Kama tunaamini maandiko yanavyotueleza juu ya Yesu kristu kwamba alizaliwa pasipo na baba( wa ki inaadamu) kwanini basi Dr Sule amemjaji kama binadamu wa kawaida yaani mimba yake ilitakiwa iwe ya( miezi Tisa)????
Sasa kama mimba yake iliingia ki miujiza jee hawezi kuzaliwa ki miujiza???
WANAZUONI wengi duniani, bado wanaumiza vichwa kuhusu tarehe sahihi aliyozaliwa Yesu Kristo, ambaye ni Nabii wa Wakristo.
Miaka nenda rudi, vitabu vingi vimeandikwa na makundi ya wanazuoni wa dini na historia kuanzia Mashariki ya Kati, Amerika, Ulaya, Afrika na bado hadi leo, maandishi mapya yanaendelea kuchapishwa juu ya kuzaliwa kwa Yetu Mnazareti.
Mjadala huo upo na hakika hautakoma kwani wanaoandika wanapingana kwa hesabu na historia. Wameshindwa kupata tarehe hasa aliyozaliwa Yesu ambaye pia huitwa Masihi.
Miaka 2000 iliyopita, mtawala wa tano wa Wayahudi, Pontio Pilato alimuuliza Yesu wa Nazareti swali lifuatalo: “Ukweli ni kitu gani?”
Aliuizwa swali hili wakati anakaribia kupewa hukumu ya kuwambwa msalabani baada ya kukamatwa akituhumiwa kujiita “Mfalme wa Wayahudi.”
Yesu hakujibu swali hili. Na hadi leo, kambi kadhaa za wanazuoni zinazidi kuvutana kuhusu jawabu sahihi kwa swali hili. Mfano mzuri wa mvutano huo unajitokeza katika mjadala kuhusu “siku ya kuzaliwa kwa Yesu wa Nazareti.”
Mpaka leo, kuna siku tatu tofauti zinazotajwa kama siku za kuzaliwa kwa Yesu. Kuna Desemba 25, Januari 6 na Januari 7. Ufafanuzi wa utata huu unafuata.
Tuanze na Desemba 25. Haya ni mawazo ya Mtakatifu Hippolytus wa Roma. Kwa mujibu wa
utafiti wa Profesa Andrew McGowan wa Chuo Kiukuu cha Melbourne, mwaka 204BK, Hippolytus aliandika kwamba, “Tarehe ya kuzaliwa Yesu, Bethlehem, ni Desemba 25.”
Hippolytus alianzia kwenye tukio la Malaika Gabriel kumtokea Zakaria hekaluni na kumwambia kwamba mkewe Elizabeth angepata mimba na kumzaa Yohane.
Zakaria alikuwa kwenye ibada ya malipizi ya dhambi. Kwa mujibu wa kalenda ya Kiebrania ibada hiyo ilifanyika tarehe Julai 10 kila mwaka wa Kiyahudi.
Ulinganisho wa kalenda ya kale ya Wayahudi na kalenda ya kisasa unaonyesha kuwa siku hiyo ni sawa na Septemba 24 ya siku hizi. Hii maana yake ni kwamba Elizabeth alianza ujauzito wa Yohane Septemba 24.
Kwa mujibu wa uchambuzi wa Hippolytus, miezi sita baadaye malaika Gabriel alimtokea Bikira Maria na kumwambia atapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Hivyo, ujauzito wa Yohane ulioanza Septemba 24 uliutangulia ujauzito wa Yesu kwa miezi sita.
Hii maana yake ni kwamba, mimba ya Yesu ilianza Machi 25 na akazaliwa miezi tisa baadaye, yaani Desemba 25, anahitimisha Hippolytus.
Lakini, bado wapo Wakristo waliopinga tafsiri ya Hippolytus. Walihoji uhalali wa hesabu zake, wakitaka awaonyeshe hiyo miezi tisa ilikuwa na jumla ya siku ngapi.
Hawa wenye kupinga Krismas ya Desemba 25, huadhimisha Krismas ya Januari 7. Ni wafuasi wa Mfamle Julius Kaizari wa dola ya Kirumi. Sababu za upinzani wao zinafuata.
Katika mwaka 46KK Julius Kaizari aliunda kalenda iliyotokana na imani kwamba mzunguko wa dunia unachukua siku siku 365 tu. Lakini, baadaye wanasayansi waligundua kuwa mzunguko wa dunia huchukua siku 365 na robo.
Robo nne zinaunda mwaka mmoja. Hii maana yake ni kwamba, kila baada ya miaka mitatu, yaani katika mwaka wa nne, mzunguko wa dunia huchukua siku 366.
Miaka mitatu huitwa miaka mifupi, na mwaka wa nne kuitwa mwaka mrefu. Mwaka mrefu hugawanyika kwa namba “nne.”
Kwa mujibu wa “Kalenda ya Julius” mwaka wenye siku 365 una miezi 12; ambapo miezi minne ina siku 30, kila mmoja; miezi saba ina siku 31, kila mmoja; na mwezi Februari una siku 28.
Hesabu hizi hazihusishi siku 365 pekee kati ya siku 365 na “robo” za mzunguko wa dunia. Hivyo, kila baada ya miaka minne, “Kalenda ya Julius” ikawa inapoteza siku moja kamili.
Kwa ajili ya kuondoa dosari hii, katika kila mwaka mrefu, Julius aliamua kuongeza siku moja kwenye mwezi wa Februari, ili uwe na siku 29, na hivyo kukamilisha siku 366 za mwaka mrefu.
Kalenda hii ina miezi minne ya siku 30, miezi saba ya siku 31, mwezi Februari wa siku 28 katika mwaka mfupi, na mwezi Februari wenye siku 29 katika mwaka mrefu. Huitwa “Kalenda ya Julius”.
Baadaye
wanasayansi waligundua tena kuwa mzunguko wa dunia hauchukui siku “365.25” pekee, bali huchukua siku “365.24218967.” Hapa kuna tofauti ya siku “0.00781033,” sawa na dakika “11.2468752.” Yaani, kimakosa, “Kalenda ya Julius” ilikuwa imeongeza dakika “11.2468752” katika mwaka mzima.
Kanisa Katoliki lilianza kutumia kalenda ya Liturijia inayofuata mantiki ya “Kalenda ya Julius” mwaka 325. Lakini, mwaka 1582 Papa Gregory wa 13 aligundua makosa hayo yaliyo kwenye “Kalenda ya Julius.”
Hivyo, Papa akakosoa dosari husika kwa kuunda kalenda mpya, ikaitwa “Kalenda ya Gregory”. Baadhi ya Wakristo waliikataa mantiki iliyoongoza utengenezwaji wa “Kalenda ya Gregory” na kuendelea kutumia “Kalenda ya Julius.”
Hivyo, tangu mwaka 325 hadi leo imepita miaka 1697. Kwa kuzingatia tofauti ya siku “0.00781033” tulizoona hapo awali, hesabu ya kuzidisha inaonyesha kwamba “Kalenda ya Gregory” inaitangulia “Kalenda ya Julius” kwa siku “13.25413001.” Huu ni wastani wa siku 13 na robo.
Hivyo, wakati Wakristo wanaofuata “Kalenda ya Gregory” wanaposherehekea Krismas ya Desemba 25, wale wanaofuata “Kalenda ya Julius” watasubiri hadi Januari 7, yaani siku 13 baadaye.
Lakini pia, kuna Wakristo wanapinga Krismas ya Desemba 25 na kukataa Krismas ya Januari 7, wao wanaadhimisha Krismas ya Januari 6.
Kitabu cha “
New Advent Encyclopedia,” kinasema hawa wanaoamini Yesu alizaliwa Januari 6 ni wafuasi wa Clement wa Alexandria, nchini Misri.
Clement alionyesha kwenye kitabu chake kiitwacho “Stromata,” kwamba Yesu alizaliwa “Januari 6.” Baadhi ya Wakristo walikubaliana na Clement hadi leo.
Kutokana na mkanganyiko huo wa siku aliyozaliwa Yesu Mnazareti, ndiyo maana yapo maeneo duniani yanaadhimisha kuzaliwa kwake Desemba 25, wengine Januari 6 na wapo wanaofanya kumbukizi Januari 7.
Mchungaji wa Kanisa la Mfalme Yesu lililoko Mwanjelwa, Mbeya, Ibarhim Kalembo akizungumza na Pambazuko kuhusu tarehe hasa ya kuzaliwa Yesu Kristo, alisema ni kweli kuna tofauti kulingana na maeneo husika, lakini uhakika kabisa hauelezwi kinagaubaga na Biblia yenyewe.
Amesema katika vitabu vingi vya vya Injili, ambavyo vikisomwa kwa pamoja, kuna utata wa siku ya kuzaliwa Yesu Kristo, kwani haitamkwi wala kuelezwa kwa uwazi.
“Hata wewe ni Mkristo, umewahi kusoma ama kuelezwa mahali kwamba Desemba 25 ndiyo hasa alizaliwa Mwana wa Mungu (Yesu), hakuna, lakini watu waliamua iwe hiyo Desemba 25 kwa wengi, pamoja na kwamba wapo wanaopinga tarehe hiyo,” ameongeza mchungaji huyo ambaye amesema ana shahada ya uzamili katika teolojia.
Anaeleza kuwa mvutano wa siku ya kuzaliwa Yesu huenda usifike mwisho na labda unaweza kutatuliwa na Yeye mwenyewe siku atakaporejea na endapo atatoa nafasi ya kuulizwa maswali.
“Hili swali limetushinda, limewashinda hata wakongwe wa historia ya maisha ya Yesu, wakiwamo Wayahudi wenyewe, huenda siku nzuri ya kupata jibu na tutakapomuona Mwenyewe,” ameongeza.
Chanzo: Gazeti laPambazuko, Toleo la Jumatatu, Desemba 26, 2022-Januari 1, 2023, ukurasa wa 10-12.
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
Iron Chuma, 50thebe, Smart911 and 11 others
[IMG alt="dudus"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/38/38243.jpg?1413178530[/IMG]
JF-Expert Member
Yesu Kristo, ambaye ni Nabii wa Wakristo.
... kwani wakristo wanasemaje kuhusu huyo Yesu? Mbona mnawawekea maneno midomoni?
Anyway, la muhimu kuliko yote ni kwamba Yesu alitwaa mwili, akazaliwa, akaa kwetu akitufundisha njia sahihi ya wokovu. Hapa hata Shetani amekwama kupinga! Hayo mengine sijui tarehe sijui nini ni blah blah tu.
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
Kamkuki, Cleophace makuli, allypipi and 9 others
[IMG alt="Scars"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/427/427454.jpg?1558029127[/IMG]
JF-Expert Member
Kwenye hiyo picha ya huyo jamaa aliyenyoosha vidole viwili kuna wahuni walim edit wakamshikisha fegi kati kati ya hivyo vidole
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
allypipi, mkwepu jr, Sultan MackJoe Khalifa and 1 other person
[IMG alt="dudus"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/38/38243.jpg?1413178530[/IMG]
JF-Expert Member
.... Robo nne zinaunda mwaka mmoja
... isomeke "siku moja".
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
mkwepu jr and Mwalimu wa tuisheni
[IMG alt="REALITY"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/233/233335.jpg?1672388028[/IMG]
JF-Expert Member
Pita hapa
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
mkwepu jr and Mlolongo
[IMG alt="Mwalimu wa tuisheni"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/571/571457.jpg?1694634030[/IMG]
JF-Expert Member
Huyo mzungu ndo yesu...?
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
castromzena, mkwepu jr, Emen and 2 others
[IMG alt="Mwalimu wa tuisheni"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/571/571457.jpg?1694634030[/IMG]
JF-Expert Member
Swala la kuzaliwa huwa sizingatii sana
Ila ile miaka 18+ ambayo kwenye biblia haijaandikwa natamani kujua alikua anafanya nini..?
Je alikua na mademu..?
Vipi alikua sio mgomvi?
Vipi kuhusu tungi hajawahi kuonja kweli..?
Story ya yesu bado ni incomplete
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
Shadow7, digba sowey, Kamkuki and 3 others
[IMG alt="REALITY"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/233/233335.jpg?1672388028[/IMG]
JF-Expert Member
Swala la kuzaliwa huwa sizingatii sana
Ila ile miaka 18+ ambayo kwenye biblia haijaandikwa natamani kujua alikua anafanya nini..?
Je alikua na mademu..?
Vipi alikua sio mgomvi?
Vipi kuhusu tungi hajawahi kuonja kweli..?
Story ya yesu bado ni incomplete
Click to expand...
Kitabu hicho juu cha miaka 18
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
Mlolongo and Mwalimu wa tuisheni
[IMG alt="Mwalimu wa tuisheni"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/571/571457.jpg?1694634030[/IMG]
JF-Expert Member
Kitabu hicho juu cha miaka 18
Kama hautajali naomba brief story ya hiyo miaka 18
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
Mlolongo
[IMG alt="DR SANTOS"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/542/542533.jpg?1696804728[/IMG]
JF-Expert Member
Mungu hachoki hazimii Wala hachunguziki
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
Saint Anno II, Globu and Mlolongo
[IMG alt="Farolito"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/506/506259.jpg?1570437012[/IMG]
JF-Expert Member
Swala la kuzaliwa huwa sizingatii sana
Ila ile miaka 18+ ambayo kwenye biblia haijaandikwa natamani kujua alikua anafanya nini..?
Je alikua na mademu..?
Vipi alikua sio mgomvi?
Vipi kuhusu tungi hajawahi kuonja kweli..?
Story ya yesu bado ni incomplete
Click to expand...
Hata hilo usizingatie sana,kama unaamini alizaliwa duniani, akafa akafufuka na atarudi tena hio inatosha.Miaka 18 hata kama ingekuwa ni wewe(mtu wa kawaida) itachukua mrundikano wa vitabu kuandika kile ulichofanya kila siku,sasa vipi kuhusu mtu maarufu kama Yesu?
Kwanza watu wasingepata hata huo muda wa kuyaishi mafundisho yake maana wangekuwa wapo bize kujua alifanya nini huku na kule wakibadilisha vitabu na vitabu na kujadiliana,na hivyo kuwapoteza watu.
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
Shadow7 and Saint Anno II
[IMG alt="Mwalimu wa tuisheni"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/571/571457.jpg?1694634030[/IMG]
JF-Expert Member
Kwanza watu wasingepata hata huo muda wa kuyaishi mafundisho yake
Huo ndo uongo tunaokaririshwa na viongozi wetu
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
Mlolongo and REALITY
[IMG alt="Mwalimu wa tuisheni"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/571/571457.jpg?1694634030[/IMG]
JF-Expert Member
usizingatie sana,kama unaamini alizaliwa duniani, akafa akafufuka na atarudi tena hio inatosha
Haitoshi, huenda ndani ya hicho kipindi kuna code nyingi ambazo hawataki mzijue, huenda yesu alikua na skills nyingi nje ya useremala lakini wameficha
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
cale, Kamkuki and Mlolongo
[IMG alt="Carlos The Jackal"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/496/496623.jpg?1636829266[/IMG]
JF-Expert Member
Duuhh nyie vipi.
Jamaan KANISA LA RUMI, Liliamua kuitumia siku tarehe 25/12 siku alozaliwa mungu wao wa Jua wakati ule wa RUMI YA KIPAGANI , Wakaihalalisha kua siku ya Kukumbuka Kuzaliwa Kwa YESU.
YESU HAKUZALIWA TAREHE 25/12.
Nchini URUSI Kwa wa Orthodox wao wanaazimisha Tarehe 7/1 .
JAMANI YESU HAKUZALIWA TAREHE 25/12 .
nikama tunavyokumbuka siku ya 17/3 .... Lkn sio siku alolalala.
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
Interlacustrine E, Gwappo Mwakatobe, Mbabani and 2 others
[IMG alt="REALITY"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/233/233335.jpg?1672388028[/IMG]
JF-Expert Member
Hata hilo usizingatie sana,kama unaamini alizaliwa duniani, akafa akafufuka na atarudi tena hio inatosha.Miaka 18 hata kama ingekuwa ni wewe(mtu wa kawaida) itachukua mrundikano wa vitabu kuandika kile ulichofanya kila siku,sasa vipi kuhusu mtu maarufu kama Yesu?
Kwanza watu wasingepata hata huo muda wa kuyaishi mafundisho yake maana wangekuwa wapo bize kujua alifanya nini huku na kule wakibadilisha vitabu na vitabu na kujadiliana,na hivyo kuwapoteza watu.
Click to expand...
Mkuu kwanini unapenda kufikiriwa bila kufanya tafiti,fikra zako ni za nini?unatakiwa usiamini unatakiwa ujue
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
Washawasha, Suleiman mchawi WA Rhymes, Mr. Wise and 2 others
L
JF-Expert Member
Yesu wa Nazareth
WANAZUONI wengi duniani, bado wanaumiza vichwa kuhusu tarehe sahihi aliyozaliwa Yesu Kristo, ambaye ni Nabii wa Wakristo.
Miaka nenda rudi, vitabu vingi vimeandikwa na makundi ya wanazuoni wa dini na historia kuanzia Mashariki ya Kati, Amerika, Ulaya, Afrika na bado hadi leo, maandishi mapya yanaendelea kuchapishwa juu ya kuzaliwa kwa Yetu Mnazareti.
Mjadala huo upo na hakika hautakoma kwani wanaoandika wanapingana kwa hesabu na historia. Wameshindwa kupata tarehe hasa aliyozaliwa Yesu ambaye pia huitwa Masihi.
Miaka 2000 iliyopita, mtawala wa tano wa Wayahudi, Pontio Pilato alimuuliza Yesu wa Nazareti swali lifuatalo: “Ukweli ni kitu gani?”
Aliuizwa swali hili wakati anakaribia kupewa hukumu ya kuwambwa msalabani baada ya kukamatwa akituhumiwa kujiita “Mfalme wa Wayahudi.”
Yesu hakujibu swali hili. Na hadi leo, kambi kadhaa za wanazuoni zinazidi kuvutana kuhusu jawabu sahihi kwa swali hili. Mfano mzuri wa mvutano huo unajitokeza katika mjadala kuhusu “siku ya kuzaliwa kwa Yesu wa Nazareti.”
Mpaka leo, kuna siku tatu tofauti zinazotajwa kama siku za kuzaliwa kwa Yesu. Kuna Desemba 25, Januari 6 na Januari 7. Ufafanuzi wa utata huu unafuata.
Tuanze na Desemba 25. Haya ni mawazo ya Mtakatifu Hippolytus wa Roma. Kwa mujibu wa
utafiti wa Profesa Andrew McGowan wa Chuo Kiukuu cha Melbourne, mwaka 204BK, Hippolytus aliandika kwamba, “Tarehe ya kuzaliwa Yesu, Bethlehem, ni Desemba 25.”
Hippolytus alianzia kwenye tukio la Malaika Gabriel kumtokea Zakaria hekaluni na kumwambia kwamba mkewe Elizabeth angepata mimba na kumzaa Yohane.
Zakaria alikuwa kwenye ibada ya malipizi ya dhambi. Kwa mujibu wa kalenda ya Kiebrania ibada hiyo ilifanyika tarehe Julai 10 kila mwaka wa Kiyahudi.
Ulinganisho wa kalenda ya kale ya Wayahudi na kalenda ya kisasa unaonyesha kuwa siku hiyo ni sawa na Septemba 24 ya siku hizi. Hii maana yake ni kwamba Elizabeth alianza ujauzito wa Yohane Septemba 24.
Kwa mujibu wa uchambuzi wa Hippolytus, miezi sita baadaye malaika Gabriel alimtokea Bikira Maria na kumwambia atapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Hivyo, ujauzito wa Yohane ulioanza Septemba 24 uliutangulia ujauzito wa Yesu kwa miezi sita.
Hii maana yake ni kwamba, mimba ya Yesu ilianza Machi 25 na akazaliwa miezi tisa baadaye, yaani Desemba 25, anahitimisha Hippolytus.
Lakini, bado wapo Wakristo waliopinga tafsiri ya Hippolytus. Walihoji uhalali wa hesabu zake, wakitaka awaonyeshe hiyo miezi tisa ilikuwa na jumla ya siku ngapi.
Hawa wenye kupinga Krismas ya Desemba 25, huadhimisha Krismas ya Januari 7. Ni wafuasi wa Mfamle Julius Kaizari wa dola ya Kirumi. Sababu za upinzani wao zinafuata.
Katika mwaka 46KK Julius Kaizari aliunda kalenda iliyotokana na imani kwamba mzunguko wa dunia unachukua siku siku 365 tu. Lakini, baadaye wanasayansi waligundua kuwa mzunguko wa dunia huchukua siku 365 na robo.
Robo nne zinaunda mwaka mmoja. Hii maana yake ni kwamba, kila baada ya miaka mitatu, yaani katika mwaka wa nne, mzunguko wa dunia huchukua siku 366.
Miaka mitatu huitwa miaka mifupi, na mwaka wa nne kuitwa mwaka mrefu. Mwaka mrefu hugawanyika kwa namba “nne.”
Kwa mujibu wa “Kalenda ya Julius” mwaka wenye siku 365 una miezi 12; ambapo miezi minne ina siku 30, kila mmoja; miezi saba ina siku 31, kila mmoja; na mwezi Februari una siku 28.
Hesabu hizi hazihusishi siku 365 pekee kati ya siku 365 na “robo” za mzunguko wa dunia. Hivyo, kila baada ya miaka minne, “Kalenda ya Julius” ikawa inapoteza siku moja kamili.
Kwa ajili ya kuondoa dosari hii, katika kila mwaka mrefu, Julius aliamua kuongeza siku moja kwenye mwezi wa Februari, ili uwe na siku 29, na hivyo kukamilisha siku 366 za mwaka mrefu.
Kalenda hii ina miezi minne ya siku 30, miezi saba ya siku 31, mwezi Februari wa siku 28 katika mwaka mfupi, na mwezi Februari wenye siku 29 katika mwaka mrefu. Huitwa “Kalenda ya Julius”.
Baadaye wanasayansi waligundua tena kuwa mzunguko wa dunia hauchukui siku “365.25” pekee, bali huchukua siku “365.24218967.” Hapa kuna tofauti ya siku “0.00781033,” sawa na dakika “11.2468752.” Yaani, kimakosa, “Kalenda ya Julius” ilikuwa imeongeza dakika “11.2468752” katika mwaka mzima.
Kanisa Katoliki lilianza kutumia kalenda ya Liturijia inayofuata mantiki ya “Kalenda ya Julius” mwaka 325. Lakini, mwaka 1582 Papa Gregory wa 13 aligundua makosa hayo yaliyo kwenye “Kalenda ya Julius.”
Hivyo, Papa akakosoa dosari husika kwa kuunda kalenda mpya, ikaitwa “Kalenda ya Gregory”. Baadhi ya Wakristo waliikataa mantiki iliyoongoza utengenezwaji wa “Kalenda ya Gregory” na kuendelea kutumia “Kalenda ya Julius.”
Hivyo, tangu mwaka 325 hadi leo imepita miaka 1697. Kwa kuzingatia tofauti ya siku “0.00781033” tulizoona hapo awali, hesabu ya kuzidisha inaonyesha kwamba “Kalenda ya Gregory” inaitangulia “Kalenda ya Julius” kwa siku “13.25413001.” Huu ni wastani wa siku 13 na robo.
Hivyo, wakati Wakristo wanaofuata “Kalenda ya Gregory” wanaposherehekea Krismas ya Desemba 25, wale wanaofuata “Kalenda ya Julius” watasubiri hadi Januari 7, yaani siku 13 baadaye.
Lakini pia, kuna Wakristo wanapinga Krismas ya Desemba 25 na kukataa Krismas ya Januari 7, wao wanaadhimisha Krismas ya Januari 6.
Kitabu cha “
New Advent Encyclopedia,” kinasema hawa wanaoamini Yesu alizaliwa Januari 6 ni wafuasi wa Clement wa Alexandria, nchini Misri.
Clement alionyesha kwenye kitabu chake kiitwacho “Stromata,” kwamba Yesu alizaliwa “Januari 6.” Baadhi ya Wakristo walikubaliana na Clement hadi leo.
Kutokana na mkanganyiko huo wa siku aliyozaliwa Yesu Mnazareti, ndiyo maana yapo maeneo duniani yanaadhimisha kuzaliwa kwake Desemba 25, wengine Januari 6 na wapo wanaofanya kumbukizi Januari 7.
Mchungaji wa Kanisa la Mfalme Yesu lililoko Mwanjelwa, Mbeya, Ibarhim Kalembo akizungumza na Pambazuko kuhusu tarehe hasa ya kuzaliwa Yesu Kristo, alisema ni kweli kuna tofauti kulingana na maeneo husika, lakini uhakika kabisa hauelezwi kinagaubaga na Biblia yenyewe.
Amesema katika vitabu vingi vya vya Injili, ambavyo vikisomwa kwa pamoja, kuna utata wa siku ya kuzaliwa Yesu Kristo, kwani haitamkwi wala kuelezwa kwa uwazi.
“Hata wewe ni Mkristo, umewahi kusoma ama kuelezwa mahali kwamba Desemba 25 ndiyo hasa alizaliwa Mwana wa Mungu (Yesu), hakuna, lakini watu waliamua iwe hiyo Desemba 25 kwa wengi, pamoja na kwamba wapo wanaopinga tarehe hiyo,” ameongeza mchungaji huyo ambaye amesema ana shahada ya uzamili katika teolojia.
Anaeleza kuwa mvutano wa siku ya kuzaliwa Yesu huenda usifike mwisho na labda unaweza kutatuliwa na Yeye mwenyewe siku atakaporejea na endapo atatoa nafasi ya kuulizwa maswali.
“Hili swali limetushinda, limewashinda hata wakongwe wa historia ya maisha ya Yesu, wakiwamo Wayahudi wenyewe, huenda siku nzuri ya kupata jibu na tutakapomuona Mwenyewe,” ameongeza.
Chanzo: Gazeti laPambazuko, Toleo la Jumatatu, Desemba 26, 2022-Januari 1, 2023, ukurasa wa 10-12.
Click to expand...
Hii story ni nzuri kuitafakari Ila kuna jambo moja au mawili ya kurekebisha.1)Yesu siyo nabii,Ni Mungu.2)Kusherehekea Christmass ni kumbukumbu tu ya kimapokeo,hii ina muhimu kwetu sisi wakristo kwa sababu inafanya tutafakari ujio wa masihi ulivyokuwa na umuhimu wake kwa ukombozi wetu,Ila kumbuka pia wapo wanaoisherehekea sikuu hii kama sikuu ya mwisho wa mwaka.wala haijabeba umuhimu wowote wa kiroho kwao.Hao wanaweza kupoteza muda wao kuitafuta tarehe kamili ya kuzaliwa Yesu. Na kwa kuwa wote tunakubaliana Huyu Yesu,ambaye ni Mungu alikuja duniani kama mwandamu kwa kuzaliwa na Bikira Maria, kwa hiyo wale wanaoiangalia siku hii kwa jicho la Rohoni,tafakari kubwa zaidi kwao ni juu ya kuzaliwa kwake kwa ajili ya sisi wenye dhambi na Upendo wa Mungu kwetu.kwamba alizaliwa tarehe ngapi hasa, hili lina uzito mdogo zaidi ingawaje ni mtego pia wa ku-poteza focus usipokaa vizuri.
Hili ni sawa na ule mjadala wa ni ipi siku sahihi ya sabato ya juma ,je ni jumapili,jumamosi au ijumaa.Ile kwamba kuna ya saba unemeifanya na kuitoa kwa bwana kwa ajili ya kuitakasa na kuifanya ni siku ya Bwana,inatosha.siku uliyoupokea kutoka kwa waliokutangulia itunze sababu siku zote hizo tatu ni sahahi kwa kila upande.
Kumbuka ,huendi mbinguni kwa kuiheshimu pekee siku sabato wala tarehe Yesu alizaliwa,unaenda mbinguni kwa kumkiri kwa Kinywa chako na kuamini Moyoni mwako kwamba huyo Yesu ni Bwana,kwamba alizaliwa akateswa akafa na akafufuka kutoka kwa wafu pia kuzishika amri kuzitimiza amri zake kwa imani
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
Saint Anno II and dudus
[IMG alt="REALITY"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/233/233335.jpg?1672388028[/IMG]
JF-Expert Member
Kama hautajali naomba brief story ya hiyo miaka 18
Inshort yesu alienda india akiwa na miaka 14 akajiunga na buddhism akamaliza mafunzo akarudi kwao akafanya yale aliyoyafanya ila hakufa msalabani wala hakupaa alitumia supernatural powers na kuescape na kurudi india na kumaliza maisha yake.yesu hakupaa maana hakuna nafasi ya mwili kwenye ulimwengu wa kiroho ila alikuwa ni buddhah kama mimi ,wewe,dai lama,osho na wengine ,buddhah ni mtu ambaye hana dini na anaona uwepo wa Mungu bila msaada wa yeyote na ndo asili ya mtu,kwahiyo wangeandika hayo kwa biblia kanisani ungekuta patupu na biashara ya dini ingekufa.
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
Washawasha and IGWE
[IMG alt="Mwalimu wa tuisheni"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/571/571457.jpg?1694634030[/IMG]
JF-Expert Member
Inshort yesu alienda india akiwa na miaka 14 akajiunga na buddhism akamaliza mafunzo akarudi kwao akafanya yale aliyoyafanya ila hakufa msalabani wala hakupaa alitumia supernatural powers na kuescape na kurudi india na kumaliza maisha yake.yesu hakupaa maana hakuna nafasi ya mwili kwenye ulimwengu wa kiroho ila alikuwa ni buddhah kama mimi ,wewe,dai lama,osho na wengine ,buddhah ni mtu ambaye hana dini na anaona uwepo wa Mungu bila msaada wa yeyote na ndo asili ya mtu,kwahiyo wangeandika hayo kwa biblia kanisani ungekuta patupu na biashara ya dini ingekufa.
View attachment 2459867View attachment 2459869
Click to expand...
Ukiwaambia wakariri dini, kuwa hizi ni biashara kama biashara nyingine wanaona umekengeuka
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
Washawasha, REALITY and IGWE
[IMG alt="REALITY"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/233/233335.jpg?1672388028[/IMG]
JF-Expert Member
Kama hautajali naomba brief story ya hiyo miaka 18
Na kingine ukristu ulianzishwa na paul na siyo yesu,ndo maana biblia inamikanganyiko mingi rejea kitabu cha matayo,marko na luka ni luka tu ananyooka flani kuwa yesu alijengwa kwa kupitia Mungu na mtu(buddhahhood),wengine mara alipaa mara hivi na karatasi nyingi sana zimechomolewa zingine zimefichwa zingine hazijulikani wapi zilipo ni hizi chache ambazo watu wamehustle mpaka kujua ukweli alikuwa wapi 18 years
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
Reactions:
IGWE and Gavana
[IMG alt="Mwalimu wa tuisheni"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/571/571457.jpg?1694634030[/IMG]
JF-Expert Member
Mikanganyiko ni mingi mno,
Matumizi ya pombe
Ndoa za mitala
Kuchepuka
Nguvu za asili (walizoita wazungu eti ushirikina)
Thanks Quote Reply
Select for moderation
Report
1 of 9
Next Last
BoldItalicMore options…
Insert linkInsert imageMore options…
UndoMore options…
Preview
Font sizeText colorFont familyListAlignment
- Align left
- Align center
- Align right
- Justify text
Paragraph formatStrike-throughUnderlineInline spoilerInline code
SmiliesQuoteInsert videoMediaInsert tableInsert horizontal lineSpoilerCodeSubscriptSuperscript
RedoToggle BB codeRemove formattingDrafts
Write your reply...
Post reply
Attach files
Similar Discussions
Share