Natumai mu wazima wa afya. Pole kwa wanaoumwa, Mungu awajaalie mkapate afya njema.
Nimeona niwashauri kuhusu kozi na taaluma za kuwa nazo, vijana wetu wenye lengo la kwenda kujitolea JKT ili baadae waje kupata nafasi ya kuandikishwa JWTZ kwa urahisi.
Kijana, kama una nia ya kuja kulitumikia taifa letu hili pendwa la Tanzania kupitia kuwa mwanajeshi JWTZ, soma kozi hizi ili ukienda kujitolea JKT ikuwie rahisi kuandikishwa kufanya kozi ya jeshi la wananchi JWTZ.
1. Kozi zote za afya. Udaktari, unesi, ufamasia, radiographia n.k pata certificate, diploma, degree, masters mpaka PhD ya taaluma za afya, hutajutia.
2. Urubani. Ukisoma kozi hii, hata JKT unaweza usipite, ila sasa hakikisha kwenu muwe mna hela ya kutosha sio ya kubababisha maana urubani si mchezo, mpaka milioni 200 +.
Hizi ndio kozi za uhakika, ukiwa na hizo fani, ukaenda JKT, siku JWTZ wakija kuwafanyia usaili hutakosa kupata nafasi kwenda kuvaa bakabaka.
Mbali na hapo, jiandae kutoboa mkataba na kurudi nyumbani, au ujiandae kwenda polisi, Magereza, uhamiaji au wanyamapori (ukibahatika).
Ni hayo tuu kwa leo, nakaribisha michango ya wengine. Muwe na muda mwema sana