Bachelor of Science in Mathematics.
Hata chuo kilikua na mpango wakuimodoa hii kozi, sijui kama bado ipo kama ilivokua.
Aliyekuja kunikagua field alikua honest, "nakushauri kama kijana mwenye ndoto, ili usipate shida kwenye career yako, lazima field yako uichanganye na either uchumi, takwimu au finance", alinishauri. Hayo alishauri niyafanye kwa masters maana it was too late kwa bachelor.
Asante Dr. ____, ulinipa A ukanitoa kimasomaso ila huku mtaani mi ni bwege tu kama mabwege wengine. Familia duni sikuweza kusoma masters. Sijawahi ona kazi inamtaka Mathematician.
Nimedandia kazi nyingi sana za watu. Nimeshafundisha mpaka shule ya msingi(teh teh).
Mkuu wa department alisemaga one of the most paying job in America is being Mathematician. Sasa nimejiandaa kumpigia kura Hashim Rungwe kama sio Gwajima(Jimboni), nadhani ule mpango wenye umarekani unaweza badilisha maisha yangu.
Nikimaliza CPA naweza nikadandia kazi za wahasibu. Nikikwama hapo basi 2022 nitafungua kanisa. Samahani ninaexplore option zote, sitaki kufa nikiwa fukara.
Af kuna mtu kanambia nikisoma postgraduate education ntaajiriwa kama mwalimu halmashauri, nitalipwa laki saba na kumi na sita (716,000/=)
Take home 467,000/= Mbona nayo maisha tuu..