe na mtu hivyo prevention inaweza shindikana.

Achana na kuweka resistance linapokuja suala la mwanaume na nduguze. Hutoishi kwa amani kamwe!
 
mimi wanawake siwaamini kabisa. yupo radhi apindue ukweli ili aonewe huruma na hadhira. mlete mumeo naye tumsikie
 
Mimi najua ukimkosea mume atakufanya kitu kibaya Sana.

Hata kama umekosea unaweza ukamrudisha kwenye mstari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…