Kua uyaone, mikoani madukani kuna kipimo cha sukari hadi ya shilingi 200, mafuta 100

Mbona hili limeanzia Dar? Siku nyingi wanapima sukari na mafuta namna hii.
 
Huku kawaida mkuu , haaa tena hapa nlipo kawaida, wafu wa dar mnajidai sana siku niende😂😂cc Fake P Dar kuna nini rafiki angu😂😂
 
Wewe unaijua Dar es salaam kweli? Au umekulia ushuani?

Kwa taarifa yako dar kuna mitaa siyo sukari ya 200 tu. Mkate unauziwa nusu au robo. Karoti, hoho, na nyanya vimekatwa unauziwa kipande.
 
Mkuu sisi huku mikoani ndio maisha yetu🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mikoani ndio wapi huko. Mimi nilishangaa kufika Dar watu wanakula utumbo wa kuku tena barabarani wakati kijijini tunawapa mbwa na paka. Dar kuna maisha magumu sana sema tu watu hawataki kuonekana wameshindwa maisha kwa kurudi vijijini.
 
Daalam hajuna sukari ya 200
Siku Moja tembelea kwenye migodi ya wachimbaji wadogo wadogo nenda migahawa au Kwa jina maarufu hoteli za masankuroni ujionee wali wa jero una kula na unabakiza!

Usiulize sana ila nakupa code
Kule chakula hakitupwi yaani ukimaliza kula na ukabakiza kidogo Basi huo uliobaki unaenda kuchanganywa na mwingine unakuwa kama mchanyato fln Hivi

Sema harufu ndo inakuwa haieleweki maana kama ulikula wali na samaki mwingine samaki,dagaa,maharage au hata na mboga za majani wote huchanganywa pamoja.

Hata chapati unaulizwa unahitaji ya sh ngap? Zinakuwa nusu nusu 😂😂😂
 
Hapa Dar nimeishaziona pakiti za sukari za sh200 product ya Bakhresa,sema hazijasambaa sana.
 
Huku jijini Mbeya ukitaka kula spaghetti basi jiandae kununua zile za kisasa kwenye packet, ila dar ukitaka kula spaghetti basi zipo zile za mafungu nakumbuka miaka ya 2010 bimkubwa alikuwa akinunua za buku tu tunakula watu kibao na Chai ya iriki asubuhi shwaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…