Kuajiriwa vs Kujiajiri kipi Bora? Mdau karibu utupe maoni yako

Naomba maoni yako hapo chini je kati ya Kujiajiri au kuajiriwa ni kipi una prefer na ni kwanini?
Hata ajira nayo ni biashara kwani kule β€œunauza” muda na skills zako

What matters ni nini unaingiza mwisho wa mwezi kama net profit. Kuna watu wamejiajiri ila honestly ni kama wapo kwenye ajira tu na wanapaswa kutafuta kazi inayolipa zaidi
 
Kama hujasoma au umesoma kozi haina ajira, utaishia kusema kujiajiri kuna faida...
Ila ukweli ni kwamba mshahara wa serikali ni mtamu sana, hauna stress hauna presha... Ufanye vizuri ufanye vibaya mwisho wa mwezi unapokea...
Kama ni kuajiriwa ni utumwa basi kujiajiri ni Utumwa namba 1, maanina kila siku naamka saa 11 nafungua biashara saa 1.00 asubuhi naanza kujichekesha na kubembeleza wateja ili wanunue bidhaa... Biashara ni headache
 
Naomba maoni yako hapo chini je kati ya Kujiajiri au kuajiriwa ni kipi una prefer na ni kwanini?

Binafsi, naona kujiajiri kuna faida kubwa zaidi kwa muda mrefu. Ingawa kuna hatari na changamoto, fursa ya uhuru na kuongeza kipato bila kikomo inafanya iwe chaguo la kuvutia zaidi. Inakupa uwezo wa kuunda thamani yako mwenyewe na kudhibiti hatima yako ya kifedha.
Hata hivyo, kuna njia nyingi za kuanza. Unaweza kuanza kwa kufanya kazi kwa kuajiriwa huku ukijifunza na kutunisha mtaji kwa ajili ya biashara yako ya baadaye. Hii inakupa fursa ya kupata uzoefu na usalama wa kifedha wakati unaweka misingi ya kujiajiri kwako.
Kwa hiyo, muhimu siyo tu kuchagua kati ya "kujiajiri" au "kuajiriwa," bali ni kupanga mikakati inayolingana na wewe ili uweze kufikia malengo yako ya muda mrefu.
Wewe unaona ni njia ipi itakufaa zaidi kwa sasa, na kwa nini?
 
Kuajiriwa ni risk free

Ila kujiajiri ni kutafuta kisukari ila kama ikilipa inalipa kweli na ukipoteza unapoteza kweli
Low or no risk wote duniani hawana hela.The lower the risk , the lower the retun (risk aversers)
 
Kujiajiri ni best japo kwa Tz hii yenye mrundikano wa kodi ni shida sana. Kila mtu anataka anufaike na unachokifanya.
Nimeshangaa eti Scania box 6*4 p 410 ya 2012 wanataka kodi 82m uchakavu tu 10,000 usd kweli hiyo Nchi ndio maana watu wanakwepa sana kodi aisee vitu vya msingi wao wanavitia kodi kubwaa ila wafanye wachache..
 
ukiwa katikati ya harakati za kujiari, unashangaa mbona watawala hawataki, kulisikia hili jambo?

utaona wanasema vijana jiajirini then wao, wanafariki bado wakiwa na ajira zao.
 
KUJIAJIRI KUNALIPA.HATA WALIOAJIRIWA BAADHI HUACHA KAZI ILI KUJIAJIRI BAADA YA KUPATA MTAJI.
 
Kujiajiri ni bora sababu kuna watu wanaacha kuajiriwa ili wakajiajiri ila sijawahi ona mtu anaacha biashara zake eti ili aende kuajiriwa mifano iko mingi hata wachekeshaji wengi bongo walikuwa walim wakaacha ili wajiajiri na vipaji vyao na wametoboa wameacha wengi walioajiriwa wako hoi na ajira zao
 
Kaka IQ yako Ina range above average πŸ™ŒπŸ»πŸ™ŒπŸ»
 
Yeah nadhani success has no guarantee, anyone can become successful as long as mazingira yana support na pia you have good plan and action to your plan effectively nothing can't be archived with a smart mindset
 
Ndugu wewe ni mfia dini?
 
AI generated content must be used effectively note points but don't take everything from it I might say Kuna IQ ya kiroboto imetembea hapa
 
Nimeshangaa eti Scania box 6*4 p 410 ya 2012 wanataka kodi 82m uchakavu tu 10,000 usd kweli hiyo Nchi ndio maana watu wanakwepa sana kodi aisee vitu vya msingi wao wanavitia kodi kubwaa ila wafanye wachache..
Kodi ni mzigo mkubwa sana sijui hawafanyi tathmini kila baada ya muda, misamaha ya kodi nayo inawaangukia wenye nazo. Hii nchi ukipata fursa ya kuikimbia ni nafuu zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…