Kuacha kufanyika Maadhimisho ya sherehe za Miaka 61 ya Uhuru ni sahihi?

Kuacha kufanyika Maadhimisho ya sherehe za Miaka 61 ya Uhuru ni sahihi?

Tatizo liko wapi kama mazingira ya kusomea yakiboreshwa kuliko hizo pesa zikatumike na watu wachache siku moja na hazitaludi tena sisi watanzania sijui tunatakaga nini aisee
Kati ya sherehe ya uhuru na mbio za mwenge ipi inayoghalimu pesa nyingi zaidi?
 
Rais Samia Suluhu amesema mwaka huu hakutakuwa na sherehe za uhuru na pesa zilizokuwa zimetengwa kwaajili ya sherehe izo ziende kuimarisha sekta ya elimu wadau wengi wa maendeleo wameunga mkono maamuzi haya na kusema kuwa hili ni wazo zuri halijawai kutokea toka Tanzania ipate uhuru.

Leo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amesema "Rais Samia ameelekeza Sh. milioni 960 zilizopangwa kutumika kwenye maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru, zikajenge mabweni katika shule 8 za msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum".

Shule hizo za msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum zitakazojengewa mabweni ni Buhangija- Shinyanga, Goheko - Tabora, Darajani - Singida, Mtanga - Lindi, Songambele - Manyara, Msanzi - Rukwa,

Mungu aendelee kumuweka Rais Smaia Suluhu kwa maendeleo ya taifa letu
Nia ni nini. Kuokoa billion moja? Mbona hiyo ni sawa na gharama ya magari mawili tu ya mawaziri, makatibu, maDC/RC, wakurugenzi, ma-mayor! au hayo ma V8 yanayoongozana kwenye misafara ya viongozi! So hapa ni kuwahadaa wananchi. Nadhani, kama iko nia njema, basi serikali itoke hadharani ikemee na kujutia maamuzi kwa sababu hii inatuonyesha, waziri mmoja amekalia mabweni manne ya wanafunzi. Rais wa Zambia amenukuliwa akiwaeleza watendaji wake, kama unataka kutembelea V8? nunua ya kwako. Kwa nini uchukue pesa ya kujengea mabweni manne ukawe unaitembelea kwenda kazini na kwenye bar?
Kwa hiyo, mie naona, sikukuu ingeadhimishwa ili kuendeleza kuikumbuka siku hiyo, kisha, chukua maV8 yote ya viongozi, piga mnada na kubakisha machache yatakayokuwa central govenment/commworks kwa ajili ya kutumika pala yanapohitajika. Viongozi watumie magari binafsi kama ilivyo kwa wabunge. Huwezi ukatutolea kuadhimisha siku yetu muhimu, pale majeshi yanapofanya magwaride na kuapa kwa ajili ya CiC na nchi kwa hionea huruma bilion moja ambapo haiumi kutumia billion 350 kununua magari ya anasa kwa ajili ya viongozi.
 
Tumpongeze Mama kwa Maamuzi hayo mazuri. Hakuna haja ya sherehe ya kutumia hizo pesa zote...Nadhani sherehe kama hizo zisifanyike kabisa.
 
Mwenge una maana kubwa sana katika nchi yetu then mwenge unawakilisha uhuru pia kwaiyo hata hapa ni moja ya kusherekea Rais Samia Suluhu ameona kuliko pesa kuliwa na wachache ni bora ziendelee zipeleke maendeleo kwenye jamii ambayo yatawanufaisha mamilioni ya watanzania kwa miaka mingi zaidi
Nambie maan halisi ya mwenge kwa uhalisia husika!!
 
B 900+ shule nane tuu kwa majengo haya tunayajua yanavyokuaga mmmhhhh. Mi naona Bora Zimbabwe
 
Rais Samia Suluhu amesema mwaka huu hakutakuwa na sherehe za uhuru na pesa zilizokuwa zimetengwa kwaajili ya sherehe izo ziende kuimarisha sekta ya elimu wadau wengi wa maendeleo wameunga mkono maamuzi haya na kusema kuwa hili ni wazo zuri halijawai kutokea toka Tanzania ipate uhuru.

Leo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amesema "Rais Samia ameelekeza Sh. milioni 960 zilizopangwa kutumika kwenye maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru, zikajenge mabweni katika shule 8 za msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum".

Shule hizo za msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum zitakazojengewa mabweni ni Buhangija- Shinyanga, Goheko - Tabora, Darajani - Singida, Mtanga - Lindi, Songambele - Manyara, Msanzi - Rukwa,

Mungu aendelee kumuweka Rais Smaia Suluhu kwa maendeleo ya taifa letu

Mbona sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar hazijawahi kuahirishwa na pesa kwenda kujenga skull na hospitali?

Kupuuza sherehe za Uhuru wetu ni kosa kubwa sana. Huku ni kuua U-Taifa! Siku ya Uhuru wa Tanganyika inapotea!
 
Sherehe ya nchi inayotimiza miaka 61 bila ya ubunifu wowote ni upotezaji wa pesa kwa njia za upigaji ule ule wa miaka yote.

Kama sherehe zenyewe ndio hizo za kuvunja mawe juu ya vifua vya makomandoo naona kama ni kuzinguana tu kwa sasa.

Tunaona mbwembwe za waokoaji halafu katika maisha halisi ndege inaanguka na watu wanapoteza maisha bila ya uokoaji wowote wa maana kufanyika.

Ni wazo sahihi hizo pesa kwenda kusaidia sekta nyingine kuliko kurudia matukio yale yale ya kila mwaka kiasi cha kuonekana ni wizi tu uliozoeleka.
 
Ni ngumu kuachana na mwenge sababu kuna makafara ya damu yalitolewa sababu ya mwenge. Forojo Ganze alikufa mara tu baada ya kutoka kukabidhiwa mwenge kuzimu.
Nchi imejengwa kwenye misingi ya uwongo, uzinzi, uchawi na ghiliba.
Ibada za mwenge huambatana na ulevi na zinaa
Sio kweli kwamba nchi imekabidhiwa mizimu. Tarehe 8 Desemba 1961 siku moja kabla ya uhuru nchi ilikabidhiwa kwa ulinzi wa Mama Bikira Maria na baada ya hapo Mwalimu akaikabidhi tena kwa dua za kiislam.

Usione matukio mabaya yanakuja na kuondoka tukibaki na amani ukadhani ni bahati tu huwa inatokea.

Usione vimbunga vinajikusanya baharini halafu vinatoweka tu, kuna nguvu ya ulinzi wa Mungu inayofanya kazi.
 
Nampongeza Mh. Raisi kwa usmuzi wa busara.

🇹🇿 Pamoja na nchi zinazoendelea , heshima yetu haiji kwa kufanya sherehe Bali kitu Cha kuonekana ulichokifanya.

🇹🇿Nimeona maadhimisho mengi, mengi yanatumianfedha nyingi kujenga mabanda, kuyaremba, kulipana posho, kuweka mavifaa, masherehe kula ,kulala ,unakuta taasisi zinatumia fedha nyingi kuliko hata uzalishaji wake.

🇹🇿Ningekuwa Raisi kitu ambacho sio na haiwezekani Mimi kuwa Raisi, ningefuta maonyesho yoote na maadhimisho yanayotumia fedha nyingi mpaka pale tutakapofika uchumi wa kati.

🇹🇿Hainijii akili I kukusanyika siku Moja na kufuta mabilioni ya fedha kwa siku Moja wakati unaweza kuzitumia fedha hizo kwa ajili ya kutengeneza huduma za msingi za wananchi kama hizi fedha zilizopelekwa kubotesha elimu 👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏
 
Kwa mala ya Kwanza nimemuelewa huyu Mama.Hatujawahi kupata Uhuru Sasa tunasherekea nini?? Uhuru wa Bendera.??
 
Back
Top Bottom