Krismasi za kukumbuka (sad memories)

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Ikabidi ujikatae fasta kabla akijanuka aisee maisha aya sio powa
 
Bibi yako anakaa sehemu gani? Hapo ifoza mimi pia kwa babu na bibi zangu kule.
 
Bibi yako anakaa sehemu gani? Hapo ifoza mimi pia kwa babu na bibi zangu kule.
Hata majina sikumbuki sahiv, ila alikuwa anaishi karibu na posta (zamani) pale round about (tulikuwa tunaita mwenge wa bandia) mbele kidogo. Sijui kama sahivi kuna mazingira hayo. Maana sasa yapata zaid ya miaka 25
 
Nakumbuka Christmas moja sikumbuki mwaka,sikuwa hata na mia,natamani kula vizuri na njaa inagonga mbaayaa😂😂😂,ghafla nkaona muamala,kiasi Tzs.50,000/=kutoka kwa Siafu na Manga akaniambia mkuu nmepata kiasi fulani hapa nmeona tugawane. ,Siwezi kueleza kiwango cha furaha yangu ile siku. Nkatoka nkaenda baa nkaagiza wali kuku😂😂😂,nkala nkarudi gheto. Mkuu Siafu na Manga ni Mungu tu atakulipaga.
 
Mkuu japo inaumiza Sana ila nimecheka Sana dah
 
Mwaka huo wa 1993 SIKU ya ya krismas mkuu wa wilaya ya korogwe akiitwa Margret Ndaga alitukuta njiani hatujui tuendako akatupakia na dereva wake kwenye Pajero akatupeleka kwake ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuangalia video na kula pilau ya ukweli. Huyu mama Margret Ndaga popote alipo abarikiwe.
 
Krismas ya mwaka 1992 zilitoka suruali flani za kishua Zina zipu zipu kibao Mimi nimevaa nikijua ndio ntakua wa kwanza (sitataja location) hamadi naingia street nakuta zile suruali mademu watatu wanazo copyright na yangu msela ........naishia hapa.
 
Hata majina sikumbuki sahiv, ila alikuwa anaishi karibu na posta (zamani) pale round about (tulikuwa tunaita mwenge wa bandia) mbele kidogo. Sijui kama sahivi kuna mazingira hayo. Maana sasa yapata zaid ya miaka 25
Ok napajua huko km unaelekea kivukoni. Sawa rudi sasa hivi aisee siyo ile ya miaka ya 90 huko imechangamka sana na kuendelea pia. Miye nimeamua kila mwaka narudi kukaa hata wiki moja alafu nasepa zangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…