Kuacha kufanyika Maadhimisho ya sherehe za Miaka 61 ya Uhuru ni sahihi?

Kuacha kufanyika Maadhimisho ya sherehe za Miaka 61 ya Uhuru ni sahihi?

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Rais Samia Suluhu amesema mwaka huu hakutakuwa na sherehe za uhuru na pesa zilizokuwa zimetengwa kwaajili ya sherehe izo ziende kuimarisha sekta ya elimu wadau wengi wa maendeleo wameunga mkono maamuzi haya na kusema kuwa hili ni wazo zuri halijawai kutokea toka Tanzania ipate uhuru.

Leo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amesema "Rais Samia ameelekeza Sh. milioni 960 zilizopangwa kutumika kwenye maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru, zikajenge mabweni katika shule 8 za msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum".

Shule hizo za msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum zitakazojengewa mabweni ni Buhangija- Shinyanga, Goheko - Tabora, Darajani - Singida, Mtanga - Lindi, Songambele - Manyara, Msanzi - Rukwa.

Mungu aendelee kumuweka Rais Smaia Suluhu kwa maendeleo ya taifa letu.

=====

Rais Dk Samia aagiza fedha za sherehe za uhuru zitumike kujenga miundombinu ya shule

Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan ameelekeza Shilingi milioni 960 zilizotengwa na Wizara na Taasisi kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe za Uhuru mwaka huu, zipelekwe Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa ajili ya ujenzi wa mabweni katika shule naneza msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Disemba 5,2022 ,Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amesema kuwa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara mwaka huu 2022 zitafanyika kwa njia ya midahalo na makongamano mbalimbali yatakayofanyika katika wilaya zote hapa nchini.

“Midahalo na makongamano hayo itatanguliwa na ratiba mbalimbali kwa viongozi wa Mikoa na Wilaya kufanya shughuli za Kijamii kama vile kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali, shule, nyumba za Wazee na makundi yenye mahitaji maalum. Hivyo, sherehe za mwaka huu hakutokuwa na Gwaride na shughuli nyingine za Kitaifa,”- amesemA Simbachawene.

ameongeza kuwa “Midahalo na Makongamano hayo itatanguliwa na ratiba mbalimbali kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya kufanya shughuli za Kijamii kama vile kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali, shule, nyumba za Wazee na makundi yenye mahitaji maalum. Hivyo, sherehe za mwaka huu hakutokuwa na Gwaride na shughuli nyingine za Kitaifa.”

Simbachawene amesema kuwa Maadhimisho ya Sherehe za miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara mwaka huu 2022 yataadhimishwa kwa Kauli mbiu inayosema:- MIAKA 61 YA UHURU: AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU.

Waziri huyo ameongeza kuwa kauli mbiu hiyo inaonyesha nia ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha uchumi unaojikita katika maendeleo ya watu kwa kufanya mabadiliko katika sekta zote za kiuchumi na kijamii ili kufikisha neema na Maendeleo

Pia soma:

Dar: Yaliyojiri Maadhimisho ya Miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika Uwanja wa Uhuru

Rais Samia ashiriki Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
 
Wapunguze safari, manunuzi na matumizi ya MaV Eighty.

Hiyo Million 900 ni ya MaV Eighty mawili tu. Wasitufanye watanzania ni mazuzu. Aseme hana muda au atakuwa amechoshwa na vikao vya CCM hivyo a ahitaji mapumziko.
 
Uhuru wa Tanganyika unamhusu nini Bibi wa Kojani?.
Sahihi

Sherehe uhuru wa Zanzibar mgeni rasmi huwa raisi wa Zanzibar

Sherehe za uhuru wa Tanganyika mgeni rasmi haeleweki mtanganyika

Raisi wa Muungano sherehe inamhusu ni sherehe ya Muungano

Mama Samia yuko sahihi hadi hapo katiba itakaporekenishwa kwenye hili kuonyesha mhusika mkuu upande wa Tanganyika siku.yao ya uhuru ambaye ni mtanganyika ni nani kikatiba?

Vinginevyo pesa zote za sherehe za uhuru wa Tanganyika ziendelee kupelekwa kwenye miradi mingine iliyopo Tanganyika kama alivyofanya
 
Back
Top Bottom