Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Habari wadau,
Hapa niko mahali fulani nasubiri kukamilisha jambo fulani na kwakuwa jambo husika linachukua muda, nimeamua kujilaza kwenye benchi nikisubiri kuhudumiwa.
Wakati nikiwa nimejilaza kwenye benchi(nimetoka shift ya usiku), nikiwaza mambo mbalimbali, likanijia wazo la kesi ya Mbowe na hapo hapo nikapata hisia kuwa huenda Mbowe leo ataachiwa.
Baada ya kupata hisia hiyo, nikanyanyuka nikaingia JF na kukutana na breaking news kuwa Mbowe kaachiwa. Hakika nimefurahi mno kwa ushindi huu wa kisiasa alioupata Mbowe,na pia nimeamini hisia za kweli zipo, na zaidi kuna uhusiano wa hisia tunazopata katika nafsi zetu na kinachoendelea katika Ulimwengu wa nje.
Hii si mara yangu ya kwanza kuwaza au kupata hisia juu ya jambo fulani na jambo husika kutokea, ila hili la Mbowe kuachiwa na watesi wake limenigusa mmo na kunifanya ni-share hii experience.
Intuition is real!
Hongera Mbowe na wenzako!
God is great!