Wakuu,
Tulikuwa tunapiga stori kijiweni wakasema kama huna kovu la ndui kwenye bega la mkono wa kulia basi ujue chanjo hiyo haijafanya kazi. Kwahiyo sisi ambao hatuna hilo kovu ndio inamaanisha chanjo iligoma kufanya kazi au?
Hii ni kweli, au maneno tu ya mtaani? Maana sioni kabisa uhusiano kati ya kovu na chanjo kufanya kazi.
Tulikuwa tunapiga stori kijiweni wakasema kama huna kovu la ndui kwenye bega la mkono wa kulia basi ujue chanjo hiyo haijafanya kazi. Kwahiyo sisi ambao hatuna hilo kovu ndio inamaanisha chanjo iligoma kufanya kazi au?
Hii ni kweli, au maneno tu ya mtaani? Maana sioni kabisa uhusiano kati ya kovu na chanjo kufanya kazi.
- Tunachokijua
- Kifua kikuu ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya bakteria na huenezwa kwa njia ya hewa.
Mtu mwenye maambukizi ya kifua kikuu akikohoa, kupiga chafya au kutema mate ovyo husambaza vijidudu hivyo hewani, huweza kumwambukiza mtu mwingine.
Ugonjwa wa kifua kikuu huwa na dalili nyingi. Baadhi ya dalili muhimu za ugonjwa huu ni;
- Kukohoa kwa muda wa wiki 2 au zaidi
- Maumivu ya kifua
- Homa za usiku
- Kutoka jasho kwa wingi usiku
- Kupungua uzito
- Kukohoa damu
- Kukosa hamu ya kula na mwili kuwa dhaifu
Bakteria wanaosababisha ugonjwa huu jamii ya Mycobacterium tuberculosis waligunduliwa rasmi Machi 24, 1882 na Dr. Robert Koch. Hadi leo, Kifua Kikuu imebaki kuwa hanga kubwa linaloondoa uhai wa watu wengi duniani.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), mwaka 2021, watu milioni 10.6 waliugua ugonjwa huu huku wengine milioni 1.6 wakipoteza maisha.
Uhusiano wa chanjo na kovu
Kifua kikuu ni miongoni mwa magonjwa yaliyo na chanjo. Chanjo hii inayofahamika kwa jina la Bacille Calmette-Guérin (BCG)) hutumika katika kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa kifua kikuu. Ilianza kutumika kwa binadamu kwa mara ya kwanza mwaka 1921 baada ya kugunduliwa na wanasanyansi wawili Albert Calmette na Camille Guérin.
Kwa Tanzania, chanjo hii huchomwa kwenye bega la mkono wa kuume. Hufahamika zaidi kwa lugha ya utani kama Kovu la Mtanzania.
Uhusiano wa kovu na kinga ya Kifua kikuu
Mjadala wa kutokea kwa kovu baada ya kupata chanjo ya kifua kikuu kama njia ya kupima ufanisi wa chanjo husika umekuwepo kwa miaka mingi.
Kwa maana rahisi kabisa, uwepo wa kovu hutoa ishara chanja ya ufanisi wa chanjo husika katika kutoa kinga ya ugonjwa wa kifua kikuu. Vipi wasio na kovu?
Utafiti wa Adam Roth et al (Juni 2005) wenye kichwa cha habari "BCG vaccination scar associated with better childhood survival in Guinea-Bissau" unatoa mwanga juu ya mjadala huu.
Pamoja na uwepo wa madai kuwa kovu sio ishara halisi ya ufanisi wa chanjo, na kwamba sio lazima kuirudia kwa watoto ambao hawajapata kovu hilo, Adam na wenzie wanasisitiza kuwa kwa mujibu wa utafiti wao, watoto waliokuwa na kovu nchini Guinea Bissau baada ya kupatiwa chanjo hiyo walikuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kupambana na magonjwa kuliko wale wasio na kovu.
Aidha, wanabainisha pia kuwa uchunguzi mmoja uliofanyika kwenye mojawapo ya hospitali nchini Malawi ulionesha watoto wenye kovu kuwa na kiwango kidogo cha kupatwa na maambukizi ya ngozi na mchafuko wa damu kuliko wale wasio na kovu.
Huu ni ushahidi unaoweza kutumika katika kuthibitisha madai ya kovu na uhusiano wake katika kuonesha ufanisi wa chanjo.
Hata hivyo, ukubwa wa kovu hauna athari yoyote katika kuwakilisha uthabiti wa kinga ya mwili wa mtu.
Utafiti wa J A Stenne et al wenye kichwa cha habari "Does bacille Calmette-Guérin scar size have implications for protection against tuberculosis or leprosy?" unathibitisha haya.
Hitimisho la utafiti huu linasema;
"Hatuoni ushahidi kwamba ongezeko la ukubwa wa kovu la BCG ni uhusiano na uwezo wa kinga inayotokana na chanjo dhidi ya kifua kikuu au ukoma."
Hii inatoa maana kuwa mtu mwenye kovu kubwa na mtu mwenye kovu dogo wote huwa na kinga sawa dhifi ya kifua kikuu na ukoma.
Pia, kovu hili ni njia rahisi ya kutambua watoto waliochanja na wasio chanja. Husaidia kwenye kampeni za kupambana na ugonjwa huu hasa kwenye jamii zisizo na uwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu wa chanjo wanazopatiwa watoto.
Kwa mujibu wa utaratibu wa Mpango wa Taifa wa Chanjo Tanzania ulio chini ya Wizara ya Afya, BCG hutolewa baada ya mtoto kuzaliwa au pindi anapofika kliniki kwa mara ya kwanza. Ikiwa kovu halitajitokeza, chanjo husika hupaswa kurudiwa ndani ya miezi 3.