Kozi zitakazokuwezesha kujiunga kirahisi na JWTZ

Kozi zitakazokuwezesha kujiunga kirahisi na JWTZ

Nakumbuka miaka ya nyuma wakati nipo jkt walikuja kufanya usahili wa kuchukua vijana waliosoma science yani PCM,PGM, na PCB na walivyo na akili walikuja wakati wa (six week) kipindi hicho mtu akikwambia tukuandikishe ili badae uende jwtz ukapige kozi ilikuwa ni ngumu sana kukushawishi kutokana na mateso yale ya jkt afu ukateseke tena jwtz Hapana! Nakumbuka waliambulia vijana wachache tena kwa kulazimisha akiwemo rafiki yangu mmoja ambae alikuwa doja mzuri tu na mvivu wa kazi za shamba. Baada ya kumaliza mafunzo ya jkt tulienda chuo tukiwa mwaka wa kwanza rafiki yangu akapigiwa simu kuwa anahitajika kambi ya abdallah twalipo 95kj nadhani kama sijakosea akafanye usahili wa kuingia jeshin, nakumbuka tulimcheka sana nakumsihi asiende uko maana ataumia vibaya kwa mateso ila mwisho alienda na nikapoteza mawasiliano nae.
Siku moja katika harakati zangu za maisha wakati huo sina ajira na chuo nishamaliza
nilienda benki kumlipia mdogo wangu ada ya shule, wakati nimefoleni kwenye mstari kusubiri huduma nilishaanga kumuona askari polisi(FFU) nakusaruti kijeshi ile kutaamaki namuona jamaa yangu kavaa full kombati za kijeshi na ana cheo cha luten nyota mbili daaha roho iliniuma na nilijiona mjinga sana
Anyway wadogo zangu hiyo nafasi ukiipata usichezee kabisa
[emoji38][emoji38] sema maisha ni fumbo gumu Sana, anyway vipi saizi mishe zimekaa fresh au BADO kitaa hakisomi
 
Yeah ni kweli kweli inashavu sana yeah unaweza kuwa rubani wa kumpaisha rais kwenda nchi mbalimbali na misele ya angani
Natumai mu wazima wa afya. Pole kwa wanaoumwa, Mungu awajaalie mkapate afya njema.

Nimeona niwashauri kuhusu kozi na taaluma za kuwa nazo, vijana wetu wenye lengo la kwenda kujitolea JKT ili baadae waje kupata nafasi ya kuandikishwa JWTZ kwa urahisi.

Kijana, kama una nia ya kuja kulitumikia taifa letu hili pendwa la Tanzania kupitia kuwa mwanajeshi JWTZ, soma kozi hizi ili ukienda kujitolea JKT ikuwie rahisi kuandikishwa kufanya kozi ya jeshi la wananchi JWTZ.

1. Kozi zote za afya. Udaktari, unesi, ufamasia, radiographia n.k pata certificate, diploma, degree, masters mpaka PhD ya taaluma za afya, hutajutia.

2. Urubani. Ukisoma kozi hii, hata JKT unaweza usipite, ila sasa hakikisha kwenu muwe mna hela ya kutosha sio ya kubababisha maana urubani si mchezo, mpaka milioni 200 +.

Hizi ndio kozi za uhakika, ukiwa na hizo fani, ukaenda JKT, siku JWTZ wakija kuwafanyia usaili hutakosa kupata nafasi kwenda kuvaa bakabaka.

Mbali na hapo, jiandae kutoboa mkataba na kurudi nyumbani, au ujiandae kwenda polisi, Magereza, uhamiaji au wanyamapori (ukibahatika).

Ni hayo tuu kwa leo, nakaribisha michango ya wengine. Muwe na mda mwema sana [emoji120]
 
Badala ya kuwaza kuwa waziri unawaza kuwa mwanajeshi daaaaaaa. Hii dunia ina mambooo kweli.
Huyo waziri lazima alindwe na askari kijana. Mwenyezi Mungu amempatia karama tofauti kila mmoja wetu, wote tukiwa mawaziri nani atailinda nchi yako dhidi ya uvamizi wa adui ? Nani atatibu wagonjwa ? Nani atakuwa raia ? N.k Ndio hivyo wewe unavyopenda uwaziri, wenzio wanapenda jeshi. Wengine wanapenda upadre, uchungaji n.k ndio mpango wa Mungu huu.
 
Jeshi halikaririki Mkuu..na Jeshi halina mtu muhimu..
 
Wapo mpaka maprofesa jeshini kijana, ni kawaida tuu. Jeshi limekuwa la kisasa linaenda na wakati.
uko sawa kabisa jeshini kuna wasomi walibobea kinyume na wanavyofikiri watu.Yuko mwanajeshi mmoja ni Professor,Dr Brigadier general Yadon ana taaluma ya udaktari.Hakuna taaluma uraiani jeshini haipo.Mnakumbuka muhimbili ma dr waligoma wanajeshi wakaenda kukamata usukani? mnakumbuka waongoza ndege airpot dar waligoma wanajeshi wakaenda kushikilia.Mnao dhani wanajeshi ni vilaza mnapotea sana.Hata Marekani wanaanga wengi wa NASA waliokwenda mwezini walikuwa ni wanajeshi.Pia gunduzi nyingi za kitabibu marekani zinafanywa na jeshi.Haa Lockheed Martin ina mkono wa jeshi
 
Huyo waziri lazima alindwe na askari kijana. Mwenyezi Mungu amempatia karama tofauti kila mmoja wetu, wote tukiwa mawaziri nani atailinda nchi yako dhidi ya uvamizi wa adui ? Nani atatibu wagonjwa ? Nani atakuwa raia ? N.k Ndio hivyo wewe unavyopenda uwaziri, wenzio wanapenda jeshi. Wengine wanapenda upadre, uchungaji n.k ndio mpango wa Mungu huu.
umemjibu hadi raha
 
Jeshi halikaririki Mkuu..na Jeshi halina mtu muhimu..
Linao watu muhimu ndugu, ndio maana wataalamu wanaohitajika huko huwa wanafanyiwa usaili wa kujiunga na JWTZ moja kwa moja. Hizo za kusema "jeshi halina watu muhimu" zinabaki kuwa siasa tuu za maneno, ila uhalisia ndio huo.
 
Nimekaa jkt miaka mitatu na ka bachelor kangu ka engineering lakini sijaambulia kitu aisee. In short jeshini sifa kushikwa mkono maana ajira zilipotolewa za wale jamaa waliojenga ikulu watoto wa wenye mibanga ndio walioongezewa kweny ajira bila kujali wew ni telecom eng. Civil eng. Comp eng. Software developer wala nn.
Inshort JKT to TPDF or to any defence organ, connection matters always, labda awamu hii mambo yabadilike ila Op mirerani daa tuliingia choo cha kike.
 
Linao watu muhimu ndugu, ndio maana wataalamu wanaohitajika huko huwa wanafanyiwa usaili wa kujiunga na JWTZ moja kwa moja. Hizo za kusema "jeshi halina watu muhimu" zinabaki kuwa siasa tuu za maneno, ila uhalisia ndio huo.
Haya wewe kariri tu kuwa jeshi lina mtu muhimu.
 
Tatizo humu kila mtu anaongea lake

Jeshini nako siku hizi connection kama hauna refa tena mwenye cheo kikubwa kule utasota sana hata uwe na masters ya aeronautical engineering

Nina ndugu yangu ana diploma ya sociology aliingia jeshini kwa connection na ndani ya miaka mitano tu akawa tayari ni lieutenant anakula maisha wakati kuna mtu na degree yake hiyo miaka mitano bado ni private anakimbizana na kuruta na kulima mashamba kila siku

Sent from my SM-G973F using JamiiForums mobile app
Acha uongo wewe
 
Back
Top Bottom