Sizungumzii kumshauri mtoto wako, huo ni wajibu wako. ikiwezekana hata kumsaidia ili asonge mbele.
Pili, sikatazi wazazi kuomba msaada kwa watoto wao au watoto kuwasaidia wazazi wao.
Nachozungumzia mimi ni wazazi kuwapa watoto space, hivi kwa mfano mtoto wako ndo kaingia kwenye ndoa, hajajenga, wewe mzazi uko nyumbani kwako?
Inaingia akilini kumkomalia mtoto wako afanye ukarabati wa nyumbani kwako/kwao huku hata kiwanja hana? kwa nini usimkomalie ajenge kwanza?
Pili, ndo kwanza amepata mtoto au hajapata, kuna sababu ya msingi kumkomalia asaidie kusomesha watoto wa ndugu zake? badala ya kumkomalia akazane fasta apate watoto mapema?
Tatu, unaamia nyumbani kwa mtoto wako, hauumwi, wala huko kwako sio kwamba mafuriko yameharibu nyumba au kuna vita, why? unajifanya wewe mtoto wao au?