Kuachiwa kwa Kaijage kwarasimisha vita kati ya walosoma wakaelmika na walosoma lakini hawajaelimika

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,890
Reaction score
26,440
Mwadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma bwana Melkisedek Kaijage leo kaachiwa huru baada ya upande wa mashtaka unoiwakilisha serikali kusema kwamba hauna nia ya kuendelea na kesi hiyo ya mchongo.

Hiyo ni kesi ya mchongo kwasababu siku wanasheria wa UDOM wakihangaikia dhamana kwa ajili yake dhidi ya kosa la uchochezi, wakashtukia Kaijage akiamriwa kupelekwa mahabusu baada ya mashtaka kubadilishwa kinyemela na kuwa ni ya Ugaidi na uhujumu uchumi!

Baada ya hapo ni kisanga cha kuzungushwa na khakikisha mwadhiri huyo ataabika yeye binafsi, familia yaka na pia mwajiri wake ambae ni Chuo Kikuu cha Dodoma.

Kitendo cha kumkamata mwadhiri huyo kwa kumtuhumu kuwa na kosa la uchochezi kupitia mtandao ni kubinya haki ya kupata elimu kwa wanafunzi wake ambao ndo wategemewa kuwa think tank wetu wa baadae na ambao watakuwa wakifikiri "critically" kuhusu siasa za Tanzania na khasa siasa zisizoeleweka za wakati huu.

Pia kitendo cha kumwachia huru lakini kwa masharti ya kuripoti kituo cha polisi na pia kuwa na wadhamini wawili kutoka ndani ya Dodoma pia ni kumzuia mwadhiri huyo kutenda kazi zake kwa uhuru zikiwemo matayarisho ya lectures zake ambazo bila shaka nyingi zitakuwa ni kwa njia ya mtandao. Pia ni kukiuka haki zake za binadamu kwa kumfanya asiweze kuwa huru kwenda mahala popote ambapo patahitaji kuwa nje ya muda ambao apaswa kuripoti kituoni.

Pia kwa kutoelewa polisi na mahakama kwa kumtaka Kaijage awe na wadhamini wawili (WAISHIO Dodoma) ni kumwambia kwamba haruhusiwi kutafuta fursa zingine nje ya Dodoma kama vile ajira katika vyuo vingine zaidi ya UDOM.

Sasa mambo haya ni mfululizo wa mambo ambayo katiba ya sasa ni lazima ibadilishwe ili kila mtanganyika amuheshimu mtanganyika mwenziwe kwa kuzingatia haki za msingi zinotokana na katiba hiyo MPYA na twasema "fresh baked Constitution".

Watawala wakiwemo vyombo vya ulinzi na usalama bado waogopa kuletwa kwa katiba mpya ya nchi ambayo moja ya mambo inopaswa kuondoa ni ukikukaji wa wazi na wa makusudi wa haki za binadamu, kuthamini na kuheshimu utu wa mtu na pia kuzingatia sheria ambazo zitatungwa na bunge la wabunge wanojielewa.

Hili tukio la leo la kuachiwa kwa Kaijage ni kielelezo tosha cha tofauti kubwa iliyopo kati ya wale walosoma na wakaelimika na wale walosoma lakini wasielimike hata kwa sekunde moja.

Mtu aliesoma na akaelimika ana ile kitu twaita "Critical Thinking" kwamba ana uwezo wa kuchanganyua interpret, kuoanisha na kuchakata vigezo (facts) na taarifa (information) zilizopo ili kutoa hukumu (judgment) au uamuzi kwamba jambo fulani ni sahihi au sio sahihi yaani right and wrong.

Na hii critical thinking mtu huipata akiwa chuo kikuu pekee ambako kutakiwa kutoa ushahidi wa kile akisemacho au kukieleza.

Mtu aliesoma na hajaelimika ni yule ambae amemua kuweka "critical thinking" pembeni na kuungana na wale wasokwenda kabisa mbali kielimu wakiwemo watu wenye elimu ya msingi na wale wenye elimu za kuungaunga.

Naweza kuwa niko "wrong or right" lakini kwa sasa ipo vita na ni "real" kwamba wale walosoma na hawajaelimika ndo wale waloshika mpini huku wale walosoma wakaelimika wakiwa wameshika makali.

Je, twatokaje hapo zaidi ya kupata katiba mpya?
 
Wasomi ni kina nani na wasiosoma ila hawajaelimika ni kina nani mnayakuza mambo sana who is Kaijage in this country? Unawajua wabongo wewe atasahaulika hutaamini
 
Suali lako ni gumu kuelewa.

Na pia unaposema "who is Kaijage in this Country" wamaamisha nini?
 
Mwadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma bwana Melkisedek Kaijage leo kaachiwa huru baada ya upande wa mashtaka unoiwakilisha serikali kusema kwamba hauna nia ya kuendelea na kesi hiyo ya mchongo.

Hiyo ni kesi ya mchongo kwasababu siku wanasheria wa UDOM wakihangaikia dhamana kwa ajuli yake dhidi ya kosa la uchochezi, wakashtukia Kaijage akiamriwa kupelekwa mahabusu baada ya mashtaka kubadilishwa kinyemela na kuwa ni ya Ugaidi na uhujumu uchumi!

Baada ya hapo ni kisanga cha kuzungushwa na khakikisha mwadhiri huyo ataabika yeye binafsi, familia yaka na pia mwajiri wake ambae ni Chuo Kikuu cha Dodoma.

Kitendo cha kumkamata mwadhiri huyo kwa kumtuhumu kuwa na kosa la uchochezi kupitia mtandao ni kubinya haki ya kupata elimu kwa wanafunzi wake ambao ndo wategemewa kuwa think tank wetu wa baadae na amabo watakuwa wakifikiri critically kuhusu siasa za Tanzania na khasa siasa zisizoeleweka za wakati huu.

Pia kitendo cha kumwachia huru lakini kwa masharti ya kuripoti kituo cha polisi na pia kuwa na wadhamini wawili kutoka ndani ya Dodoma pia ni kumzuia mwadhiri huyo kutenda kazi zake kwa uhuru zikiwemo matayarisho ya lectures zake ambazo bila shaka nyingi zitakuwa ni kwa njia ya mtandao. Pia ni kukiuka haki zake za binadamu kwa kumfanya asiweze kuwa huru kwenda mahala popote ambapo patahitaji kuwa nje ya muda ambao apaswa kuripoti kituoni.

Pia kwa kutoelewa polisi na mahakama kwa kumtaka Kaijage awe na wadhamini wawili (WAISHIO Dodoma) ni kumwambia kwamba haruhusiwi kutafita fursa zingine nje ya Dodoma kama vile ajira katika vyuo vingine zaidi ya UDOM.

Sasa mambo haya ni mfululizo wa mambo ambayo katiba ya sasa ni lazima ibadilishwe ili kila mtanganyika amuheshimu mtanganyika mwenziwe kwa kuzingatia haki za msingi zinotokana na katiba hiyo MPYA na twasema "fresh baked Constitution".

Watawala wakiwemo vyombo vya ulinzi na usalama bado waogopa kuletwa kwa katiba mpya ya nchi ambayo moja ya mambo inopaswa kuondoa ni ukikukaji wa wazi na wa makusudi wa haki za binadamu, kuthamini na kuheshimu utu wa mtu na pia kuzingatia sheria ambazo zitatungwa na bunge la wabunge wanojielewa.

Hili tukio la leo la kuachiwa kwa Kaijage ni kielelezo tosha cha tofauti kubwa iliyopo kati ya wale walosoma na wakaelimika na wale walosoma lakini wasielimike hata kwa sekunde moja.

Mtu aliesoma na akaelimika ana ile kitu twaita "Critical Thinking" kwamba ana uwezo wa kuchanganyua interpret, kuoanisha na kuchakata vigezo (facts) na taarifa (information) zilizopo ili kutoa hukumu (judgment) au uamuzi kwamba jambo fulani ni sahihi au sio sahihi yaani right and wrong.

Na hii critical thinking mtu huipata akiwa chuo kikuu pekee ambako kutakiwa kutoa ushahidi wa kile akisemacho au kukieleza.

Mtu aliesoma na hajaelimika ni yule ambae amemua kuweka "critical thinking" pembeni na kuungana na wale wasokwenda kabisa mbali kielimu wakiwemo watu wenye elimu ya msingi na wale wenye elimu za kuungaunga.

Naweza kuwa niko "wrong or right" lakini kwa sasa ipo vita na ni "real" kwamba wale walosoma na hawajaelimika ndo wale waloshika mpini huku wale walosoma wakaelimika wakiwa wameshika makali.

Je, twatokaje hapo zaidi ya kupata katiba mpya?
ok.🐒
 
Back
Top Bottom