Kozi hizi za degree zimesitishwa kwenye vyuo vifuatavyo, Fanya maamuzi mengine kama ulikuwa na mipango ya kusomea

nguvu ya buku

Senior Member
Joined
Jul 15, 2025
Posts
168
Reaction score
549
Vyuo hivi havitapokeo maombi ya kozi zifuatazo kwa mujibu wa Tume ya vyuo vikuu (TCU)

SAUT Mwanza
  • Bachelor of Laws
  • Bachelor of Arts in Sociology
  • Bachelor of Philosophy with Education
  • Bachelor in Tourism and Hospitality Management

UDOM
  • Bachelor of Education in Science with ICT
  • Bachelor of Education in Psychology
  • Bachelor of Education in Science
  • Bachelor of Education in Commerce
  • Bachelor of Education in Arts
  • Bachelor of Education in Adult Education and Community Development
  • Bachelor of Education in Guidance and Counselling
  • Bachelor of Education in Administration and Management
  • Bachelor of Education in Policy Planning and Management

St. John - Degree ya Pharmacy

Kampala - Degree ya Medical Doctor
 
Duuh, bora kwenda chuo cha kati kusoma certificate ya jinsi ya kufuga kuku, samaki au nyuki kwa muda wa miezi 3 hadi 9 kisha urudi mtaani kutumia ulichojifunza.

Hayo madigirii mtaani hayana nafasi kama hauna maarifa ya kupambana na mtaa.
 
Vyuo hivi havitapokeo maombi ya kozi zifuatazo kwa mujibu wa Tume ya vyuo vikuu (TCU)

SAUT Mwanza
  • Bachelor of Laws
  • Bachelor of Arts in Sociology
  • Bachelor of Philosophy with Education
  • Bachelor in Tourism and Hospitality Management

UDOM
  • Bachelor of Education in Science with ICT
  • Bachelor of Education in Psychology
  • Bachelor of Education in Science
  • Bachelor of Education in Commerce
  • Bachelor of Education in Arts
  • Bachelor of Education in Adult Education and Community Development
  • Bachelor of Education in Guidance and Counselling
  • Bachelor of Education in Administration and Management
  • Bachelor of Education in Policy Planning and Management

St. John - Degree ya Pharmacy

Kampala - Degree ya Medical Doctor
Ohooo kwanini wameamua kutoa,
 
Law School wanafunzi wanaoongoza kwa ufaulu ni Udsm na Mzumbe

Hao SAUT umewapima kwa mitihani ya ndani ya chuo chao au ?

Halafu Saut kwa kiasi kikubwa wanaosoma Law ni tawi la Arusha na Mbeya ambao wamebadili jina, kwa Mwanza nafasi walikuwa wanadahili wanafunzi wachache sana
Achana na siasa za 1st seating ni SAUT na Tumaini Makumira ndio vyuo vyenye wahitimu wengi wa Law School. Kasome fact sheet ya LST
 
Ni fact kwamba vyuo vya makanisa kama Tumaini, Teku, Mwecau, SAUT hasa ya Mbeya iliyobadili jina kuwa CUom na Ruaha wanatoa graduates wengi wa sheria. ni kawaida kukuta batch inatoa graduates 300 kila mwaka

Cha ajabu ni kwamba bado wanakimbizwa Law School na wahitimu wa Udsm na Mzumbe, kumbuka law school wanaopita ni wachache, sio kama vyuoni almost watu wote wanagraduate kwa kutofautiana gpa.

Hata ukija kwenye Uhasibu mitihani ya CPA vyuo vya makanisa bado vipo nyuma kwenye ufaulu.

Nachovisifu vyuo vya makanisa ni gharama nafuu za ada, wanajitahidi mfano kusomea law CUom Mbeya ni milioni 1 na laki 2 tu, hata lecturers wa vyuo vya makanisa wanalipwa kawaida maana ni kazi ya kujitolea zaidi.
 
Ningekuwa sijapita Law School ningekusikiliza hichi kitu unataka kusema. Ila nimepita pale napafahamu vyema LST. Graduates wa SAUT na Tumaini Makumira ndio wanaonesha kufanya vizuri zaidi LST.

Na kuna scandal kibao kuhusu hao unaowatetelea hapa.
 
Nimefuatilia nimeona ni kweli SAUT Mwanza walikuwa wanakimbiza licha ya uchache wao wa wahitimu tofauti na vyuo vingine vinavyofyatua wahitimu zaidi ya 150+

Lakini najiuliza maswali mengi

Kama chuo kilikuwa kinafanya vizuri kwanini kimefungiwa ?

Ni siasa za kuzidi kuididimiza kielimu mikoa ya kanda ya ziwa ?

Rejea uzi huu

Nimefuatilia nimeona ni kweli SAUT Mwanza walikuwa wanakimbiza hasa first pass

Lakini najiuliza maswali mengi

Kama chuo kilikuwa kinafanya vizuri kwanini kimefungiwa ?

Ni siasa za kuzidi kuididimiza kielimu mikoa ya kanda ya ziwa au ?

Rejea uzi huu

Yapo mengi kwa sasa tu pale SAUT kuna wanafunzi takribani elfu tatu wanasoma fani ya sheria tu. Pata picha.

Nadhani serikali na wadau wa sekta wameamua kupunguza idadi ya wahitimu kwenye hii fani na njia rahisi ni kuondoa kwa baadhi ya vyuo ili pia kupunguza gharama za uendeshaji na labda wameichagua SAUT kwasababu tayari ina wanafunzi wengi wa kitivo husika

Haya ni mawazo yangu tu, inapasa hii taarifa iwekwe wazi na sababu kuondoa taharuki kwa wazazi ambao watoto wao wanasoma fani hizi kwenye vyuo hivyo
 
Kwanini iwe chuo ambacho kinategemewa na mikoa yote ya ziwa na mingine ya magharibi ? (Mwanza, Kagera, Geita, Mara, Simiyu, Shinyanga, Kigoma, Katavi na Tabora) hivi sasa hakuna mbadala wa chuo chochote kinachotoa degree ya sheria katika mikoa yote hio, kama ni kupunguza wangeenda kwengine sehemu zenye vyuo vingi vya sheria. kumbuka kwa wakati huo huo Saut Arusha na Mbeya wanaendelea kutoa kozi hio ya law,

Wanafunzi elf 3 wa Sheria ni wote Diploma hadi Degree au ?

Nimeuliza hivyo kwasababu figure za udahili zipo tofauti, hizi ni screenshot za pdf ya udahili wa mwaka uliyopita mfano 2024 nimeona nafasi kwa kozi za sheria zipo chache hazifiki hata 100, tofauti na kozi nyingine kama za ualimu, business administration na arts zenye udahili mkubwa hadi wanafunzi 1000

1753229809149.png

1753229726560.png

1753229774027.png
 
Kwa saut hizo ndio course ambazo zinawabeba saba kuziondoa ni kuwafanya wapotee katika soko la ushindanishi

Udom hapo ni kubalance tu mambo lakini hapo kuna fitina za udini
Roma inatafutwa kwe ye uwekezaji wake

Mi sio mroma ni mruther kabisa lakini hapa naona kuna kuumizana kusiko sababu na ndio mana wanafuta bila kuanisha sababu maana itakuwa aibu
 
Yaani hadi inashangaza, Kozi walizotoa Saut Mwanza hadi unajiuliza hupati majibu yaliyonyooka.

Kuhusu udini sijajua maana kuna vyuo vingine vya kikatoliki havijaguswa

  • Chuo katoliki cha Mbeya - Kinakuwa kwa kasi, uwekezaji uliofanyika ni mkubwa sana ndani ya muda mchache
  • Chuo katoliki cha Ruaha - Iringa
  • Chuo Katoliki cha hospitali ya Bugando - Mwanza
  • Chuo Katoliki cha Mwecau - Moshi

Na vyote kasoro Bugando vinatoa kozi za Sheria kwa wanafunzi kibao kila mwaka.

Labda kama wamelenga kikubwa zaidi
 
Kwa saut hizo ndio course ambazo zinawabeba saba kuziondoa ni kuwafanya wapotee katika soko la ushindanishi

Udom hapo ni kubalance tu mambo lakini hapo kuna fitina za udini
Roma inatafutwa kwe ye uwekezaji wake

Mi sio mroma ni mruther kabisa lakini hapa naona kuna kuumizana kusiko sababu na ndio mana wanafuta bila kuanisha sababu maana itakuwa aibu
Hata mimi nahisi kuna harufu ya kitu hapa. Siku zote hakuna jambo lenye mwanzo, halafu likakosa kuwa na mwisho. Muda utasema.
 
Back
Top Bottom