Kuajiriwa vs Kujiajiri kipi Bora? Mdau karibu utupe maoni yako

Kuajiriwa vs Kujiajiri kipi Bora? Mdau karibu utupe maoni yako

Naomba maoni yako hapo chini je kati ya Kujiajiri au kuajiriwa ni kipi una prefer na ni kwanini?
Hata ajira nayo ni biashara kwani kule “unauza” muda na skills zako

What matters ni nini unaingiza mwisho wa mwezi kama net profit. Kuna watu wamejiajiri ila honestly ni kama wapo kwenye ajira tu na wanapaswa kutafuta kazi inayolipa zaidi
 
Kama hujasoma au umesoma kozi haina ajira, utaishia kusema kujiajiri kuna faida...
Ila ukweli ni kwamba mshahara wa serikali ni mtamu sana, hauna stress hauna presha... Ufanye vizuri ufanye vibaya mwisho wa mwezi unapokea...
Kama ni kuajiriwa ni utumwa basi kujiajiri ni Utumwa namba 1, maanina kila siku naamka saa 11 nafungua biashara saa 1.00 asubuhi naanza kujichekesha na kubembeleza wateja ili wanunue bidhaa... Biashara ni headache
 
Naomba maoni yako hapo chini je kati ya Kujiajiri au kuajiriwa ni kipi una prefer na ni kwanini?

Binafsi, naona kujiajiri kuna faida kubwa zaidi kwa muda mrefu. Ingawa kuna hatari na changamoto, fursa ya uhuru na kuongeza kipato bila kikomo inafanya iwe chaguo la kuvutia zaidi. Inakupa uwezo wa kuunda thamani yako mwenyewe na kudhibiti hatima yako ya kifedha.
Hata hivyo, kuna njia nyingi za kuanza. Unaweza kuanza kwa kufanya kazi kwa kuajiriwa huku ukijifunza na kutunisha mtaji kwa ajili ya biashara yako ya baadaye. Hii inakupa fursa ya kupata uzoefu na usalama wa kifedha wakati unaweka misingi ya kujiajiri kwako.
Kwa hiyo, muhimu siyo tu kuchagua kati ya "kujiajiri" au "kuajiriwa," bali ni kupanga mikakati inayolingana na wewe ili uweze kufikia malengo yako ya muda mrefu.
Wewe unaona ni njia ipi itakufaa zaidi kwa sasa, na kwa nini?
 
Kuajiriwa ni risk free

Ila kujiajiri ni kutafuta kisukari ila kama ikilipa inalipa kweli na ukipoteza unapoteza kweli
Low or no risk wote duniani hawana hela.The lower the risk , the lower the retun (risk aversers)
 
Kujiajiri ni best japo kwa Tz hii yenye mrundikano wa kodi ni shida sana. Kila mtu anataka anufaike na unachokifanya.
Nimeshangaa eti Scania box 6*4 p 410 ya 2012 wanataka kodi 82m uchakavu tu 10,000 usd kweli hiyo Nchi ndio maana watu wanakwepa sana kodi aisee vitu vya msingi wao wanavitia kodi kubwaa ila wafanye wachache..
 
ukiwa katikati ya harakati za kujiari, unashangaa mbona watawala hawataki, kulisikia hili jambo?

utaona wanasema vijana jiajirini then wao, wanafariki bado wakiwa na ajira zao.
 
KUJIAJIRI KUNALIPA.HATA WALIOAJIRIWA BAADHI HUACHA KAZI ILI KUJIAJIRI BAADA YA KUPATA MTAJI.
 
Kujiajiri ni bora sababu kuna watu wanaacha kuajiriwa ili wakajiajiri ila sijawahi ona mtu anaacha biashara zake eti ili aende kuajiriwa mifano iko mingi hata wachekeshaji wengi bongo walikuwa walim wakaacha ili wajiajiri na vipaji vyao na wametoboa wameacha wengi walioajiriwa wako hoi na ajira zao
 
Mimi nipo upande wa kujiajiri kwa sababu zifuatazo.
1. Kwanza nipo huru na kazi yangu tofauti na kuajiriwa.mfano muda wa kufungua kazi

2. Kuepuka kulele na kero kwa boss kwa ambao wameajiriwa wanekewa kelele unazo pigiwa 😂😂. Na muda mwingine unakuta boss n mdogo kwako alafu anakugombeza kama mtoto.

3.kutengeneza kipato kikubwa . Kwa mfano mtu ambaye ameajiriwa anazalisha pesa ambayo yy inato faida kwa boss na mshahara wako.NB kwa kitu ambacho atawewe unaweza fanya ni vizuri ukafanya wew ili faida iwe kwako yote. Lakin mtaji ndio tatizo kubwa kwa sisi watu wengi.

4.kuongeza ubunifu kwenye biashara yako kwa sababu siyo kila boss anapoke ushauri wa mfanyakazi wake. Lakin kazi ikiwa yako utaboresha wew mwenyw

NA SUPPORT KUJIAJIRI KWA ASILIMIA 💯
Kaka IQ yako Ina range above average 🙌🏻🙌🏻
 
Niliwahi kuwaambia wanangu kwamba...
Mafanikio yapo kwenye bidii na bahati.
Lakini sio kila mwenye bidii ni lazima atafanikiwa.
But, ukiwa na bahati ukaongeza bidii basi itakusogeza haraka kwenye mafanikio.
Na......
Kuajiriwa ama biashara hakukupi uhakika wa kufanikiwa.
Mafanikio yanatokea kwenye inner cycle ya maisha yako daily
Yeah nadhani success has no guarantee, anyone can become successful as long as mazingira yana support na pia you have good plan and action to your plan effectively nothing can't be archived with a smart mindset
 
Inategemea na drive (motivation ) yako
Kama huna ndoto kubwa (ajiriwa).

Ukiwa umezaliwa na ndoto kubwa za kipato,mandinga makali,nyumba kubwa kubwa ,financial freedom,generational wealth,Exploration of the world,watoto wakali....roho inapenda etc etc (Jiajiri)

Hata kwenye dini sijawahi kusikia tajiri aliyeajiriwa (except wanasiasa wa Africa ,you know what i mean here)
Wenye ndoto kubwa wote...whether we like or not duniani ni risk takers,hata hao wazungu waliokuja kutukamua huku,wakatembea baharini miezi kadhaa kwenye mawimbi makubwa ,wakatoboa wakalijua dark planet wakafanikisha kupata madini,vilimo vya mazao ya biashara na mikataba feki ni risk takers,ambao walilipwa na utajiri mkubwa na kujenga mitaa mikubwa ulaya!!
Ndugu wewe ni mfia dini?
 
Binafsi, naona kujiajiri kuna faida kubwa zaidi kwa muda mrefu. Ingawa kuna hatari na changamoto, fursa ya uhuru na kuongeza kipato bila kikomo inafanya iwe chaguo la kuvutia zaidi. Inakupa uwezo wa kuunda thamani yako mwenyewe na kudhibiti hatima yako ya kifedha.
Hata hivyo, kuna njia nyingi za kuanza. Unaweza kuanza kwa kufanya kazi kwa kuajiriwa huku ukijifunza na kutunisha mtaji kwa ajili ya biashara yako ya baadaye. Hii inakupa fursa ya kupata uzoefu na usalama wa kifedha wakati unaweka misingi ya kujiajiri kwako.
Kwa hiyo, muhimu siyo tu kuchagua kati ya "kujiajiri" au "kuajiriwa," bali ni kupanga mikakati inayolingana na wewe ili uweze kufikia malengo yako ya muda mrefu.
Wewe unaona ni njia ipi itakufaa zaidi kwa sasa, na kwa nini?
AI generated content must be used effectively note points but don't take everything from it I might say Kuna IQ ya kiroboto imetembea hapa
 
Nimeshangaa eti Scania box 6*4 p 410 ya 2012 wanataka kodi 82m uchakavu tu 10,000 usd kweli hiyo Nchi ndio maana watu wanakwepa sana kodi aisee vitu vya msingi wao wanavitia kodi kubwaa ila wafanye wachache..
Kodi ni mzigo mkubwa sana sijui hawafanyi tathmini kila baada ya muda, misamaha ya kodi nayo inawaangukia wenye nazo. Hii nchi ukipata fursa ya kuikimbia ni nafuu zaidi.
 
Back
Top Bottom