Valuhwanoswela
JF-Expert Member
- Jun 27, 2019
- 1,229
- 1,125
Kushinda kesi ya madai ni kulipa na anayeshinda ni mdai siyo mdaiwa kwa hiyo Watanzania tufurahi na kutembea kifua mbele tu kuwa sasa deni moja kati ya mengi limelipwa. Watajwa hawana haja ya kuomba msamaha kwa tendo la ndege zetu za abiria kukamatwa mara tatu katika muda mfupi kumetia doa baya sana kibiashara maana abiria wa nchi za nje wataogopa kusafiri na ATCL. Pia biashara ya usafiri wa anga unaendeshwa kwa kukopa, mfano, mafuta ya ndege hutembei nayo kwenye madumu, vyakula unakuwa na kampuni maalum ya catering kutoa huduma hiyo, nk kwahiyo kama tuna tabia kutolipa madeni, nao wataogopa kutoa huduma ili kuepuka kuburuzana mahakamani.Ndugu zangu,
Takribani majuma mawili yaliyopita Waziri wa Mambo ya nje Prof.Palamaganda Kabudi aliutaarifu Umma kutokea Dodoma siku ambayo Rais Magufuli alikuwa na kazi ya kikatiba kuwaapisha mabalozi wetu.
Prof.Kabudi alimuelezea rais huku akieleza jinsi ambavyo wananchi wa Tanzania watauchukua ushindi dhidi ya kaburu Stein kwa mara nyingine baada ya ''kumcharaza'' katika mahakama ya Gauteng kule bondeni (Afrika ya kusini).
Aliyekuwa wa kwanza kubeza ni Ndugu Membe huku akiaminisha umma kuwa Prof.Kabudi hatafanikiwa, akishauri kuwa njia pekee ni kumuita mkulima Stein kwenye meza na ''kumlipa chake. Ajizi nyumba ya njaa naye Tundu Lissu na Fatuma Karume wakauvagaa mkenge huku akiwa hawana uzoefu wowote na mashauri katika korti ya kimataifa, walijaribu kuwaapooza wafuasi wao ambao walikuwa wenye hasira nyingi baada ya kushauriwa vibaya kujitoa uchaguzi wa serikali za mitaa.
Bila kuchelewa, wafuasi wa CHADEMA na wanasiasa hao wakaivagaa mitandao huku wakionesha dharau kwa Prof.Kabudi na Watanzania, wakisema Mkulima Stein ni ''kiboko'' wakiowanukuu Lissu,Fatuma na Membe.
Wanasheria wetu wazalendo walinyamaza kimya huku wakiandaa hoja za kumshinda ''Mkulima Stein'' kortini. Kwa hoja zilizotolewa kortini hatimaye siku mbili zilizopita Mahakama ya Canada iliipa Tanzania ushindi kwa mara nyingine tena huku ikiweka ''precedence'' kwa siku zijazo.
Nimalize tu kwa kusema, Hongereni wananchi wazalendo wa Tanzania, Mmeshinda tena!