Wakuu,
Kwa mtu ambae anataka kununua gari mtandaoni kutoka Japan na pia anataka ku-save pesa kidogo, leo kuna kitu
kidogo sana nimeona tushirikishane.
Sio kitu cha ufundi, ila ni
patience. Ukiwa unafanya survey ya gari, ukishachagua model unayotaka, nashauri usikimbilie kulipia hapo hapo. Jipe muda. Lifuatilie ilo gari ata kwa mwezi mmoja au zaidi uone bei yake inavyoshuka.
Mwezi uliopita tulikua tunafuatilia Toyota Aqua na ilishuka jumla ya $1,200 tokea tuanze kuifuatilia, ila tulichelewa kidogo kuna mtu akaiwahi.
Hapa ndio maana kuepuka hili, nashauri uwe unafuatilia magari ata matatu (ya muundo ulioutaka) kwa pamoja.
Nakupa mfano hapa (nitatumia BF na gari Mazda Axela) nitajitahidi ku-update bei ya hii gari hadi itakavyokuja kulipiwa.
Jumanne, Tar 01 October.
View attachment 3115915
Alhamis, Tar 03 October.
View attachment 3115916
Jumamosi, Tar 05 October.
View attachment 3115917
Inamaanisha ndani ya siku 5 imepungua zaidi ya laki 3.5 inamaanisha gari ikiendelea kukaa zaidi ya mwezi itashuka maradufu.
Na hapo uhakika wa kupunguziwa $150-200 upo ukiwasiliana nao.
Stay tuned.